Dereva wa Lissu: Sikumwambia Lissu kuwa kuna magari yanatufuata hadi nilipoegesha gari

Dereva wa Lissu: Sikumwambia Lissu kuwa kuna magari yanatufuata hadi nilipoegesha gari

😆😄😆 aisee we jamaa mjuaji sana
Nimeuliza swali kwa jinsi gari lilivyomiminiwa risasi haziwez kuwa zimempata mtu mmoja inakuwaje dereva hakupatwa na risasi ambazo zilimpatq mweshimiwa Lissu pekee?

wewe mwenye akili nyingi nifafanulie sijauliza kiushabiki wa kisiasa.
Waulize waliofyatua risasi kwa nini hawakumlenga dereva? Hao tu ndio wanaweza kukupa jibu la uhakika.
 
Huwezi kuwa consistent katika mazungumzo yaani miaka karibu sita imepita Bado awe na sentensi zile zile!! Hebu ongea kitu Sasa hivi halafu mtu akuulize jioni uone kama utaongea kilekile. Hiyo ni kanuni ya fasihi simulizi unless uwe ulirekodi au umeandika mahala. Ewe mgalatia usiye na akili ni nani aliyekuloga?
Kuwa masharki wakati ulikuwa mgharibi ni kitu ambacho hakiwezekani kamwe
 
😆😄😆 aisee we jamaa mjuaji sana
Nimeuliza swali kwa jinsi gari lilivyomiminiwa risasi haziwez kuwa zimempata mtu mmoja inakuwaje dereva hakupatwa na risasi ambazo zilimpatq mweshimiwa Lissu pekee?

wewe mwenye akili nyingi nifafanulie sijauliza kiushabiki wa kisiasa.
Kwani walikuwa wanazipiga risasi randomly au walikuwa wanalenga target? Kama walikuwa wanalenga target basi kilichotokea sio maajabu.
 
Adam Mohamed Bakari, dreva wa Mh. Lissu aliyasema haya katika mahojiano yake na DW kwa mara ya kwanza akiwa nchini Ubelgiji, zaidi ya mwaka mmoja na nusu tangu kutokea kwa mashambulizi hayo.


===
Adam Mohamed Bakaria aliyekuwa Dereva wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu A. Lisu amehojiwa na DW nchini Ubelgiji ambapo ameelezea tukio la kupigwa risasi la aliyekuwa bosi wake.

Amesema baada ya kujua kuwa wanafuatiliwa alianza kuwa makini sana kwa kuwa wao hawakuwa watu wa kwenda maeneo ya club nk. Siku ya tukio amesema aliona gari mbili zinamfuata, ambapo alipunguza speed ili ziwapite lakini hazikuwapita. Baadae alijua gari hizo zinawafuatilia lakini hakumwambia Tundu Lissu.

Wakati huo alikuwa katika mwendo wa kawaida, baadae ikabidi aongeze speed na akaona ni kweli gari hizo zilikuwa zinawafuata. Baada ya kupita Club 84 alisimama na gari nyingine aina ya V8 iliwafuata kwa speed. Ilibidi aingie ndani walipokuwa wanakaa na kupark gari ambapo gari zilizokuwa zinawafuata zikapaki ndani.

Wakati huo akamwambia Lissu asishuke kwa kuwa kuna watu wanawafuatilia. Hapo wakakaa ndani ya gari ili kusubiri waliokuwa wanawafuatilia watoke ili wawajue, hata hivyo watu hao hawakushuka. Baada ya kukaa kwa muda mrefu watu hao waligeuza gari kuelekea walipotokea, baadae wakarudi reverse kwa speed na kuanza kushambulia.

Dereva wa Lissu amesema bosi wake alikuwa kushoto kwake, kwa hiyo wakati wa mashambulizi aliupigamlango kutoka nje, na alimvuta Lissu upande wake.

DEREVA ASEMA HAHUSIKI NA SHAMBULIO HILO
Adam Mohamed amesema amekuwa dereva wa Lissu kwa miaka 16 na anamchukulia kama ndugu yake na sio bosi wake. Amesema wanaosema kuwa yeye anahusika na shambulio hilo au kuwa alikimbia ni watu wasiojua hali halisi kwa kuwa walikaa Nairobi kwa miezi mitatu na hakuna aliyekwenda kuwahoji.

Aidha amesema yeye ndiye aliyempeleka Tundu Lissu, General Hospital Dodoma na polisi walikuwa wanakwenda na wanamuona na wala hawakumuhoji. Amesisitiza kuwa yeye hakukimbia wala hakufichwa, na alikuwa tayari kwa mahojiano.

Aidha amesema alipata mfadhaiko baada ya tukio hilo kwa kuwa yeye hakuzoea masuala ya vita.

View attachment 2509215

Naon mataga wazee wa legacy mnapima upepo, ila kila mmoja atapata haki yake hapahapa dunian kwa udhalimu ule!!
 
Ni kweli kupigwa risasi kwa lissu ni tukio lililopangwa kijinga na watu wajinga,nje ya siasa,lissu ana maisha yake mengine,hivyo huwez kujua,lkn kuihusisha serikali na huo upuuzi,inabidi uwe na Akili mbirikimo na fikra zenye matege.
Chain of events inaonyesha kwamba serikali ilihusika kupanga, kuratibu na kutekeleza shambulio lile vinginevyo kwa kuhusishwa Jiwe kama suspect namba moja angehakikisha culprits wanakamatwa na wangetumikia kifungo fasta.
Ukimya wa polisi na hata kushindwa kwao kukanusha hivi Lissu anavyosema muhusika au mtoa amri wa shambulio lile ni Magu ujue wanaogopa mambo yasifukuliwe, wanashindwa nini kumwambia atoe ushahidi kwa nini anasema kwenya vyombo vya habari kwamba Magu ndiyo aliyetoa order ashambuliwe.
 
Ila angekuwa sio yeye lazima kwa nguvu aliyonayo angetaja wahusika na wangegikishwa mahakamani

Issue ni kwamba jamaa alikuwa mshamba aka hire none professional kufanya kazi za professional sniper

Watu wanapiga risasi kama vichaa inamaana ata jamaa angekuwa na ka pistol angewauwa wote
Kina Makonda na mitako ile watoe wapi shabaha.
 
Hivi hii habari ya CCTV na walinzi nani aliipromote?
Good question.
-Na swali jingine ni 'kwa nini polisi hawaongelei zilipo footages za CCTV cameras na ni akina nani walipaswa kuwa lindoni na kwanini hawakuwepo?'
-Je kwani polisi hawajui nani walikuwa wahusika wa kupanga ratiba ya polisi wanaolinda pale wakati ni polisi wenzao? Je wanalindana?
-Yaani makundi mawili tofauti ya polisi na G4 security guards wote wakosekane sehemu inayopaswa kulindwa 24/7? Hii si coincidence bali ni pattern ambayo inajidhihirisha kabisa.
 
Msome huyu nchangiaji

CYP Mkutubi​

3 years ago (edited)
Huyu dereva, nimeyasikiliza maelezo yake kwa umakini sana ... kuna haja kubwa sana ya kuhojiwa na Idara ya Upelelezi ya Jeshi la Polisi. Jeshi letu la Polisi halina utaratibu wa kwenda kuwahoji washukiwa nje ya nchi, wewe kama Mtanzania ulitakiwa kuhitikia wito wa Jeshi la Polisi kuja kuhojiwa Tanzania. Ulikaidi, na hata sasa hutaki kurudi Tanzania. Mwenye akili za kupembua anaona kabisa kuna siri nzito zimefichwa! Wahusika wanazidi kujificha kwa kuelekeza lawama serikalini ili wasifikiriwe! Njoo uhojiwe!! Kikulacho kinguoni mwako, ipo siku MUNGU Mwenyezi atawafunulia Wana-CHADEMA. Jiulizeni ... kwanini kila anaeinuka kuwania Uwenyekiti wa CHADEMA lazima ashambuliwe au kufa kabisa, au kunyang'anywa uwanachama kabisa?! Huyu Top kwanini yeye haya hayamkuti?? !!! CHADEMA fikirieni mara nyingine tena! Mzua pembe ndo mzika pembe!!
Show less
Jeshi halina utaratibu wa kuhoji watu nje ya nchi? Utakuwa mshamba sana au illiterate au unajitoa tu ufahamu.
-Kwa taarifa yako polisi wakimuhitaji mtuhumiwa wanampata, kuna utaratibu wa kuwarudisha kwa either kutumia Interpol au kutumia vyombo vya usalama vya nchi husika.
 
Lisu amesharejea nyumbani ,huyo dereva yuko wapi ,mbona anaonekana lisu tu peke yake !!?
Nini kinawazuia polisi kumuhoji Lissu?
Yaani kijana ameshapata ajira ya kudumu tena Ulaya aende tena mavumbini akawe dereva? Wamuhoji Lissu kama wako serious na upelelezi.
 
Nadhani huyu dereva anajua mengi sana kuhusu hilo tukio
 
Mungu asipopanga jambo lake hakuna anaeweza kufanya iwe.

Wengine wameshaoza ila lissu anatamba mjini
 
Msome huyu nchangiaji

CYP Mkutubi​

3 years ago (edited)
Huyu dereva, nimeyasikiliza maelezo yake kwa umakini sana ... kuna haja kubwa sana ya kuhojiwa na Idara ya Upelelezi ya Jeshi la Polisi. Jeshi letu la Polisi halina utaratibu wa kwenda kuwahoji washukiwa nje ya nchi, wewe kama Mtanzania ulitakiwa kuhitikia wito wa Jeshi la Polisi kuja kuhojiwa Tanzania. Ulikaidi, na hata sasa hutaki kurudi Tanzania. Mwenye akili za kupembua anaona kabisa kuna siri nzito zimefichwa! Wahusika wanazidi kujificha kwa kuelekeza lawama serikalini ili wasifikiriwe! Njoo uhojiwe!! Kikulacho kinguoni mwako, ipo siku MUNGU Mwenyezi atawafunulia Wana-CHADEMA. Jiulizeni ... kwanini kila anaeinuka kuwania Uwenyekiti wa CHADEMA lazima ashambuliwe au kufa kabisa, au kunyang'anywa uwanachama kabisa?! Huyu Top kwanini yeye haya hayamkuti?? !!! CHADEMA fikirieni mara nyingine tena! Mzua pembe ndo mzika pembe!!
Show less
Urukeruke utakavyoruka lakini bayana suspect namba moja atabaki kuwa Mwendakuzimu.
Kuna namna nyingi za kupeleleza kesi, kwani dereva angekufa kwenye tukio ndiyo na upelezi ungefia hapohapo?
Ipo siku footages za CCTV cameras zitavujishwa na polisi asiyekubali uonevu na hao polisi waliozificha wataumbuka, hata kama polisi wamezifuta kuna namna somewhere kwenye servers au hata system ya kampuni ilyotengeneza au iliyofanya installation kutakuwa na copies za footages na baadhi ya polisi au usalama wa taifa wataumbuka kwa sura zao kubainika.
A picture speaks thousand words, kwa nini tuzunguke na longolongo wakati video footages za tukio zima zilirekodiwa kwenye CCTV cameras?
 
Msome huyu nchangiaji

CYP Mkutubi​

3 years ago (edited)
Huyu dereva, nimeyasikiliza maelezo yake kwa umakini sana ... kuna haja kubwa sana ya kuhojiwa na Idara ya Upelelezi ya Jeshi la Polisi. Jeshi letu la Polisi halina utaratibu wa kwenda kuwahoji washukiwa nje ya nchi, wewe kama Mtanzania ulitakiwa kuhitikia wito wa Jeshi la Polisi kuja kuhojiwa Tanzania. Ulikaidi, na hata sasa hutaki kurudi Tanzania. Mwenye akili za kupembua anaona kabisa kuna siri nzito zimefichwa! Wahusika wanazidi kujificha kwa kuelekeza lawama serikalini ili wasifikiriwe! Njoo uhojiwe!! Kikulacho kinguoni mwako, ipo siku MUNGU Mwenyezi atawafunulia Wana-CHADEMA. Jiulizeni ... kwanini kila anaeinuka kuwania Uwenyekiti wa CHADEMA lazima ashambuliwe au kufa kabisa, au kunyang'anywa uwanachama kabisa?! Huyu Top kwanini yeye haya hayamkuti?? !!! CHADEMA fikirieni mara nyingine tena! Mzua pembe ndo mzika pembe!!
Show less
Acha kuwa na akili finyu. Yaani makazi ya viongozi yanayolindwa Chadema wawe na uwezo wa kuwaondoa walinzi wa serikali?
 
Naomba kuuliza swali. Zilipigwa risasi zaidi ya 30 na wanaonyesha walipanga kuua hawa watu hizi ni risasi nyingi sana. Swali langu Je huyu dereva alipigwa risasi ngap?
Kwa mfano ukijua Ni mbili au hakuna iliempata itafanyaje au kuhusika vp kujua walioshambulia

Kuna maswali ya kikuda Sana mtu mwenyewe akili timamu hawezi uliza
 
Target ni Lissu ndio upande ulioshambuliwa na matundu yalionekana baada ya kufyatua risasi dereva akailaza siti yake pamoja na ya lissu na lissu Alilalia tumbo huku akiwa amesogea zaidi siti ya nyuma ya abiria ,sasa wale kina makonda wakawa wanamimina tuu risasi hovyo upande wa abiria pasipo kumrushia risasi upande wa dereva na tinted ilisaidia wakiendeleea kumimina risasi dereva alikua ameshashuka na kukaa ubavuni mwa tairi ya gari ...

Nimeamua nikujibu wewe moja kwa moja ili ukakojoe ukalale huko View attachment 2508644
Wapigaji was mwendazake Ni manyumbu Sana


I swear kwa movie za Vita nilizoangalia hakuna mtu angechomoka kwenye hio gari kwa risasi walizotumia ,,


Sema ndo hivo aliewatuma akili Hana na wapigaji akili hawana
 
Angekuwa Magufuli. Lissu angekuwa hana pa kukimbilia. Ni mpumbavu Tu anayeweza Amini kuwa nguvu ya Rais wa Tanzania atumie watu wakampige Risasi maeneo ambayo ya government ambapo kila mjinga Kama wewe anaweza kurelate.

Mission za mtu wa Serikali alihitaji Risasi moja Tu. Na Hata kuwa kwake ubelgiji asingepona. Hao wakina kagame wanatuma watu mpaka marekani na utauliwa. Lissu Hakuwa na lolote na kumfanya Rais amwone tishio.

Lissu Ni Kama wale wanafunzi wa sekondari ambao lazima abishane kwa ajili ya cheap popularity. Lakini kwenye maslahi yake wala haongei. Kwa namna ya CHADEMA ilivyo na uenyekiti wa mbowe miaka yote hii na hulka mnayompachika Lissu pasingeiva.

Shetani na nusu uliza Museveni. Kagame. Paul B wa Cameroon nk. Tanzania ni tamu sana. Endeleeni Tu kuishi kwa ujinga ujinga.
Yaani hapo umeona umetoa bongeee la hoja yaraabi!!?

Kwamba Lissu ana uwezo wakuwaondoa walinzi wa serikali ambao muda wote wanakuwepo eneo la makazi ya viongozi wa serikali kama mawaziri na wabunge?

Kwamba Lissu ndiye aliyeng'oa CCTV camera ili tukio lisionekane?

Chadema waliomba interpol hasa FBI waje wasaidiane na polisi wetu kufanya uchunguzi wa tukio lakini mamlaka ziligoma kabisa wakisema polisi wetu wana weledi mkubwa kwenye uchunguzi hivyo ndani ya siku 21 tu ripoti ya uchunguzi itakuwa wazi.

Hadi leo ni miaka kadhaa imepita pamekuwa kimya hata file la uchunguzi halijulikani lilipo.
 
Dreva analaumu polis kwann hawakumuohoji lisu akiwa general hospital?

Hivi amewaza nini? Na
Ni kwa uwezo gani au namna gani risas 38 zote 17 lisu tu zote yeye alikuwa wapi?
 
Target ni Lissu ndio upande ulioshambuliwa na matundu yalionekana baada ya kufyatua risasi dereva akailaza siti yake pamoja na ya lissu na lissu Alilalia tumbo huku akiwa amesogea zaidi siti ya nyuma ya abiria ,sasa wale kina makonda wakawa wanamimina tuu risasi hovyo upande wa abiria pasipo kumrushia risasi upande wa dereva na tinted ilisaidia wakiendeleea kumimina risasi dereva alikua ameshashuka na kukaa ubavuni mwa tairi ya gari ...

Nimeamua nikujibu wewe moja kwa moja ili ukakojoe ukalale huko View attachment 2508644
Muda wa kugeuk mpaka kulalia tumbo hapana mnatupanga nafasi ya ile siti na sehem ya miguu sio rahis kugeuka katika mazingira yale
 
Back
Top Bottom