Dar es Salaam ili uende kazini na kurudi lazima uandae elfu 10 ya usafiri pamoja na chakula. Maskini hana chake hapa nchini

Ndio maana kuna room ya kujifunza.. sasa nyakati hizi ni za kuchagua kazi kweli wakati upatikanaji wa kazi yenyewe ni mtihani
 
Tatizo hiyo 8M hana, hata hiyo 3M ya Kibaha analipia kidogokidogo. Kipato kikiwa kidogo mtu analazimika kufanya mambo yaliyo ndani ya uwezo wake
Mkuu, huyu mtu kajenga kabisa,
Ina mana kama unaweza kujenga nyumba ya 30M tu, halafu unashindwa kulipa 8M ya kiwanja sehemu nzuri, ? Ambayo nayo unalipa kidogo kidogo?
 
Sema na kuishi mbali sana jau,
Hapo mkuu kama hio ratiba ni kweli nakuonea huruma,

Sometimes tunakimbilia viwanja vya bei rahisi ila mara mia ulipe pesa kubwa upate sehemu nzuri sio kujificha huko porini.
Mtoa mada anadai "kununua kiwanja center labda awe fisadi. Wengi tunajuchanga tunapata viwanja Chanika, Bagamoyo, Kisarawe, Pugu n.k."

Huwa ninashindwa kuwaelewa watu wanaosema kuna ardhi ya mbali.

Unapodai Kisarawe ni mbali, una maanisha umbali toka center ya Dar hadi Kisarawe; sawa!

Kwani ni lazima ukae Dar center?

Unadai pia kununua kiwanja Dar center huwezi, na labda uwe fisadi! Aisee! Kwani ni lazima ununue kiwanja Dar Center?

Utasema huko Dar Center ndipo unafanyia kazi; sawa! Pia siyo lazima ufanye kazi City Centre! Tafuta kazi nyingine!

Halafu kwa taarifa tu, mwaka 1995 pale Sinza viwanja vilikuwa Tsh laki 5, ila sasa hivi ni milioni zaidi ya 200. Na wakati huo palikuwa shamba maana mji uliishia Magomeni na Stendi ya Mikoani ilikuwa pale Kisutu.

Ukiona huwezi kuishi maisha ya kufanya kazi City Center kwa kuwa ni gharama basi ujue unaishi fake life, yaani maisha yasiyoendana na kipato chako, hivyo inakupasa kubadilisha mindset na kutafuta shughuli nyingine; ukilalamika hakuna atakayekusaidia kamwe!

Halafu ni ushamba kufikiri kwamba ili ununue kiwanja ni lazima uwe fisadi!

Ninachokifahamu, usipokifuata unachokitaka basi utabaki ulivyo tu!

Watu mnaangamia kwa kukosa maarifa!
 

JF kila mtu matawi..et natumia 15k kwenda kazini na kurudi mara chache dalaladala huwa natumia daladala..humu mnatupanga sana kama una uwezo wa kutumia 15k unalalamika nini hiyo nauli? Au ndo kipato chako laki 2.5 unajifanya unasemea wengine?
 
Nimesoma koment yako secretary wa waziri mkuu
[emoji106]
 
Daaaa !!Ila wa Tanzania tumezidi ukoondoo..Hizi nauli zinapandishwa kihuni sana.
 
Nilijua una usafiri... Anyway... kulihudumia gari kunagharama zake mkuu.. kama unanua gari lazima uwe mtu wa mishe mishe.. au kama umeajiriwa uwe unapata mshahara ambao unaweza save 60% ya salary yako ,hapo utaenjoy..
Lakini nauli zimepanda una lalamika , sizani kama unaweza mudu kuhudumia gari kwa kucomplain 20K per day
 
Sina gari mkuu, niliongea theory ambayo nahisi hata wenye magari wanaona tofauti. Zamani waliweza kwenda sheli na kuweka mafuta ya 10k(tulikuwa tunawaona), leo 10k is a joke.
 
Mkuu acha kutukumbusha machungu... watu tumetoka mbali sanaa.. nakumbuka niliwah endakariakoo asubuh nilirud saa 11 sikula ata kitu zaidi ya kandoro ya 200 aisee..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…