Dar es Salaam ili uende kazini na kurudi lazima uandae elfu 10 ya usafiri pamoja na chakula. Maskini hana chake hapa nchini

Dar es Salaam ili uende kazini na kurudi lazima uandae elfu 10 ya usafiri pamoja na chakula. Maskini hana chake hapa nchini

Maisha ni kuchagua. Kuna ambaye anang'ang'ania kukaa mjini huku akipambania mlo tu hana uwezo wa kufanya savings yoyote, na kuna anayekaa bushi ambaye mlo kwake ni wa uhakika na ana savings ya kufanya maendeleo.


Endeleeni kung'ang'ania mjini tu. Mtakumbuka shuka kukiwa tiyari kumeshakucha
Ukienda mikoani asilimia kubwa hali ni mbaya bora hata dar
Mikoani matajari ni wale wale au familia zile zile miaka nenda rudi
 
Tupige hesabu za mtu anayetumia gari ndogo tu inayokula wese la kawaida tu, say 1.3L engine. Mtu huyu anaendesha 50km kwenda kazini na kurudi kila siku. Gari inakula walau 1L kwa 10-12km/hr kwa wastani. Huyu mtu anahitaji kila siku kuweka wese angalau 5L x 3150 = 16,000 ≈ 20,000...hapo ameenda na kurudi, hajapata mishe yoyote ya kuongeza km.

Mwanzo tuliona wanaomiliki pikipiki hawajielewi, leo hii naona wao ndio wanafurahia maisha. Nasikia 1L inaweza kutembea hadi 60km sijui kama kuna ukweli hapo.
Tatizo unakaa uko kerege alafu unategemea nini
 
Hili suala wengi hawazingatii, wewe unalipwa laki tatu halafu unakaa kilomita 45-50 mbali na kazini utakuwa maskini mpaka uzeeni... kaa mbali kama una usafiri wako nje ya hapo unazingua
Hata kama usafiri ni wako, hayo mafuta unakuta kwa mwezi umetumia laki 6 minimum.
 
  • Je Uma maanisha vibarua vya mashamba ya makampuni ambavyo hulipa 5,000/- kwa siku inayoanza saa 1 mpaka 10 jioni?
  • Kama ni mamba ya kujilimia, kilimo si kazi lelemama kama wengi wanavyodhani.
  • Ushauri wangu: Ni vyema kijana kwenda mji mwingine wenye ahueni ya maisha - hasa miji ya mipakani - akaendeleze pambano huko.
Vijana hamtaki kazi zenye kulipa. Mnataka mteremko wa kuajiriwa kwa maslahi mazuri.

Kama unataka kazi inayolipa vizuri anzisha ya kwako.

Usitarajie tajiri akutajirishe!
 
Dah nmetoka kupiga jana tu hesabu ya mwezi maana nlidownload app ya budget playstore ambayo nilikua naandika kila income na expenses nlizokuwa natumia mbona macho yaligeuka mekundu na nguvu kuniisha

Maana daily 20k mafuta gari
Daily 20k home na hapo baadh ya vitu vipo
Bills umeme,maji nk 50k
Chakula job 10k hpo ndo kujibana
Vocha
Na mengineyo.
NB;
Sinywi pombe wala si mtu wa starehe
Umefka mwsho wa mwezi Expenses zimegonga 3m+ nikawa kama nimemwagiwa maji
Halafu kuna mwanamke anakwambia me sihitaji mwanaume, kama wanaume wanapitia uchumi huu hawa wanawake wetu itakuwaje aiseee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Naandika hii mada nikiwa na uchungu moyoni.

Sasa hivi nina miezi kama 4 hivi natumia Daladala kwenda na kurudi kazini na mara chache, tena chache sana huwa natumia bodaboda kazini mpaka home, home mpaka kazini.

Kutoka Nyumbani mpaka kazini nikipanda bodaboda direct ni elfu 15. Go and return inalala 30000 sh
Nikipanda bodaboda 1500 sh. mpaka kituo cha Daladala na nikipanda Daladala moja mpaka kazini awali nilikuwa natumia 1000 sh. Jumla 2500 sh, kwenda na kurudi natumia sh. 5000 kamili, nikipanda gari mbili nilikuwa natumia kama elfu 6 hivi. Pesa ambayo himilivu kwangu.

Ila sasa nikipanda Daladala itanilazimu nitumie takribani 7000 kwenda na kurudi.

Hapo ukiweka na chakula na maji around 5000.

Kwahiyo Mimi tu inabidi nitumie angalau elfu 12 kwaajili ya kazini. Familia kwa sasa hali ilivyo kwa siku ni sh. 10 -20 hapo mahitaji yote muhimu kama gas, mkaa, chumvi, Michele na unga viko ndani. Kama havipo lazima uangushe 20.

Kwahiyo inanilazimu kwa siku nitumie kuanzia elfu 30.

Vipi kwa anayelipwa laki 2.5 au laki tatu kwa Wahindi?

Vipi anayelipwa elfu 7 kiwandani kwa siku?

Kipato changu kidogo nahisi kupata msongo wa mawazo.
Kwa mwezi natumia karibu milioni 1 kwa chakula nyumbani , kazini , usafiri na dharura ndogondogo.
Hapo ukiweka dharura kubwakubwa kama kufiwa na ada za shule watoto mwezi mmoja naangusha zaidi ya milioni.

Serikali ipunguze nauli, watu wanashindia mihogo makazini Ili kubana nauli za kurudia nyumbani jioni.

Hakuna mtumishi wa umma au mwajiriwa wa sekta binafsi Dar es Salaam anaweza kununua kiwanja center labda awe fisadi. Wengi tunajuchanga tunapata viwanja Chanika, Bagamoyo, Kisarawe, Pugu n.k.

Kwa nauli hizi Ili ugeuke na gari upate seat lazima ujipange. Unakuta kila ukipiga hesabu 20 imeenda kwa usafiri na misosi.

Umaskini utaendelea kutupiga maana hatuna mtetezi.
Hakuna atakaye kusikia Mkuu!

Yote uloongea yapo nje ya uwezo wa Rais tuliyenaye kuyatatua.
 
Hata kama usafiri ni wako, hayo mafuta unakuta kwa mwezi umetumia laki 6 minimum.
Acha mafuta yaani Dar foleni unaipata vile vile kama kawaida yaani kama hizi mvua ,unaweza kutamani kiacha gari kweny foleni ili uwahi home kwa bodaboda..


Kwa Dar kama unakaa sehemu daladala zinafika bora upande daladala ...Gari ya kawaida unatakiwa kuwahi sana asubuhi kuepuka foleni
 
Kati ya usafiri ambao hauna risk naweza kusema boda boda.
Boda n umakini wako dereva tu.
Ukiona huwezi kupita main road unaweza kupita service road.
Kwani Kama ukipita high way na ukafuata Sheria utapata changamoto gani?

Mf kwenye mataa ukasimama na kwenye kuendesha ukakaa Lane yako hapo huwezi kupata ajali kizembe.

Ajali nyingi za boda boda ni uvunjifu wa Sheria unakuta
kwenye Mataa unaforce kupita
Unapenya Kati Kati ya roli na basi
Una overtake basi au roli kwa pembeni au upande wa dereva .

Ila ukiwa smart njiani hutopata ajali za ki puuzi.
Kingine Kama huna uwezo wa kubeba wawili chukua abiria 1 tu mwepesi.

Nyongeza

Boda boda.
Hakai foleni
Hakaguliwi na polisi
Hatoi hela ya ku brush viatu
Hapigwi mkono na polisi

Kupanga ni kuchagua.
Weweeeee
Daladala huku mtu anatembea kwa miguu huku wewe unaendesha boda, akiyumba anakubali amwache raia wa miguu anakugonga wewe pamoja na abiria wako.
Wanasemaga kuwa ukigonga boda hata elfu 30 hulipishwi. Ni kama panzi tu
 
Mkuu, huyu mtu kajenga kabisa,
Ina mana kama unaweza kujenga nyumba ya 30M tu, halafu unashindwa kulipa 8M ya kiwanja sehemu nzuri, ? Ambayo nayo unalipa kidogo kidogo?
Haya tufanye umekopa milioni 10 nininue kiwanja cha 8 ml. Milioni mbili nifix mambo ya kifamilia. Mkopo ni wa miaka 7. Itanichukua miaka 7 tena kuweza kukopa milioni 15 ya kusimika Nyumba ya kuanzia. Huoni huo ni u crazy?
Unanja unakopa pesa let say 15 milioni unanunua kiwanja 2 milioni, 13 milioni unajenga nyumba ya kuanzia, baada ya deni kwisha unaweza kukopa pesa kubwa zaidi maana mshahara utapanda kidogo unafungua maduka 2 ya jumla Moja Chanika, jingine Gongolamboto .
Baada ya miaka 10 ya utumishi unakuwa doni.
 
Haya tufanye umekopa milioni 10 nininue kiwanja cha 8 ml. Milioni mbili nifix mambo ya kifamilia. Mkopo ni wa miaka 7. Itanichukua miaka 7 tena kuweza kukopa milioni 15 ya kusimika Nyumba ya kuanzia. Huoni huo ni u crazy?
Unanja unakopa pesa let say 15 milioni unanunua kiwanja 2 milioni, 13 milioni unajenga nyumba ya kuanzia, baada ya deni kwisha unaweza kukopa pesa kubwa zaidi maana mshahara utapanda kidogo unafungua maduka 2 ya jumla Moja Chanika, jingine Gongolamboto .
Baada ya miaka 10 ya utumishi unakuwa doni.
Kiwanja cha 400sqm kimara unaweza pata kwa 8M, kwa mfipa unapata kwa 4M utofauti ni 4M, hii pesa kama upo serious na mradi unaweza isave ndani ya mwaka na ukaishi maisha yako vema,
Kuliko ukimbilie porin huko kisha uje ulete uzi kama huu wa kulalamikia daladala + habari za kufika home saa 5 na kuamka saa 9 kuwahi ofisini,

Hakuna faida ya kukimbilia kufanya kitu kama kitakuletea shida tu huko mbeleni
 
Halafu kuna mwanamke anakwambia me sihitaji mwanaume, kama wanaume wanapitia uchumi huu hawa wanawake wetu itakuwaje aiseee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Si ndo kudanga,michepuko na kujiuza mkuu we game la mahusiano siunaona linavoenda ni pesa tu
 
Back
Top Bottom