Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Tuambie wewe nani alipaswa kuwa Mkuu wa Majeshi? Maana Mabeyo wakati JPM anaingia tayari alikuwa ni moja ya makamanda wa ngazi ya juu kabisa jeshini wala si kwa kubebwa na Magufuli!

..Mabeyo aliteuliwa wakati ameshavuka umri wa kustaafu.

..Jiwe alikuwa hafuati sheria na taratibu. Mfano mwingine ni jinsi alivyomteua Dr.Bashiru kuwa Kmk.
 
..Davis Mwamunyange kazaliwa 1959.

..Venance Mabeyo kazaliwa 1956.

..Mwamunyange alipostaafu Jiwe akamteua Mabeyo.

..Sasa hamuoni kuna tatizo hapo?

Cc Nguruvi3, sambulugu

Mkuu haiwezekani 1959 kuwa ndio mwaka aliozaliwa jenerali mstaafu Davis adolf Mwamunyange, Mwamunyange amepewa nyota yake ya kwanza JWTZ mwaka 1973 batch moja na luteni jenerali Abdurahaman Amir Shimbo

Abdurahman Amir Shimbo na Davis Adolf Mwamunyange wameingia kwa pamoja vyote viwili yaani mafunzo ya awali ya kijeshi (RTS) na uafisa kadeti (ni coursemates kwenye kuingia kwenye uaskari pamoja na uafisa)
 
Binafsi hii imenishangaza baada ya kusikiliza mahojiano
Baada ya mheshimiwa kufariki ni kama kulikuwa na sintofahamu ya nini kinatakiwa kifanyike na kwa wakati gani
Rais wa marekani alipo uwawa tu masaa machache makamu aliapishwa tena ndani ya ndege
 
Jamaa ameongea mengi, mengine angebaki nayo tu..

Hii inaonyesha wale wapumbavu wote waliosimama majukwaani wakisema "raisi yuko vizuri na anaendelea na majukumu yake" hawajui chochote na ni makapuku tu kama sisi wananchi...Yani kumbe nchi Ina kama ka-kamati Cha watu wanaopanga Mambo yaendaje??
 
Binafsi hii imenishangaza baada ya kusikiliza mahojiano
Baada ya mheshimiwa kufariki ni kama kulikuwa na sintofahamu ya nini kinatakiwa kifanyike na kwa wakati gani
Rais wa marekani alipo uwawa tu masaa machache makamu aliapishwa tena ndani ya ndege
Marekani wamekufa Marais wanne wakiwa madarakani,Wana experience kidogo..

Ila walivyoona raisi anaumwa tu ilibidi waanze kuchukua hatua
 

..Cdf na CoS wanastaafu wakiwa na miaka 60.

..kwa hiyo bado Mabeyo aliteuliwa akiwa ameshapitisha umri.
 
Binafsi hii imenishangaza baada ya kusikiliza mahojiano
Baada ya mheshimiwa kufariki ni kama kulikuwa na sintofahamu ya nini kinatakiwa kifanyike na kwa wakati gani
Rais wa marekani alipo uwawa tu masaa machache makamu aliapishwa tena ndani ya ndege
Kwa Tanzania, hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Rais kufia madarakani.

Kwa Marekani, ni marais 8 ambao wamefia wakiwa madarakani.

Marekani wana uzoefu juu ya hilo. Tanzania tumeupata uzoefu huo miaka 3 tu iliyopita.

Tujipe nafasi ya kujifunza kuhusu matukio kama hayo.
 
Msaada Mr Nyani, hakuna namna ya kuweza kuitoa hiyo video kwenye youtube format?
 
Sio kwa kiwango unachotaka kufikiria kiongozi
Hali ya rais ilikuwa inajulikana kwa viongozi wa juu ila wakati kifo chake kinatokea wengine hawakuwepo eneo la tukio
 
No 5 nimekuelewa saanaaaa yaani Dah
 
Wewe nae hujawahi kulia? Kulia ni kawaida
 

..Mwamunyange ilikuwa aastaafu mwaka 2016 maana yake huo ndio mwaka aliotimiza miaka 60. Hivyo basi ni sahihi kusema Mwamunyange alizaliwa mwaka 1956.

..Taarifa za kwenye mitandao zinasema Mabeyo amezaliwa mwaka 1956. Yaani mwaka mmoja na Mwamunyange.

..Hoja yangu bado inasimama kwamba kulikuwa na walakini ktk uteuzi wa Mabeyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…