Uchaguzi 2020 Dkt. Bashiru: Wanaotegemea Tume Huru iwape ushindi wanajidanganya! Tume haipigi kura

Uchaguzi 2020 Dkt. Bashiru: Wanaotegemea Tume Huru iwape ushindi wanajidanganya! Tume haipigi kura

Kuna mchangiaji mmoja kasema kuwa hawa watu wakisha kabidhiwa madaraka ndani ya chama basi sharti lao kuu ni kukabidhi weredi wao kwa wateuzi

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni kweli kabisa mkuu.

Huwezi kutegemea kauli kama hiyo itolewe na mtu anayejiita Dr.

Nadhani ana ugonjwa wa ulevi wa madaraka pia!
 
Hamjajua kiini cha mambo! Hata wakati wa Katiba Mpya wapinzani waliingia kichwa kichwa wakachezeshwa mchakamchaka baadae wakakimbia ukumbi na mechi ikaisha kwa kufungwa mabao 2 kwa 0. Hata hili nina uhakika Mfumo wa CCM utawafunga 2 kwa Zero kwa kuwa mna vichwa maji. Dr. Bashiru wakaonyesha kiduchu lakini badala ya kufikiri zaidi ndiyo kwanza wanamubeza!!
Kumbe kwenye katiba mpya tulikuwa tunashindana?sikujua mkuu basi hongereni kwa ushindi
 
Hivi Bashiru nae ni PhD holder? ccm anafanya biashara gani za kuweza kutoa elimu bure kwa watanzania,au kujenga barabara na miundombinu ya maji,Kama ana PhD basi nchi yetu itakuwa imepigwa laana si bure,sasa Kama msomi wa PhD anafanya siasa za level ya Msukuma Kuna nini tena hapo
Hizi PhD za CCM ndiyo zinatuletea ushindi bila kupingwa
 
huyu ni msomi mpumbavu hata kama mwalimu wangu. sijui kwann dr. bashiru amekuwa mpumbavu hivi tangu awe GS Wa ccm
shida sio bashiru shida ni ccm hata wewe ukishakuwa ccm tutakushangaa kuwa umepatwa na nini. siku akitoka ccm atarudi kwenye ubora wake
 
Kuna comments zimenishangaza humu, jamani huyu jamaa hata alipokuwa UDSM hakuwa na ubora wowote both as an academic and political analyst. Alipokuwa huko UDSM nimemsikiliza sana especially alipokuwa akihojiwa au kuombwa kutoa maoni mbali mbali na BBC na DW, upeo wake ni mdogo, anazidiwa mbali na waandishi na wachambuzi ambao hawana hata degree mbili, na kama nilivyowahi kusema humu, huyu jamaa hana kabisa objectivity ya mwanataaluma. Ni dishonest na mnafiki.

Kama anajua tume huru haipigi kura, basi yeye na hicho chama chake na serikali waruhusu mchakato wa kuipata hiyo tume. Na sio tu tume na katiba mpya pia. Kama wame deliver na kuperform kiasi hicho, uwoga wa nini? Yamevuruga mpaka chaguzi za serikali za mitaa, eti yameshinda kwa kwa 99%. Siku hizi hata aibu hayana.
 
Under pressure Bashiru is singing his master's voice. He is sandwiched between the ruthless forces of oppression and tyranny.
 
Binafsi nimeshindwa kumuelewa kabisa huyu bwana mkubwa wa CCM.

Maneno aliyo yaongea na elimu aliyo nayo sidhani kama vinaendana.

HOTUBA YA DR. BASHIRU KWA UFUPI

CCM inatoa salamu za mwaka mpya 2020, niwahakikishie watanzania kuwa tutaongoza siasa safi,ni mwaka wa kuheshimu maoni na uamuzi wa Umma, na tutashinda kwa kishindo kwa kuwa wananchi walihitaji huduma ya maji, elimu bure, afya na sasa wanapata huduma hizo,wananchi sio wanafiki.

CCM inapingana na udhalilishaji unaojitokeza ktk chaguzi, Wanawake kabla ya kugombea wanaitwa majembe, wakichukua fomu za kugombea wanaanza kuchimbwa na kupewa kashfa,wanajazwa hofu na wanaogopa, awamu hii CCM haitakubali wanawake wadhalilishwe na haki ni lazima itendeke kwa wote.

Wapo wanaolilia tume huru iwasaidie kupata ushindi, tume haipigi kura bali inasimamia uchaguzi, chama kisicho na wapigakura kisitegemee tume iwape ushindi, CCM imetafuta wapigakura kwa kutoa elimu bure, afya, maji na barabara, wao waseme wapiga kura wamewapataje.

Wenyeviti wa vijiji na mitaa, ninyi ni wajumbe wa vikao vya CCM kwenye Matawi na Kata, mtusaidie kupata wagombea bora, ikiwa mnaona kuna watu wanawazidi nguvu na kupendekeza wagombea wasio na sifa kwa maslahi yao, leteni taarifa haraka kusaidia Chama.

He is trying to brain wash those who have shallow mind to make them forget what happened during street chairmanship elections for 2019

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi nimeshindwa kumuelewa kabisa huyu bwana mkubwa wa CCM.

Maneno aliyo yaongea na elimu aliyo nayo sidhani kama vinaendana.

HOTUBA YA DR. BASHIRU KWA UFUPI

CCM inatoa salamu za mwaka mpya 2020, niwahakikishie watanzania kuwa tutaongoza siasa safi,ni mwaka wa kuheshimu maoni na uamuzi wa Umma, na tutashinda kwa kishindo kwa kuwa wananchi walihitaji huduma ya maji, elimu bure, afya na sasa wanapata huduma hizo,wananchi sio wanafiki.

CCM inapingana na udhalilishaji unaojitokeza ktk chaguzi, Wanawake kabla ya kugombea wanaitwa majembe, wakichukua fomu za kugombea wanaanza kuchimbwa na kupewa kashfa,wanajazwa hofu na wanaogopa, awamu hii CCM haitakubali wanawake wadhalilishwe na haki ni lazima itendeke kwa wote.

Wapo wanaolilia tume huru iwasaidie kupata ushindi, tume haipigi kura bali inasimamia uchaguzi, chama kisicho na wapigakura kisitegemee tume iwape ushindi, CCM imetafuta wapigakura kwa kutoa elimu bure, afya, maji na barabara, wao waseme wapiga kura wamewapataje.

Wenyeviti wa vijiji na mitaa, ninyi ni wajumbe wa vikao vya CCM kwenye Matawi na Kata, mtusaidie kupata wagombea bora, ikiwa mnaona kuna watu wanawazidi nguvu na kupendekeza wagombea wasio na sifa kwa maslahi yao, leteni taarifa haraka kusaidia Chama.

Ukivimbiwa unakua hujui kwamba unesema hakuna tume huru ya uchaguzi
 
Ndugu yangu ,Kakurwa,Tume ya uchaguzi ambayo inachaguliwa na chama kimoja kuna mashaka kama yawezekana ku exercise impartiality wananchi wanaingia kwenye uchaguzi wakiwa na mashaka.Walio madarakani wanatamani kushida hata goli la mkono inaskitisha.
 
Back
Top Bottom