DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Hizo habari zenu za kupata tabu yeye hazimuhusu, hawezi kusoma anasoma taarifa zinazomuhusu ukiandika kwa kumtaja kuhusu huo mradi na kumkosoa kiasi cha kitishia uhai wako kwa kutekwa na kupotezwa kabisa hapo lazima atasoma tu
Upo sahihi kabisa. Sio shida zake
 
Upo sahihi kabisa. Sio shida zake
Ndio wewe ukitaka iwe shida zake shika bango kwa kumtajataja kuhusu hilo suala la Dart kiasi cha kutishia kuanza kufuatwafuatwa na wale jamaa wanaotembea na Gari lisilo na plate number hapo lazima atasoma
 
Dart ni w@##$$$&&&&ge tu mnakalisha watu masaa mawili anasubiria gari hiyo mnaosema mnaleta magari kabla ya mwezi wa tisa ni kampeni za ki(&&$#&ge tu kwani hamuoni shida ya sasa
 
Dart ni w@##$$$&&&&ge tu mnakalisha watu masaa mawili anasubiria gari hiyo mnaosema mnaleta magari kabla ya mwezi wa tisa ni kampeni za ki(&&$#&ge tu kwani hamuoni shida ya sasa
Ndio maana nataka hii tbread ifutwe na dart wapigwe ban hapa JF.
Thread yao haina msaada na haina tofauti na ile thread ya kula tunda kimasihara
 
Reactions: Lax
Hivi Ndugu zetu huwa mna akili timamu kweli?? Ma bus hamna ila mme ng'ang'ana kuuza kadi, hii si ni sawa na kuwauzia watu miujiza ya kwamba yesu atarudi kuwakomboa??!!
Suala la kadi ni la kisheria ili kudhibiti uvujaji wa mapato ya serikali na pia kutunza mazingira, aidha matumizi ya kadi yameondoa kero ya ukosefu wa chenchi na kupanga foleni ya kukata tiketi za karatasi, hivyo halikwepeki. Kuhusu Mabasi ondoa shaka tumeshasaini mikataba na makampuni kadhaa ambayo wako kazini usiku na mchana wanatengeneza mabasi ama kwa hakika yajyo yanafurahisha ni suala la muda tu.
 
Dart ni w@##$$$&&&&ge tu mnakalisha watu masaa mawili anasubiria gari hiyo mnaosema mnaleta magari kabla ya mwezi wa tisa ni kampeni za ki(&&$#&ge tu kwani hamuoni shida ya sasa
Jaribu kuwa na staha sasa kama tumeeleza Mabasi yatakuja kabla ya mwezi huo uliotaja inamaana gani kulalamika na kutukana? subiri uone utekelezaji kwani mwezi husika haujafika.
 
Suala la kadi ni kweli tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, msisitizo wetu ni kwamba kila mmoja wa watumiaji wa huduma zetu ahakikishe ananunua kadi yake kwa bei ya Tsh, 1,000/= tu, kama ulivyoona uchafuzi wa mazibngira umepungua kutokana na kutokuwepo kwa kaaratasi lakini pia majibizano yasiyo ya lazima ya kukosekana kwa chenchi nayo hayapo tena.

Kuhusu Mabasi tumeshasaini mikataba na watoa huduma ambao wataleta Mabasi mapya ni suala la muda tu, na ikumbukwe kuwa mabasi hayo sio kwa awamu hii ya kwanza tu pia ni kwa awamu ya pili kuelekea Mbagala, tuendelee kuwa na subra wakati watoa huduma hao wakiendelea kutengeneza mabasi.
 
Kwa kuwa hamna mabasi kwa sasa toeni nafasi kwa daladala kufika kwenye maeneo kama mbezi posta na mbezi kkoo.

Hii ya watu kulundikana hadi kuingilia madirishani sio sawa.
 
Mabasi 100 ya gesi mlioahidi mwezi huu yamefikia wap. Au meli imekwama?

Kwa nini hamna final say na mnakuwa waongo waongo.

Kuweni wawazi, na toeni updates kila week. Hii ndo kazi ya PR
 
Hivi Ndugu zetu huwa mna akili timamu kweli?? Ma bus hamna ila mme ng'ang'ana kuuza kadi, hii si ni sawa na kuwauzia watu miujiza ya kwamba yesu atarudi kuwakomboa??!!
walisema mwezi wa nane kuna ndinga zitaingia, kampuni ya mofat wamewapa ruti ya gerezani mbagala.

mwendokasi una hali mbaya sana ni kuskilizia tu kama ni kweli --- hiyo ruti ya mbezi nayo simanzi tu
 
ngetakiwa kutoa ripoti kwanza kwanini mmeyaua mabasi ya mwanzo yale na usababishia usumbufu wananchi
 
Mabasi 100 ya gesi mlioahidi mwezi huu yamefikia wap. Au meli imekwama?

Kwa nini hamna final say na mnakuwa waongo waongo.

Kuweni wawazi, na toeni updates kila week. Hii ndo kazi ya PR
Hakuna pahala ambapo tuisema mwezi huu tunaleta mabasi 100, utakuwa umechanganya na jielimishe zaidi kujua tofauti ya DART na wengine.
 
ongezeni mabasi, sio jambo zuri watu kupanga foleni na kusubiri hadi wanachelewak azini, ni picha mbaya sana kwamba una mwendo kasi ila watu waanapandia madirishani kama wanaenda basi za mbagala zamani. dunia nzima kwenye mwendo kasi hakuna watu wanapandia madirishani. au hamuoni? pia leteni tiketi electronic, watu waamue kukata ya siku, wiki au mwezi mashine iwepo mlangoni mwa basi kama majuu. acheni ushamba.
 
Fahamu zaidi kuhusu Mwendokasi Card namna ya kujisajili na kuweka salio kwa mitandao ya simu na Benki.
 

Attachments

  • kuweka salio benki.jpg
    17.8 MB · Views: 37
  • mahitaji kusajili.jpg
    17.1 MB · Views: 31
Hakuna pahala ambapo tuisema mwezi huu tunaleta mabasi 100, utakuwa umechanganya na jielimishe zaidi kujua tofauti ya DART na wengine.
Admin unapotea mkuu, hii gia yako ni mbaya kwa kuendeshea akaunti ya shirika la umma.

NA KAMA UNAJIAMINI TOA TIMEFRAME TUWE TUNAIFATILIA MKUU.

kila la kheri
 
Mabasi yanakuja kama tunavyosisitiza kila wakati, na kama ni mfuatiliaji mzuri wa mitandao tayari kuna mzigo uko tayari uko kwenye hatua za kupakiwa na mengie yanatengenezwa kwa kasi kubwa.Mifumo ya kielektroniki ipo ndio maana tumezima mtambo wa tiketi za karatasi sasaivi tunatumia kadi janja tu na pia tuna app yetu inaitwa Mwendokasi App inapatikana kwenye App store na Android vyote hivyo ni kuepuka kabisa matumizi ya tiketi za karatasi sasahivi dunia imehama malipo mengi sio kwa fedha taslimu ni mifumo ya kielektroniki tu.
 
Admin unapotea mkuu, hii gia yako ni mbaya kwa kuendeshea akaunti ya shirika la umma.

NA KAMA UNAJIAMINI TOA TIMEFRAME TUWE TUNAIFATILIA MKUU.

kila la kheri
Tupo kila siku mkuu na kwenye nyuzi nyingi huko juu tumeshaelezea ni lini hasa watanzania wataanza kuonja mafanikio ya serikali yao na kusahau machungu, endelea kutufuatilia kwa karibu pia katika mitandao yetu ya kijamii, facebook,instagram, (X) na linkedlin kwa anuani ya @DARTMwendokasi, kwenye Youtube @DARTTV na pia tuna namba ya bure 0800110147 karibu sana.
 
Reactions: Lax
Safi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…