Dar es Salaam ili uende kazini na kurudi lazima uandae elfu 10 ya usafiri pamoja na chakula. Maskini hana chake hapa nchini

Dar es Salaam ili uende kazini na kurudi lazima uandae elfu 10 ya usafiri pamoja na chakula. Maskini hana chake hapa nchini

sasa mkuu huko Kimara na Maramba si ni yale yale tu, bora useme Keko, Chang'ombe, Magomeni, Kinondoni, Manzese nk.

Lakini pia mkuu, hakuna anayependa kuishi Kibaha ndanindani, umasikini mkuu, jamii ya kubwa ya Watanzania ni masikini.
Ndio umaskini, lakin tazama utofaut wa nauli na cost nyingine unapoenda panga chumba mbali kwa kigezo cha kusave pesa,

And kimara hadi Kkoo ni gari moja, toka kibaha huko hadi kkoo ni gari si chin ya 3, nadhani utaona cost ya nauli na muda,

Pia mleta mada kajenga, so hana umaskin wa kutisha, angejipiga anunue kiwanja malamba, au kimara ingemsaidia kuliko kwenda kujificha maporin huko unasave 5M ya kiwanja, ila ukihamia kila mwezi unalipia cost ya 300K ya kukaa mbali
 
Naandika hii mada nikiwa na uchungu moyoni.

Sasa hivi nina miezi kama 4 hivi natumia Daladala kwenda na kurudi kazini na mara chache, tena chache sana huwa natumia bodaboda kazini mpaka home, home mpaka kazini.

Kutoka Nyumbani mpaka kazini nikipanda bodaboda direct ni elfu 15. Go and return inalala 30000 sh
Nikipanda bodaboda 1500 sh. mpaka kituo cha Daladala na nikipanda Daladala moja mpaka kazini awali nilikuwa natumia 1000 sh. Jumla 2500 sh, kwenda na kurudi natumia sh. 5000 kamili, nikipanda gari mbili nilikuwa natumia kama elfu 6 hivi. Pesa ambayo himilivu kwangu.

Ila sasa nikipanda Daladala itanilazimu nitumie takribani 7000 kwenda na kurudi.

Hapo ukiweka na chakula na maji around 5000.

Kwahiyo Mimi tu inabidi nitumie angalau elfu 12 kwaajili ya kazini. Familia kwa sasa hali ilivyo kwa siku ni sh. 10 -20 hapo mahitaji yote muhimu kama gas, mkaa, chumvi, Michele na unga viko ndani. Kama havipo lazima uangushe 20.

Kwahiyo inanilazimu kwa siku nitumie kuanzia elfu 30.

Vipi kwa anayelipwa laki 2.5 au laki tatu kwa Wahindi?

Vipi anayelipwa elfu 7 kiwandani kwa siku?

Kipato changu kidogo nahisi kupata msongo wa mawazo.
Kwa mwezi natumia karibu milioni 1 kwa chakula nyumbani , kazini , usafiri na dharura ndogondogo.
Hapo ukiweka dharura kubwakubwa kama kufiwa na ada za shule watoto mwezi mmoja naangusha zaidi ya milioni.

Serikali ipunguze nauli, watu wanashindia mihogo makazini Ili kubana nauli za kurudia nyumbani jioni.

Hakuna mtumishi wa umma au mwajiriwa wa sekta binafsi Dar es Salaam anaweza kununua kiwanja center labda awe fisadi. Wengi tunajuchanga tunapata viwanja Chanika, Bagamoyo, Kisarawe, Pugu n.k.

Kwa nauli hizi Ili ugeuke na gari upate seat lazima ujipange. Unakuta kila ukipiga hesabu 20 imeenda kwa usafiri na misosi.

Umaskini utaendelea kutupiga maana hatuna mtetezi.
Badala ya kufikiria kujiongezea kipato wewe unafikiria kuwaumiza wenzio, au unafikiri spare parts za magari wanaokota bure? Au mafuta wanaokota bure?
 
20231209_135117.jpg
 
Kabisa,

Au mtu anaambiwa kimara kiwanja 8M, na Kibaha kiwanja 3M anakimbilia Kibaha, ila akishahamia Kibaha cost per month za kukaa mbali ni 300k
Tatizo hiyo 8M hana, hata hiyo 3M ya Kibaha analipia kidogokidogo. Kipato kikiwa kidogo mtu analazimika kufanya mambo yaliyo ndani ya uwezo wake
 
Kazi ni kazi kikubwa mkono uende kinywani
Siyo kweli.

Hilo ni mpaka uwrme hauna uzoefu wowote wa kazi yoyote.

Binadam inatakiwe useme ulichowahi kukifanya, kama hujawahi ufanya chochote, unasema ukweli.

Unasema mimi nimesoma mpaka darasa ??

Nimewahi kufanya au kujifunza kazi hii au hii.

Ndiyo maana vijana wengi mnakosa kazi za kufanya, mnashndwa hata kujieleza ukweli wenu.
 
Back
Top Bottom