Dkt. Mollel: Ni ujinga Waziri kutoa Data za Walioathiriwa na Corona kila siku. Bei ya chanjo ni Tsh 400,000

Dkt. Mollel: Ni ujinga Waziri kutoa Data za Walioathiriwa na Corona kila siku. Bei ya chanjo ni Tsh 400,000

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Jinsia Wazee na Watoto amesema watu wengi wanasema Tanzania haitoi data, ambapo amesema data haina haja ya kutangazwa kila siku na Waziri, utakuwa ni ujinga mtupu...
Nchi imeachafuka kiasi hiki? Kwamba proffesional yako uliyonayo inadhalilishwa na uluwa/njaa mpaka unafikia kubadilisha maneno kuongea kisicho sahihi. Inasikitisha sana.

Nimekuwa nikiona watanzania wengi wakichukua PHd zao ulaya, america na huko Asia ambako ndiko chanzo cha huu ugonjwa na wataalamu wao kusema sasa kuna CoronaVirus lakini bado Mtanzania anabalisha maneno na kuleta ujuaji hii ina maana gani hasa kwa vizazi vijavyo? Taifa gani linaenda kujengwa
 
Kinachonisikitisha ni wachache watamuelewa, hongera kwa serikali ya awamu ya 5
 
Misplaced argument!! Magonjwa yote uliyotaja ikiwemo na corona hutolewa data. Kinachotakiwa ni kutoa hizo data kwa vyombo husika, hata kama itakuwa mara moja kwa mwezi. Kama hujui hili basi wewe ni layman - data za kila siku zinaonesha upimaji na kwa kuwa upimaji unapaswa kufanyika kila siku wanakwepa hitaji hilo. Lakini kama Dr. Mollel anasema data huwasilishwa kwa mwezi - sio vibaya. Tatizo ni kutowasilishwa kabisa ili kuleta picha kuwa vifo vyote havina uhusiano na covid-19!!
sijasema data hazipo,
data za magonjwa yote zipo na zinatumiwa ktk mipango mingine ya kisayansi ya kukabiliana na maradhi husika.
kinacho semwa na naibu waziri ni kuwa hakuna sababu ya kuanika data kila wakati isipo kuwa kwa taasisi zinazo husiana na mambo ya afya.
sasa wewe raia wa kawaida unazitaka data ili zikusaidie nini ? !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walishasema Corona hamna mbona wanajitekenya halafu wanacheka
 
Amesema Data huwa inataka uchakataji ili kujua tatizo ya magonjwa yanayosababisha vifo na kujua namna ya kuyakabili.
Mh. Waziri yuko sahihi. Unatangaza data za wanaokufa ili iweje? Ili wananchi wawe na hofu? Tangaza mikakati ya watu kujikinga na magonjwa, hatushindani kwa idadi ya watu wanaokufa, ni ujinga
 
Abaki kwenye fani yake ya dentistry awaachie md specialist wa internal medicine na nyinginezo watoe mchakato wa magonjwa.
Maelezo alivyo yatoa hayahitaji uwezo wa juu sana kuogelea. Yeyote aliye fanya medicine hata kiwango cha Clinical officer anatakiwa kufahamu na kuelezea. Tusifanye hili ni tatizo COVID -19 la ajabu sana katika field ya medicine.
 
Naibu waziri akieleza sababu za kwanini Serikali hawataki Chanjo ataja na sababu nyingine Muhimu kuwa chanjo moja Ni 400,000 Tzsh yaan gharama kubwa sana.



Hilo,
 
Hata ingekuwa bure haitakiwi kuwa lazima... Hii inatakiwa kubaki kuwa hiari ya mtu mwenyewe
 
Kuna muda mwingine wanakuaga sawa ila sasa wakivuta bangi mbona mtawakubali😂😂😂
 
Back
Top Bottom