Dkt. Jakaya Kikwete amtunuku Rais Samia Shahada ya Udaktari wa Heshima UDSM. Sasa ni Dkt. Samia

Hongera Mh DR. SSH. Unaupiga mwingi sana hadi unamwigika
 
Rais Samia amekabidhiwa shahada ya udaktari wa heshima kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam leo wakati wa mahafali ya 52 duru ya 5. UDSM imesema uongozi wa Rais Samia umeleta mageuzi ya kiuchumi na mengineyo, pia umeleta tumaini jipya.
Ametunukiwa au amekabidhiwa?
 
Nadhani itakuwa Doctorate ya Mgao wa Maji na Umeme.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Nipo hapa kijiweni shughuli zangu zimesimama tangu saa 5 asubuhi kisa umeme umekatwa.
 
Rais Samia amekabidhiwa shahada ya udaktari wa heshima kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam leo wakati wa mahafali ya 52 duru ya 5. UDSM imesema uongozi wa Rais Samia umeleta mageuzi ya kiuchumi na mengineyo, pia umeleta tumaini jipya...
Hizi PhD za mchongo nyingi zilianza enzi za utawala wa Kikwete!
 
Naona hii inaenda kufunika title ya uchifu......mwenye prospectus ya UD atuwekee vigezo vya kutunukiwa honorary degree na siye tulio huku nyambitilwa tupitishe macho kidogo.
 
Hakika Anastahili katika hili maana nimewahi kupendekeza kupitia jukwaa Hili kuwa Chuo kikuu Cha Dares Salaam kimpatie shahada ya udaktari wa Heshima kwa kazi kubwa aliyoifanya nchi yetu

Hata usingependekeza bado hicho chuo kingempa. Vyuo vya uswahilini kutoa nyadhifa kwa viongozi wa kisiasa ni fashion. Na mara nyingi sio lazima awe na sifa husika, bali ni mambo ya kienyeji tu.
 
Eti mchango kwenye jamii.

Ilaa hawa watuuu.
 
Kaka Nina family inanitegemea haha
Hiki ni kiwango cha juu kabisa cha kumpaka mafuta.

Hakuna atacholetewa na jamaa hao akawakatalia.

Wanatumia akili sana kumvuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…