Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Kweli….si umemsikia hata Jenerali Mabeyo kasema kuwa Rais Magufuli alimwambia [CDF] awaamuru madaktari wamrudishe nyumbani lakini akasema hana mamlaka hayo.

Magufuli akashangaa kwa nini CDF hawezi kuwaamuru hao madaktari wamrudishe nyumbani. Jenerali akasema hilo ni suala la madaktari na siyo CDF.

Magufuli alikuwa anadhani kwa vile Mabeyo ni CDF, basi anaweza kutoa amri kwa yeyote yule na ikatekelezwa.

Kwa kuangalia tu juu juu, Mabeyo anaonekana kama ni mtu mwenye sense.

At least that’s how he came across in the interview.
Jeshi sio kikundi cha kwaya ngabu.

Kiraia unaona jamaa alikuwa sahihi 100%kijeshi lilikuwa kosa kubwa kabisa kama alimjibu hivyo,huo ni mgomo wa wazi kabisa.labda kama alimjibu vingine kumridhisha kisha leo anatwambia hivi ni sawa.
Kama lilikuwa swala la kutumia mamlaka basi hata hao madaktari lilikuwa nje ya uamuzi wao maana mgonjwa haamui akaugulie wapi ikiwa bado hali yake hairidhishi ukizingatia ni rais wa nchi,bado hata wao wangebaki njiapanda.
 
Kwa kauli yake ‘anadhani kuna wakati washauri wake wanampa ushauri mmbaya’ (hiyo ni cue tosha), juu ya mtazamo wake wa siasa za sasa. Sema kamalizia na diplomatic language tu anashirikisha watu wengi kwenye maamuzi yake na anafanya kazi nzuri.

Tukumbuke kwa sasa general ni mstaafu na wala awezi kuwa na open opinion kuhusu siasa ata angekuwa bado CDF leo; na akuwa na upande kwenye interview yake.

Lile chozi akielezea siku za mwisho za marehemu ndio limenishangaza kuna kitu emotionally kinamsumbua na kile kifo.

Ni swali tu sijahitimisha sababu itakuwa nini ukizingatia ni ngumu sana watu wa level yake kuonyesha public emotions.
Kwa nini walimnyima Magufuli nafasi ya kuonana na familia yake
 
...hao madaktari...
Wale madaktari ni askari ama si askari? Kwenye hiyo, hospitali wanafanya kazi madaktari wa kawaida kweli mahali ambapo, CDF mstaafu anasema si rahisi kwenda, ona Hata Mama Janeth 'hakuruhusiwa' kwenda huko(kwa mujibu wa maelezo ya Jenerali, Mama hakuwa hospitalini)!

Bado unadhani wale ni madaktari wa kawaida??? Unashangaaje mshangao wa Hayati Magufuli katika hili?? Tutoe kwenye mshangao Mkuu. Timing ya interview inaweza kuwa imekosewa, Nawaza.

Naweza kutokuwa sahihi,pia.
 
Swali ni kwa nini makamu wa rais hakujulishwa mbele ya waziri mkuu au katibu mkuu??
Pia kama tuliosoma cuba ni rahisi kujua kuwa kulikua na mvutano mkubwa nani awe rais... ni ujasiri wa cdf ndio uliwezesha haya yote. Pia ingekua rahisi kama rais angeapishwa bila gwaride la kupandisha bendera ya amiri jeshi mkuu jeshi kuchukua nchi ila cdf akawa na msimamo...
 
..Cdf na CoS wanastaafu wakiwa na miaka 60.

..kwa hiyo bado Mabeyo aliteuliwa akiwa ameshapitisha umri.
Hujui sheria za jeshi kaa kimya

Kwa kawaida, sheria za jeshi huwa na masharti maalum kuhusu umri wa kustaafu. Hata hivyo, kuna hali ambapo jeshi linaweza kuongeza muda wa utumishi kwa wanajeshi baada ya kufika umri wa kustaafu kutegemea na mahitaji ya kimkakati au sera za kijeshi za nchi. Hii mara nyingi hufanyika kwa kuzingatia uwezo na uzoefu wa wanajeshi walio katika huduma.
 
Kweli….si umemsikia hata Jenerali Mabeyo kasema kuwa Rais Magufuli alimwambia [CDF] awaamuru madaktari wamrudishe nyumbani lakini akasema hana mamlaka hayo.

Magufuli akashangaa kwa nini CDF hawezi kuwaamuru hao madaktari wamrudishe nyumbani. Jenerali akasema hilo ni suala la madaktari na siyo CDF.

Magufuli alikuwa anadhani kwa vile Mabeyo ni CDF, basi anaweza kutoa amri kwa yeyote yule na ikatekelezwa.

Kwa kuangalia tu juu juu, Mabeyo anaonekana kama ni mtu mwenye sense.

At least that’s how he came across in the interview.
Kilichonishangaza hata Magufuli hakuwa na mamlaka ya kuwaamrisha Madaktari
 
Wale madaktari ni askari ama si askari? Kwenye hiyo, hospitali wanafanya kazi madaktari wa kawaida kweli mahali ambapo, CDF mstaafu anasema si rahisi kwenda, ona Hata Mama Janeth 'hakuruhusiwa' kwenda huko(kwa mujibu wa maelezo ya Jenerali, Mama hakuwa hospitalini)!

Bado unadhani wale ni madaktari wa kawaida??? Unashangaaje mshangao wa Hayati Magufuli katika hili?? Tutoe kwenye mshangao Mkuu. Timing ya interview inaweza kuwa imekosewa, Nawaza.

Naweza kutokuwa sahihi,pia.
Isikilize tena interview.

1. Prof. Janabi na Prof. mwingine jina limenitoka, nao walikuwepo. Hawa na raia wa kawaida.

2. Hata kama madaktari wote wangekuwa ni wanajeshi, huwezi tu ukatoa amri ya kibabe ku override ushauri wa kitaalamu.
 
Swali ni kwa nini makamu wa rais hakujulishwa mbele ya waziri mkuu au katibu mkuu??
Pia kama tuliosoma cuba ni rahisi kujua kuwa kulikua na mvutano mkubwa nani awe rais... ni ujasiri wa cdf ndio uliwezesha haya yote. Pia ingekua rahisi kama rais angeapishwa bila gwaride la kupandisha bendera ya amiri jeshi mkuu jeshi kuchukua nchi ila cdf akawa na msimamo...
Swali ni nani alipaswa kumpa habari za kifo makamu? Je ni katibu mkuu au waziri mkuu? Na hawakuwepo dar. Au ilibidi janab apige simu kwa makamu moja kwa moja kumpa taharifa alafu makamu atangaze bila serikali na vyombo vya usalama kujipanga? Kwa maoni yangu walikua sawa kuweka mambo vizuri kabla ya kumpa taharifa ya kutangaza. Ata hizo safari unaweza kuta ni kwa ajili ya kujipanga na makamu alijua kila kitu
 
Kumbe mtaala wa kujifunzia lazima autunge mwanafunzi mwenyewe?

Kwa nini tusijifunze kutokana na uzoefu wa wengine?

^Why isn't you seatbelt on?^

^'Cause I never had an accident.^

Halafu kule kwenye anga za CJ wanasema ^Tumetoa adhabu kali ili iwe funzo kwa...^
Kujifunza kinadharia na kujifunza kwa vitendo ni vitu viwili tofauti kabisa.

Uzoefu wa kujifunza kwa vitendo huwa ndo mwalimu mzuri zaidi.
 
Back
Top Bottom