Amani iwe nanyi wana wa MUNGU
Leo nikifatilia kongamano la Ekaristi takatifu nimemuona baba Padre Kitima akiwapandisha madhabahuni katibu mkuu wa CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi, Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika na Makamu Nwenyekiti wa CHADEMA-Bara, Tundu Lissu.
Tuendelee kuliombea amani taifa letu dhidi ya watu wenye roho za kuliangamiza na kututenganisha.
Watu muda wote wanawaza kuua kila asiye waunga mkono
Wanataka wapendwe lakini watanzani wamegoma kabisa kuwapenda
LONDON BOY
====
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Padri Dk Charles Kitima amewaita mbele ya kongamano la tano la Ekaristi Takatifu, Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi na Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, Tundu Lissu pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika kwa ajili ya kusalimia waumini.
Kongamano hilo linafanyika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, leo Jumapili, Septemba 15, 2024.
Mbali nao, viongozi wengine wa kisiasa waliohudhuria ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko na Waziri wa Ujenzi, Innoncent Bashungwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila na Spika mstaafu, Anne Makinda.
Pia maaskofu, mapadri, watawa wa kiume na kike na waumini wa kanisa hilo wamejitokeza kwa wingi kushiriki kongamano hilo lililofunguliwa Septemba 12, 2024.
Pia soma: Maaskofu Katoliki: Tunu yetu ya amani nchini imeshambuliwa kutokana na matukio ya watu kutekwa na kuuawa ya hivi karibuni