Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Wewe ni tahira,
Mabeyo amesema saa ngapi alirudishwa nyumbani!?
Mabeyo amasema walikataa kumrudisha nyumbani hiyo aliyosema walimrudisha nyumbani iko wapi!?
Waweze kumpeleka nairobi washindwe kumpeleka south!?
Lissu alipelekwa nairobi kwa sababu tu za liusalama, hakuna hiyo huduma bora mpaka raisi apelekwe
Unaijua Nairobi Hospital lakini?
 
Tuliongozwa na 'Busara' za Jenerali Mabeyo, kungeweza kutokea matatizo makubwa sana.

AG (Mwanasheria Mkuu) alitakiwa asimame kutafsiri na kuelekeza Katiba inatamka nini na kama haitamki kisheria kipi kinafanyika.

Makamu wa Rais alipaswa kuapishwa usiku saa 6 na si kusubiri siku 3 au kujiuliza viongozi watapokewaje.

Rais yupo mahututi yupo na CDF, IGP na DGIS , Makamu na Waziri mkuu wanahanja hanja! ni hatari sana.

Jamani tuacheni ubishi, tukaeni chini na kutengeneza katiba ili tupate sheria zenye miongozo
Kusema eti hatuna uzoefu kama Marekani si kweli. Tulitakiwa tutumie uzoefu wa Marekani kufanya vizuri

Ni kama vile 'tunajitahidi kutengeneza kompyuta yetu from the scratch ' badala ya kutumia zilizopo kupiga hatua

Hii interview imeeleza mambo mengi sana
Nani analeta ubishi hapa?

Ni kweli hatukuwa tumewahi kufiwa na Rais aliyepo madarakani!

Marekani wali handle kivipi walipofiwa na Rais aliyepo madarakani ilipotokea mara ya kwanza? Ilikuwa mwaka gani? Kila kitu kilienda sawa? Hawakujifunza chochote kutokana na hilo tukio la kwanza? Hawakubadili chochote toka kwenye tukio la kwanza hadi tukio la nane?

Unaweza ukaweka kitu vizuri sana kwenye maandishi lakini inapokuja kukitekeleza kwa vitendo, unakutana na mengine ambayo hukuwa umeyafikiria.

Ndiyo, kujifunza kutoka kwa wengine ni vizuri. Lakini pia, dynamics za matukio hazifanani.

Na ndo maana nasema experience hii ni fursa nzuri ya kujifunza na kurekebisha pale palipokosewa.

Huwezi kuiga kila kitu cha kwenye makaratasi kutoka Marekani halafu udhani kwamba tukio likitokea kwako, basi hakutakuwa na kwikwi katika kutekeleza kile ulichopanga.

Hata leo hii bado Wamarekani huwa wanakosea hata kwenye uapishaji wa Rais wao.

Mwaka 2009 Obama aliapa mara mbili kwa sababu ya kosa lililokuwepo kwenye kiapo cha kwanza.

Imagine wanarudia tukio kwa mara ya 44 na bado makosa yanakuwepo, seuze sisi kwa tukio la mara ya kwanza?

Likija kutokea tena tukio la Rais kufia madarakani halafu kukawa tena na makosa yaleyale yaliyofanywa kipindi cha tukio la kwanza, hapo itakuwa sawa kulalamika.

Kwa tukio la kwanza, I cut them some slack.

Hata katiba ya Marekani imefanyiwa marekebisho kwa zaidi ya mara 20! Kwa nini?
 
Kumbe mtaala wa kujifunzia lazima autunge mwanafunzi mwenyewe?

Kwa nini tusijifunze kutokana na uzoefu wa wengine?

^Why isn't you seatbelt on?^

^'Cause I never had an accident.^

Halafu kule kwenye anga za CJ wanasema ^Tumetoa adhabu kali ili iwe funzo kwa...^
Nadharia na uhalisia ni vitu tofauti sana.

Kujifunza toka kwa wengine ni nadharia tu. Tukio likikutokea wewe, huo ni uhalisia.

Na dynamics za wengine, haziwezi kufanana na za kwako.

Safari ijayo likitokea tena, unataka tuige Wamarekani wanafanyaje au tufanye vile itufaavyo kutokana na uzoefu wetu kwa kutumia taratibu zetu?
 
Jeshi sio kikundi cha kwaya ngabu.

Kiraia unaona jamaa alikuwa sahihi 100%kijeshi lilikuwa kosa kubwa kabisa kama alimjibu hivyo,huo ni mgomo wa wazi kabisa.labda kama alimjibu vingine kumridhisha kisha leo anatwambia hivi ni sawa.
Kama lilikuwa swala la kutumia mamlaka basi hata hao madaktari lilikuwa nje ya uamuzi wao maana mgonjwa haamui akaugulie wapi ikiwa bado hali yake hairidhishi ukizingatia ni rais wa nchi,bado hata wao wangebaki njiapanda.
Hivi, wewe unaona ni sawa Rais akimwamuru mkuu wa majeshi atume kikosi cha jeshi nyumbani kwako kije kiwatandike risasi mpaka mfe? Mkuu wa majeshi akisema hapana, hiyo siyo amri halali, atakuwa amekosea?

Una akili za ajabu sana.
 
In the whole world, hakuna anayekubaliana na mambo yote. Hata JPM, kuna waliompinga na waliomkataa.
Wamekataliwa mitume na manabii...
Naposema watanzania namaanisha mimi na wengine waliomkubali.
Sio lazima na wewe uwemo kwenye kundi na haijalishi. Kipendacho roho....
Ok, sentensi yako ingekaa vizuri kama ungesema baadhi ya nyie watanzania mnataka kujua.
 
Nimesema kama mpaka wale walio juu wanaganga njaa, hawaheshimu hata viapo walivyoapa. Hawana ethics za kazi....what else has remained?

Tusijifananishe na Marekani. Hii njaa yetu ni ya next level 🤣🤣🤣🤣
Hivi huko Marekani huwa hawakosei?

Katiba yao imefanyiwa marekebisho mara ngapi?

Na kwa nini katiba yao imefanyiwa marekebisho?

Na toka kwa Rais wa kwanza aliyefia madarakani mpaka Rais wa nane aliyefia madarakani, taratibu zao ni zilezile, hazikuwahi kufanyiwa maboresho au marekebisho?

Na kama zilifanyiwa marekebisho, ni kwa nini?

Marekani ilifanya kila kitu kwa usahihi kuanzia kifo cha Rais wa kwanza aliyefia madarakani mpaka kifo cha nane?
 
Ni mnyenyekevu na mcha Mungu...anamlilia rafiki yake...kama Yesu alivyomlilia Razalo na kumfufua...
 
Hujui sheria za jeshi kaa kimya

Kwa kawaida, sheria za jeshi huwa na masharti maalum kuhusu umri wa kustaafu. Hata hivyo, kuna hali ambapo jeshi linaweza kuongeza muda wa utumishi kwa wanajeshi baada ya kufika umri wa kustaafu kutegemea na mahitaji ya kimkakati au sera za kijeshi za nchi. Hii mara nyingi hufanyika kwa kuzingatia uwezo na uzoefu wa wanajeshi walio katika huduma.

Kwa hiyo jeshi halina watu wa kutosha wenye weledi wa kupewa uongozi, linategemea vibabu vichache vyenye uwezo na uzoefu ????? Unaona hiyo picha ni poa tu ?

Na unadai kuna sheria nyingine ya kustaafu inawahusu wanajeshi tu ? Na inapingana na sheria ya raia, na haijasemwa kwenye sheria ya raia kwamba kuna exception kwa wanajeshi ?

Wakati mwingine tunakuwa stressed out bure kujadili mambo ya kitaifa na wauza mbege bila kujijua.

Nchi ina tatizo sugu la ajira lakini unaona ni poa kuvunja sheria za kustaafu na kubakiza vibabu kazini ?

Eti wana uwezo na uzoefu. Kwa nini wasikuze uwezo na uzoefu wa walio chini ya umri wa kustaafu ?
 
Hivi huko Marekani huwa hawakosei?

Katiba yao imefanyiwa marekebisho mara ngapi?

Na kwa nini katiba yao imefanyiwa marekebisho?

Na toka kwa Rais wa kwanza aliyefia madarakani mpaka Rais wa nane aliyefia madarakani, taratibu zao ni zilezile, hazikuwahi kufanyiwa maboresho au marekebisho?

Na kama zilifanyiwa marekebisho, ni kwa nini?

Marekani ilifanya kila kitu kwa usahihi kuanzia kifo cha Rais wa kwanza aliyefia madarakani mpaka kifo cha nane?
Nimesoma comment zote ulizo changia kama kuna mtu hajakuelewa ana shida kubwa kwenye mfumo wake wa akili
 
Hivi huko Marekani huwa hawakosei?

Katiba yao imefanyiwa marekebisho mara ngapi?

Na kwa nini katiba yao imefanyiwa marekebisho?

Na toka kwa Rais wa kwanza aliyefia madarakani mpaka Rais wa nane aliyefia madarakani, taratibu zao ni zilezile, hazikuwahi kufanyiwa maboresho au marekebisho?

Na kama zilifanyiwa marekebisho, ni kwa nini?

Marekani ilifanya kila kitu kwa usahihi kuanzia kifo cha Rais wa kwanza aliyefia madarakani mpaka kifo cha nane?
They made mistakes, definitely. Ila njaa yetu sio njaa ya kawaida
 
..Maana yake ni kwamba aliteuliwa CoS akiwa na umri wa kustaafu, na aliteuliwa CdF akiwa ameshavuka umri wa kustaafu.

..Ndio maana nasema kuna walakini ktk uliofanywa na Jiwe.
Labda jiwe aliangalia watangulizi wake walifanyaje.

Mwinyi kamteua Kiaro kuwa mkuu wa majeshi akiwa na miaka 65. Alihudumu kwenye cheo hicho hadi 1994 alipostaafu akiwa na miaka 71.

Mtangulizi wa Kiaro, Msuguri alistaafu akiwa na miaka 68.
 
Labda jiwe aliangalia watangulizi wake walifanyaje.

Mwinyi kamteua Kiaro kuwa mkuu wa majeshi akiwa na miaka 65. Alihudumu kwenye cheo hicho hadi 1994 alipostaafu akiwa na miaka 71.

Mtangulizi wa Kiaro, Msuguri alistaafu akiwa na miaka 68.

..nakushukuru kwasababu umezungumza fact na umenielimisha.
 
They made mistakes, definitely. Ila njaa yetu sio njaa ya kawaida
Na bado wanafanya makosa!

Marekani siyo perfect.

Hata sasa hivi Democrats wanataka kutumia rungu la sheria kumnyanyasa Donald Trump kwa kumfungulia kesi uchwara na kutaka kuliondoa jina lake kwenye karatasi za kura.

Does it ring a bell? Chama gani hapa bongo huwatendea matukio wapinzani wa kisiasa?

Marekani kuna mambo mengi sana huwa wanakosea. Kuna mambo mengi sana waliyokosea.

Lakini hujifunza!
 

View: https://m.youtube.com/watch?v=9Hyg_T0yb-8

Katika dunia hii mtu wa mwisho ambae unaweza kuona chozi lake hadharani ni senior army officer na army general ndio kabisa awezi kuonyesha weakness hiyo hadharani.

Sasa cha kushangaza Mabeyo pamoja na kujitahidi kutabasamu ila chozi lilimshinda nguvu kwa sekundę kadhaa ameonekana akibubijikwa machozi ya hudhuni mbele ya camera. Kumbuka ata alipofiwa na mtoto wake rubani, general akutoa chozi alipofika eneo la tukio.

Je, anajutia kutosikiliza maamuzi ya watu waliomshauri wapindue męża ya katiba huyo mama hiyo nafasi sio size yake na kinachoendelea leo Tanzania.

Majitu ya Kanda ya ziwa mabaguzi
 
Atakuwa alilipenda kweli jeshi kama ni ivyo. Maana mwenyekiti wa bodi ya TANAPA ni mmoja wa watu wenye mshahara na marupurupu makubwa Tanzania.
Wewe nawe Kumbe hamna kitu, wenyeviti na wajumbe wa Bodi hawana mishahara. Hupata pesa kama kiinua mgongo Fulani kila baada ya miaka mitatu ambao ndiyo muda wa Bodi kuwapo madarakani. Na wengine huigawa Kwa tatu Ili kila mwaka wapate chochote. zaidi ya hapo ni posho ya vikao.
 
Back
Top Bottom