Dini zimechangia kudumaza ufahamu wa mwafrika

Hili tunalijua miaka mingi sana imepita ndiyo maana wa TZ a tunajichanganya tu, x mass, IDD EL FITR zwooote tuna sherehekea tunaishi kiujirani zaidi na kuoleana hatubagui. kwa sababu zilisha kuja zitaondoka tuuu
 
Waafrika bwana,tukizidiwa kete na mzungu tunaanza kusingizia dini.Kwani hizi dini zina muda gani hapa nchini?

Mbona kabla ya ujio wa hizi dini hatukuwa hata na maendeleo yoyote yale?
Tuache kusingizia dini Bwana!
 
Waafrika tungekuwa wavivu kama unavosema tusingeijenga marekani na ulaya. Acha kuchukia waafrika wenzako.

Self hate ndo inatusumbua. Yani unadiriki kuandika gazeti kwa ajili ya kupinga positivity. Stop that brother.
Naona huelewi maana ya neno "uvivu" pia uache kukariri kuwa mtu akikukosoa au akikuambia ukweli usioupenda kuusikia maana yake anakuchukia. Kwa taarifa yako Marekani haikujengwa na Waafrica lakini pia wale weusi unaowaona kule siyo Waafrica bali ni Wamarekani weusi, japo kuwa weusi wana asili ya Africa lakini siyo Waafrica usikariri.

Ukiwa Kiongozi muungwana jitahidi kupata kupokea mawazo tofauti hata kama mawazo hayo huyapendi, sasa kwa baadhi ya Waafrica na Viongozi wa Afrika huu ni mtihani na tabia ya kutopenda kuambiwa ukweli haianzii kwa Viongozi bali inaanzia ngazi ya familia, angalia hata kwenye mitandao ya kijamii hususan Facebook, ikitokea mtu akaweka picha yake ukamsifia atafurahi lakini ukimkosoa anaweza hata kukufungia (block) hiki ni kiashiria cha kutopenda mawazo mbadala.
 
Waafrika bwana,tukizidiwa kete na mzungu tunaanza kusingizia dini.Kwani hizi dini zina muda gani hapa nchini?
Sijasingizia dini bali ni uhalisia au wewe unaweza kuniambia kwanini wazungu wametuzidi hizo kete?
Mbona kabla ya ujio wa hizi dini hatukuwa hata na maendeleo yoyote yale?
Tuache kusingizia dini Bwana!
Ndio maana nikasema dini zimechangia kudumaza ufahamu wa mwafrika sababu mwafrika alikuwa na ufahamu uliodumaa hapo kabla.
 
Siyo kweli kuwa kabla ya kuja kwa dini hakukuwa na maendeleo yoyote Africa, yalikuwepo na watu walikuwa wameishajikusanya na kuwa na utawala (hayo siyo maendeleo!!) Kule Bukoba watu walikuwa wanafua vyuma na kutengeneza majembe ya kulimia, visu na mapanga ya kukatia. pia wazungu walikuta tumeshagundua moto hivyo tunakula vyakula vilivyopikwa. kulikuwepo na shughuli za kilimo na ufugaji ndiyo maana watu walipata chakula cha kutosha.

Kilichotokea ni kuwa Wazungu na Waarabu walikuwa na akili kubwa kuliko sisi, hivyo waliweza kudidimiza maendeleo yale kwa njia mbalimbali ikiwemo dini kwa kutuaminisha kuwa MUNGU hapendi mambo yaliyokuwa yakifanywa na Babu zetu na pia walitoa misaada iliyosaidia kuzuia kuambukiza elimu ya uhunzi, utabibu na mambo mbalimbali kutoka kizazi kimoja hadi kingine. UKWELI NI KWAMBA HAYO YOTE YALITOKANA NA KUZIDIWA AKILI (japo roho inaniuma lakini ndiyo ukweli)
 
UKWELI NI KWAMBA HAYO YOTE YALITOKANA NA KUZIDIWA AKILI
Mkuu tumia facts na sio hisia.

Kabla ya kusema wazungu wametuzidi akili itabidi utuelezee kwako akili ni nini.
Na jinsi gani wazungu wametuzidi akili?
Sababu haiwezekani ukageneralize kitu ambacho hakijafafanuliwa.

Kwako akili ni nini?
Na jinsi gani wazungu wametuzidi akili?

Tumia facts mkuu.
 
Mwambi kama yeye ni mwafrika na anahisi hana akili ni yeye sio wote. Hana akili as individual sio wote.
 
Huna akili wewe as an individual. Kutokua na akili wewe usijumuishe na waafrika wenzako
 
Wewe ni nani jf wa kuniambia mimi nirekebishe mada yangu?

Una mamlaka yoyote kuniambia hivyo?
Unadhani kwanini mods wameipitisha?
Aisee ukristo sio dini acha kubishana ukirekebishwa
 

Ila natumaini unajua tofauti kati ya :

Dini na Imani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…