Dawa ya Mpenzi anayekujibu dharau au ambaye hana muda na wewe ni hii hapa

Mimi sio mwandishi mzuri kaka.
Woooi mimi mwenyewe huyu kaka nikimuangalia anavyonipenda namuomba Mungu anipe hekima na busara niwe mtiifu kwake daima.
That's my girl...ukishikwa shikamana unaweza kuona huyu ni ......., si wapo wengine kumbe wengine wanaonekana 7bu yupo huyo ukitoka hapo ndio utajua hujui!
 
Mwanaume usipuuze redflags!… amani ya moyo wako ni jambo kuu muhimu ambalo unatakiwa kulipa kipaumbele zaidi. Jifunze kuachilia utakuwa na amani

Hakuna kampani bomba zaidi hasa ya washkaji na marafiki ambao ni productive yaani mkiwa pamoja mnakuwa busy mara nyingi.., inasahaulisha upuuzi mwingi sana!
 
Mimi sio mwandishi mzuri kaka.
Woooi mimi mwenyewe huyu kaka nikimuangalia anavyonipenda namuomba Mungu anipe hekima na busara niwe mtiifu kwake daima.
Daaah na uwe hivyo milele maana dah inatisha sana kupendwa na mtu alafu uwe unajibu hovyo.

Best of lucky
 
Umenena ukweli wenyew kaka.....niliwahi puuzia redflag kikanilamba acha tu
 
Inategemea sasa na mtu na mtu, sio ya kujaribu holela.
Kinakulamba hivi hivi, πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hayana formula, mwingine ukimfanyia hivyo ndio mazimaaa .. sema mapenzi hayalamishiwi. Penzi la kulazimisha baya sana.. Tuachane na hili, nilikuja nduki nikijua dawa ya mganga.. kuna katoto kananisumbua hapa
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Inategemea sasa na mtu na mtu, sio ya kujaribu holela.
Kinakulamba hivi hivi, πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
waweza mnyamazia mtu na ndio ikawa niagieni, lakini pia kulazimisha penzi ni hatari kwa afya..
 
Kweli Mapenz yanauma Ila hayafikii kumpa hela dada yako na unajua hatakurudishia na kumnyima huwezi
 
Usiombe ukutane na mwanaume anakudharau halafu wewe umempenda unategemea mvuke hatua ya ndoa.

Kuna jamaa alifikia sehemu akaanza verbal abuse mara "we ni mzuri na una mguu mzuri sana ila ungekuwa mwembamba zaidi ya hapa, na pia sipendi maji ya kunde napenda mdada mweupe", eeh, you mean unataka nijichubue, and I was just 62kg kwa height ya 168m, kweli jamani?. Nikaona hii ni ile wanayosema wahenga "akufukuzae hakuambii toka"

Tukapotezeana hivyo kimya kimya. Ikapita kama wiki 2 akanipigia simu nakutakia mitihani mema", nilikiwa chuo, nikasema "asante baba".. hatukuwasiliana tena. Penzi likaishia hivyo. Before alikuwa ananiambia mi ni wife material nikawa namwambia ngoja nimalize shule kwanza, nakupenda kwa dhati kabisa.

Mwaka mmoja niko zangu kazini (niliajiriwa immediately) nakutana na coworker ambaye ni mutual friend yetu. Nam-add Facebook jamaa ana-pop up up kwemye friend list ya coworker. Nikashtuka unamfahamu fulani akasema ndiyo, kanipa story fulani nikabaki nacheka tu.

Ingawa naye alipata kazi haraka ali-mess up na mdada wa watu akamtia mimba, mzazi wa mdada akakomaa hapa unaoa, silei mabinti waliozalishwa akafungishwa ndoa mithiri ya ndoa mkeka ya kanisani, you can tell hakukuwa na maandalizi yoyote just ndoa ifungwe tu.

Kilichonichekesha mdada ni mweusi kama mkaa (Sina tatizo na rangi ya mtu, all skins are beautiful, ila si alininyali mimi maji ya kunde anataka mwanamke mweupe?, kwanini nisicheke?) Kama haitoshi, mdada alivyozaa alishift kutoka model hadi jimama libonge, yaani obese kabisa. Sasa kwenye picha yao ya harusi jamaa yuko kama ananing'inia walivyo-hug maana mdada kamzudi size, nikasema dawa yako, malipo hapa hapa duniani.

Few year later tukaonana, sijui kwanini Mungu anafanyaga hivi. Analalamika eti sikufight enough, anahoji kama kweli nilikuwa nampenda, nikamwambia baba, kwenye mapenzi nafight na mtu ninayempenda against dunia, siyo mimi ni-fight na dunia peke yangu wewe ukiwa upande wa dunia. Akashauri ooh, kuna option, naweza kumwacha mke wangu tuoane ndoa ya kanisani ila kwa walokole, wale wanafungisha tu ndoa talaka ikikamilika, and he was so serious, nikamwambia baba siingilii ndoa za watu kwa namna yoyote ile, na huyo ni mpaka lifo kiwatenganishe. Kuna mjinga mmoja akampa namba yangu nikamblock.


Penzi hakika halilazimishwi, kama mnalazimika kununiana na kuchuniana kudemand attention hilo siyo penzi, nna masha na long term implications.
 
Penzi halilazimushwi hakika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…