Dereva wa Lissu: Sikumwambia Lissu kuwa kuna magari yanatufuata hadi nilipoegesha gari

Angekuwa Magufuli. Lissu angekuwa hana pa kukimbilia. Ni mpumbavu Tu anayeweza Amini kuwa nguvu ya Rais wa Tanzania atumie watu wakampige Risasi maeneo ambayo ya government ambapo kila mjinga Kama wewe anaweza kurelate.
Ila angekuwa sio yeye lazima kwa nguvu aliyonayo angetaja wahusika na wangegikishwa mahakamani

Issue ni kwamba jamaa alikuwa mshamba aka hire none professional kufanya kazi za professional sniper

Watu wanapiga risasi kama vichaa inamaana ata jamaa angekuwa na ka pistol angewauwa wote
 
Sio kila mtu ni mzito ndugu kuchukua maamuzi,binafsi nna matukio mengi yamenikuta hata nikusimulia unaweza kudhani ni movie ila ni uhalisia tupu.. hasa kila hatua unapojua unafuatiliwa nae ilikua sio siku yake hata wangepiga bomu
Hili la Lissu na dreva wake ukiliweka kwenye movie haiatapata waigizaji- ni usanii uliopitiliza
 
Nahisi kuna siku itatoka video ikionesha tukio lilivyotokea pale nyumbani.

Cctv si zimetengenezwa nje bhna, inawezekana kuna mifumo yao ya kutunza kumbukumbu wameiset kwenye hizo cctv so hata Kama tukio likitokea afria kule kwao Lina capture

Sasa kwa sababu za kibiashara hawawezi kuzi release, Ila miaka ya mbele mzigo utakuwa hadharani

Maoni yangu tu[emoji21]
Hivi hii habari ya CCTV na walinzi nani aliipromote?
 
Naomba kuuliza swali. Zilipigwa risasi zaidi ya 30 na wanaonyesha walipanga kuua hawa watu hizi ni risasi nyingi sana. Swali langu Je huyu dereva alipigwa risasi ngap?
Target ilikua lissu sio dereva hata ukiangalia matobo ya risasi unaona zililengwa kwenye siti ya abiria tena ubavuni isingiwezekana kupita mpaka kwa dereva bila kuzuiwa na mwili wa Lissu na kumbuka uyo dereva akukaa kwenye gari mpaka risasi zote 30 zilivyoisha kwa mujibu wa maelezo yake alipata mfadhaiko maana hajazoea mambo ya vita kwaiyo possibly jamaa aliluka nje kabla hata ya risasi 5 tu. Nahisi kule ndani either lissu aliilaza siti yake au nae alifanikiwa kuluka siti ya nyuma kitu ambacho waliopiga zile risasi hawakufukiria na ukizingatia gari ina tinted hawaoni ndani ndio maana wao wakakomaa na siti ya abiria tu.
 
Adam Mohamed Bakari, dreva wa Mh. Lissu aliyasema haya katika mahojiano yake na DW kwa mara ya kwanza akiwa nchini Ubelgiji, zaidi ya mwaka mmoja na nusu tangu kutokea kwa mashambulizi hayo.

===
Adam Mohamed Bakaria aliyekuwa Dereva wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu A. Lisu amehojiwa na DW nchini Ubelgiji ambapo ameelezea tukio la kupigwa risasi la aliyekuwa bosi wake.

Amesema baada ya kujua kuwa wanafuatiliwa alianza kuwa makini sana kwa kuwa wao hawakuwa watu wa kwenda maeneo ya club nk. Siku ya tukio amesema aliona gari mbili zinamfuata, ambapo alipunguza speed ili ziwapite lakini hazikuwapita. Baadae alijua gari hizo zinawafuatilia lakini hakumwambia Tundu Lissu.

Wakati huo alikuwa katika mwendo wa kawaida, baadae ikabidi aongeze speed na akaona ni kweli gari hizo zilikuwa zinawafuata. Baada ya kupita Club 84 alisimama na gari nyingine aina ya V8 iliwafuata kwa speed. Ilibidi aingie ndani walipokuwa wanakaa na kupark gari ambapo gari zilizokuwa zinawafuata zikapaki ndani.

Wakati huo akamwambia Lissu asishuke kwa kuwa kuna watu wanawafuatilia. Hapo wakakaa ndani ya gari ili kusubiri waliokuwa wanawafuatilia watoke ili wawajue, hata hivyo watu hao hawakushuka. Baada ya kukaa kwa muda mrefu watu hao waligeuza gari kuelekea walipotokea, baadae wakarudi reverse kwa speed na kuanza kushambulia.

Dereva wa Lissu amesema bosi wake alikuwa kushoto kwake, kwa hiyo wakati wa mashambulizi aliupigamlango kutoka nje, na alimvuta Lissu upande wake.

DEREVA ASEMA HAHUSIKI NA SHAMBULIO HILO
Adam Mohamed amesema amekuwa dereva wa Lissu kwa miaka 16 na anamchukulia kama ndugu yake na sio bosi wake. Amesema wanaosema kuwa yeye anahusika na shambulio hilo au kuwa alikimbia ni watu wasiojua hali halisi kwa kuwa walikaa Nairobi kwa miezi mitatu na hakuna aliyekwenda kuwahoji.

Aidha amesema yeye ndiye aliyempeleka Tundu Lissu, General Hospital Dodoma na polisi walikuwa wanakwenda na wanamuona na wala hawakumuhoji. Amesisitiza kuwa yeye hakukimbia wala hakufichwa, na alikuwa tayari kwa mahojiano.

Aidha amesema alipata mfadhaiko baada ya tukio hilo kwa kuwa yeye hakuzoea masuala ya vita.

View attachment 2509215
Atakua anahusika,maelezo hayatoshi, Nyakati zile maafisa wa Police walimtaka na chama kupitia hao kina Mbowe wakasema ameathirika kisaikolojia hawezi kuhojiwa yupo nje ya nchi, leo yeye anasema ndiyo alimpeleka TL hospital na alikuwepo hakuhojiwa na Police, sasa kuathirikaje kwa hivyo? Hapa hua Kuna namna inayo wahusi wao wenyewe ndani ya chama
 
Msome huyu nchangiaji

CYP Mkutubi​

3 years ago (edited)
Huyu dereva, nimeyasikiliza maelezo yake kwa umakini sana ... kuna haja kubwa sana ya kuhojiwa na Idara ya Upelelezi ya Jeshi la Polisi. Jeshi letu la Polisi halina utaratibu wa kwenda kuwahoji washukiwa nje ya nchi, wewe kama Mtanzania ulitakiwa kuhitikia wito wa Jeshi la Polisi kuja kuhojiwa Tanzania. Ulikaidi, na hata sasa hutaki kurudi Tanzania. Mwenye akili za kupembua anaona kabisa kuna siri nzito zimefichwa! Wahusika wanazidi kujificha kwa kuelekeza lawama serikalini ili wasifikiriwe! Njoo uhojiwe!! Kikulacho kinguoni mwako, ipo siku MUNGU Mwenyezi atawafunulia Wana-CHADEMA. Jiulizeni ... kwanini kila anaeinuka kuwania Uwenyekiti wa CHADEMA lazima ashambuliwe au kufa kabisa, au kunyang'anywa uwanachama kabisa?! Huyu Top kwanini yeye haya hayamkuti?? !!! CHADEMA fikirieni mara nyingine tena! Mzua pembe ndo mzika pembe!!
Show less
Wataelewa muda ukifika ingawa watakuwa wamechelewa sana
 
Swali la msingi kwa sasa ni kwa nini muda akihojiwa na DW anabadilisha kauli? Siku ya tukio aliongea na waandishi wa TZ akawaambia kuwa aliona gari inamfuata ila alipomueleza boss wake Lissu alijibu kuwa hakuna haja kujisalimisha polisi kwa usalama badala y
yake waendelee tu na safari nyumbani. Why a change? Sio kuwa kafundishwa cha kuzungumza? Au anadhani ulimwengu mzima umesahau alichosema siku ya tukio?
Huwezi kuwa consistent katika mazungumzo yaani miaka karibu sita imepita Bado awe na sentensi zile zile!! Hebu ongea kitu Sasa hivi halafu mtu akuulize jioni uone kama utaongea kilekile. Hiyo ni kanuni ya fasihi simulizi unless uwe ulirekodi au umeandika mahala. Ewe mgalatia usiye na akili ni nani aliyekuloga?
 
Target ilikua lissu sio dereva hata ukiangalia matobo ya risasi unaona zililengwa kwenye siti ya abiria tena ubavuni isingiwezekana kupita mpaka kwa dereva bila kuzuiwa na mwili wa Lissu na kumbuka uyo dereva akukaa kwenye gari mpaka risasi zote 30 zilivyoisha kwa mujibu wa maelezo yake alipata mfadhaiko maana hajazoea mambo ya vita kwaiyo possibly jamaa aliluka nje kabla hata ya risasi 5 tu. Nahisi kule ndani either lissu aliilaza siti yake au nae alifanikiwa kuluka siti ya nyuma kitu ambacho waliopiga zile risasi hawakufukiria na ukizingatia gari ina tinted hawaoni ndani ndio maana wao wakakomaa na siti ya abiria tu.
watu wameniandama sana kwa kuuliza hili swali. .

hata uwe mjinga vipi
1. Kwanza lazima uhakikishe umemaliz ushahidi na watu watakuwa wanajua dereva ni shahidi hawawezi kumuacha hai
2. Pili kama walijua wanafatiliwa na watu sio wazur inamaama walishakuwa na mashaka. Kitendo cha kuwaoma wanashuka kwenye gari na bunduki ilitakiwa wachukue tahadhari
3. Tatu mtu kama Mh Lisu ni mtu mzito ndani ya chama. Haiwezekani mpaka mda huu na brigadier yote ya ulinzi asipangiwe ulinzi na wakati alikuw hatarini

Shida hili swala kila anayezungumza analichukulia kisiasa. Ila kifupi tu halikutakiwa like kisiasa Lisu ana mke ana watoto na ndugu na wanahitaji kujua ndugu yao yuko salama. .

Ni mtazamo wangu tu. Shukrani kwa kusikiliza. .
 
watu wameniandama sana kwa kuuliza hili swali. .

hata uwe mjinga vipi
1. Kwanza lazima uhakikishe umemaliz ushahidi na watu watakuwa wanajua dereva ni shahidi hawawezi kumuacha hai
2. Pili kama walijua wanafatiliwa na watu sio waziristan inamaama walishakuwa na mashaka. Kitendo cha kuwaoma wanashuka kwenye gari na bunduki ilitakiwa wachukue tahadhari
3. Tati mtu kama Mh Lisu ni mtu mzito ndani ya chama. Haiwezekani mpaka mda huu na brigadier yote ya ulinzi asipangiwe ulinzi na wakati alikuw hatarini

Shida hili swala kila anayezungumza analichukulia kisiasa. Ila kifupi tu halikutakiwa like kisiasa Lisu ana mke ana watoto na ndugu na wanahitaji kujua ndugu yao yuko salama. .

Ni mtazamo wangu tu. Shukrani kwa kusikiliza. .
Nani amekusikilza Sasa!!!
 
1. Kwanza lazima uhakikishe umemaliz ushahidi na watu watakuwa wanajua dereva ni shahidi hawawezi kumuacha hai
Ni kweli mkuu hapa wale jamaa waliofanya kile kitendo hawakuwa makini, hata ivyo uenda mission aikwenda kama walivyopanga ukisikiliza maelezo ya dereva baada ya kumkataza lissu kushuka walisubiri sana ndani ya gari unaona hapa kila mmoja alikua anamsubiri mwenzake watu wasiojulikana wanamsubiri lissu ashuke wammalize lissu nae anasubiri watu wasiojulikana washuke ili awajue baada ya muda kwenda watu wasiojulikana wakaamua kushuka tu na kumaliza kazi maana muda unaenda na ukizingatia ilikua kipindi cha break bungeni maana angetokea tu mtu mwingine hapo mission ingekufa kwaiyo ile haraka haraka ya kukamilisha mission ndani ya muda wakajikuta wanamsahau shahidi ambaye ni dereva
2. Pili kama walijua wanafatiliwa na watu sio waziristan inamaama walishakuwa na mashaka. Kitendo cha kuwaoma wanashuka kwenye gari na bunduki ilitakiwa wachukue tahadhari
Tahadhari walichukua ikiwa ni pamoja na kusubiri ndani ya gari kwanza ili wanaowafatilia washuke wajue ni wakina nani, pia baada ya risasi kuanza kumiminwa dereva alirudisha nyumba kiti cha lissu na lissu nae akasogea upande ya nyuma zaidi ndio maana unaona risasi hazikumpata maeneo hatari zaidi ya mwili kama kifuani na kichwani labda tahadhari zipi unazoziongelea kwamba wakina lissu nao walitakiwa kuwa silaha wajibu mapigo au
3. Tati mtu kama Mh Lisu ni mtu mzito ndani ya chama. Haiwezekani mpaka mda huu na brigadier yote ya ulinzi asipangiwe ulinzi na wakati alikuw hatarini
Suala la kuwa hatarini alishasema kabla ya kushambuliwa na alitoa mpaka namba ya gari inayomfatilia akiwa dar nakumbuka waziri wa ulinzi muda huo alikua mwigulu akasema iyo gari ipo Arusha kwa lugha rahisi madai ya lissu ni batiri kivipi gari ipo Arusha imfatilie mtu yupo dar kwa maana iyo serikali ilipuuzia madai ya lissu kwamba yupo hatarini. Kuhusu suala la ulinzi pale kwenye makazi ya viongozi kuna ulinzi wa serikali kwa maana iyo hairuhusiwi kila mmoja aje na ulinzi wake binafsi ilitakiwa tuhoji walinzi wa serikali walikwepo wapi, kama hawakwepo ni nani alitoa amri waondolewe na nani aliondoa CCTV camera eneo la tukio
 
Atakua anahusika,maelezo hayatoshi, Nyakati zile maafisa wa Police walimtaka na chama kupitia hao kina Mbowe wakasema ameathirika kisaikolojia hawezi kuhojiwa yupo nje ya nchi, leo yeye anasema ndiyo alimpeleka TL hospital na alikuwepo hakuhojiwa na Police, sasa kuathirikaje kwa hivyo? Hapa hua Kuna namna inayo wahusi wao wenyewe ndani ya chama
Acha hilo , hata maelezo ya Lissu na yeye dreva yanapishana sana
 
Swali la msingi kwa sasa ni kwa nini muda akihojiwa na DW anabadilisha kauli? Siku ya tukio aliongea na waandishi wa TZ akawaambia kuwa aliona gari inamfuata ila alipomueleza boss wake Lissu alijibu kuwa hakuna haja kujisalimisha polisi kwa usalama badala y
yake waendelee tu na safari nyumbani. Why a change? Sio kuwa kafundishwa cha kuzungumza? Au anadhani ulimwengu mzima umesahau alichosema siku ya tukio?
Au wandhani Mungu ni kipofu
 
Ni kweli mkuu hapa wale jamaa waliofanya kile kitendo hawakuwa makini, hata ivyo uenda mission aikwenda kama walivyopanga ukisikiliza maelezo ya dereva baada ya kumkataza lissu kushuka walisubiri sana ndani ya gari unaona hapa kila mmoja alikua anamsubiri mwenzake watu wasiojulikana wanamsubiri lissu ashuke wammalize lissu nae anasubiri watu wasiojulikana washuke ili awajue baada ya muda kwenda watu wasiojulikana wakaamua kushuka tu na kumaliza kazi maana muda unaenda na ukizingatia ilikua kipindi cha break bungeni maana angetokea tu mtu mwingine hapo mission ingekufa kwaiyo ile haraka haraka ya kukamilisha mission ndani ya muda wakajikuta wanamsahau shahidi ambaye ni dereva

Tahadhari walichukua ikiwa ni pamoja na kusubiri ndani ya gari kwanza ili wanaowafatilia washuke wajue ni wakina nani, pia baada ya risasi kuanza kumiminwa dereva alirudisha nyumba kiti cha lissu na lissu nae akasogea upande ya nyuma zaidi ndio maana unaona risasi hazikumpata maeneo hatari zaidi ya mwili kama kifuani na kichwani labda tahadhari zipi unazoziongelea kwamba wakina lissu nao walitakiwa kuwa silaha wajibu mapigo au

Suala la kuwa hatarini alishasema kabla ya kushambuliwa na alitoa mpaka namba ya gari inayomfatilia akiwa dar nakumbuka waziri wa ulinzi muda huo alikua mwigulu akasema iyo gari ipo Arusha kwa lugha rahisi madai ya lissu ni batiri kivipi gari ipo Arusha imfatilie mtu yupo dar kwa maana iyo serikali ilipuuzia madai ya lissu kwamba yupo hatarini. Kuhusu suala la ulinzi pale kwenye makazi ya viongozi kuna ulinzi wa serikali kwa maana iyo hairuhusiwi kila mmoja aje na ulinzi wake binafsi ilitakiwa tuhoji walinzi wa serikali walikwepo wapi, kama hawakwepo ni nani alitoa amri waondolewe na nani aliondoa CCTV camera eneo la tukio
Aliyeleta hii hadithi ya walinzi hawakuwepo, CCTV kamera ziliondolewa ni CHADEMA wenyewe na hazijawahi kuthibitishwa
 
Huwezi kuwa consistent katika mazungumzo yaani miaka karibu sita imepita Bado awe na sentensi zile zile!! Hebu ongea kitu Sasa hivi halafu mtu akuulize jioni uone kama utaongea kilekile. Hiyo ni kanuni ya fasihi simulizi unless uwe ulirekodi au umeandika mahala. Ewe mgalatia usiye na akili ni nani aliyekuloga?
Mtatueleza tu vizuri
 
Naomba kuuliza swali. Zilipigwa risasi zaidi ya 30 na wanaonyesha walipanga kuua hawa watu hizi ni risasi nyingi sana. Swali langu Je huyu dereva alipigwa risasi ngap?
Kamuulize yeye, si yuko ubeljiji
 
Back
Top Bottom