Unadhani kwa nini polisi hawamuhoji Lissu? Si kwamba kuna kitu wanakwepa? Ok kila kilichotokea pale kiko recorded si kwamba hayo maswali yote unayojiuliza majibu yake yako kwenye footages ambazo licha ya kwamba baada ya tukio cameras zikang'olewa lakini servers huwa zinahifadhi matukio yaliyorekodiwa.
Kwa nini polisi wasishirikishe Interpol kumaliza utata ili wahalifu wabainike?
Polisi huwa wanaitisha press hata kwa matukio madogo madogo kipi kinawazuia kuufahamisha umma at least kwamba wamefikia hatua fulani(bila kutoa crucial information zinazoweza kuathiri upelelezi kama upelelezi unafanyika kweli of which I doubt)
Nani alikuwa anapanga zamu za ulinzi? Kwa nini polisi hawajiulizi inakuwaje eneo linalolindwa 24/7 tena na polisi wenye silaha pamoja na security guards wa G4 Unit hawakuwepo muda ule wa shambulio.
Pale waliposhambuliwa ndani ya ile yard huwa kuna Polisi wa kubadilishana zamu yaani anaingia mmoja kumpokea mwenzake wanasaini kitabu ndipo aliyekuwepo anatoka na opposite ni nyumba aliyokuwa akiishi tulia by then alikuwa naibu spika ambapo nje ya geti huwa wapo polisi 24/7 na wanaona kila kinachotokea nyumba ya opposite polipotokea shambulio, nani aliamuru wasiwe lindoni muda ule wa shambulio?
Hii ilipangwa na watu wa usalama ila walihusisha vigogo wa polisi kuondoa walinzi wakati ule wa shambulio, upuuzi wao wakarudi tena kung'oa cameras baada ya tukio, thank God hawakufanikiwa kumuua na leo yuko na anaotoa shuhuda ya yaliyotokea otherwise kama angefariki dereva angesharudishwa kwa msaada wa Interpol na kubambikwa hiyo kesi na wangeunganishwa wengine isemwe kwamba wameuana wenyewe kwa wenyewe eti ilikuwa ni internal power struggles. Ku-survive kwa Lissu kuliharibu plans zote za Jiwe na hapo alizidi kumchukia zaidi, akili kubwa ilitumika kumkimbizia hospitali ya Nairobi otherwise ingekuwa amebaki Tanzania angemaliziwa hospitali.
Haishangazi kuona kwamba wabunge wa CCM walipigwa mikwara wasiende kumtembelea hospitali, polisi walizuia misa maalum za kumuombea zisifanyike na T-shirts zenye maneno ya kumuombea apone haraka zilipigwa marifuku. Yote ilikuwa ni amri ya Mwendakuzimu aliyekuwa amegadhibika sana kwa zoezi lake kufeli.
Hivi wasiojulikana wameyeyukia wapi? Jiwe alitengeneza kikosi hatari sana cha kuua, kuteka, kutesa na kupora mali.