Tuliongozwa na 'Busara' za Jenerali Mabeyo, kungeweza kutokea matatizo makubwa sana.
AG (Mwanasheria Mkuu) alitakiwa asimame kutafsiri na kuelekeza Katiba inatamka nini na kama haitamki kisheria kipi kinafanyika.
Makamu wa Rais alipaswa kuapishwa usiku saa 6 na si kusubiri siku 3 au kujiuliza viongozi watapokewaje.
Rais yupo mahututi yupo na CDF, IGP na DGIS , Makamu na Waziri mkuu wanahanja hanja! ni hatari sana.
Jamani tuacheni ubishi, tukaeni chini na kutengeneza katiba ili tupate sheria zenye miongozo
Kusema eti hatuna uzoefu kama Marekani si kweli. Tulitakiwa tutumie uzoefu wa Marekani kufanya vizuri
Ni kama vile 'tunajitahidi kutengeneza kompyuta yetu from the scratch ' badala ya kutumia zilizopo kupiga hatua
Hii interview imeeleza mambo mengi sana
Nani analeta ubishi hapa?
Ni kweli hatukuwa tumewahi kufiwa na Rais aliyepo madarakani!
Marekani wali handle kivipi walipofiwa na Rais aliyepo madarakani ilipotokea mara ya kwanza? Ilikuwa mwaka gani? Kila kitu kilienda sawa? Hawakujifunza chochote kutokana na hilo tukio la kwanza? Hawakubadili chochote toka kwenye tukio la kwanza hadi tukio la nane?
Unaweza ukaweka kitu vizuri sana kwenye maandishi lakini inapokuja kukitekeleza kwa vitendo, unakutana na mengine ambayo hukuwa umeyafikiria.
Ndiyo, kujifunza kutoka kwa wengine ni vizuri. Lakini pia, dynamics za matukio hazifanani.
Na ndo maana nasema experience hii ni fursa nzuri ya kujifunza na kurekebisha pale palipokosewa.
Huwezi kuiga kila kitu cha kwenye makaratasi kutoka Marekani halafu udhani kwamba tukio likitokea kwako, basi hakutakuwa na kwikwi katika kutekeleza kile ulichopanga.
Hata leo hii bado Wamarekani huwa wanakosea hata kwenye uapishaji wa Rais wao.
Mwaka 2009 Obama aliapa mara mbili kwa sababu ya kosa lililokuwepo kwenye kiapo cha kwanza.
Imagine wanarudia tukio kwa mara ya 44 na bado makosa yanakuwepo, seuze sisi kwa tukio la mara ya kwanza?
Likija kutokea tena tukio la Rais kufia madarakani halafu kukawa tena na makosa yaleyale yaliyofanywa kipindi cha tukio la kwanza, hapo itakuwa sawa kulalamika.
Kwa tukio la kwanza, I cut them some slack.
Hata katiba ya Marekani imefanyiwa marekebisho kwa zaidi ya mara 20! Kwa nini?