Dkt. Slaa ahutubia mkutano wa CHADEMA. Asema sasa imekomaa kuongoza nchi

Dkt. Slaa ahutubia mkutano wa CHADEMA. Asema sasa imekomaa kuongoza nchi

Jaribu kufuatilia siasa za Kenya, hayo mambo ni kawaida sana
Kama hayo mambo yakionekana kawaida, basi na vyama vyetu vya upinzani vingi vitaonekana vya kawaida pia.

Mambo ya kawaida hufanywa na watu wa kawaida.
 
Kama hawangemtibua Silaa ungekuta Chadema wapo juu sana. Alijitahidi kukiondoa chama kwenye mfuko wa mtu mmoja ila akamwaga manyanga.
Kwann asingebaki CCM aifikishe mbali? Kama ana misingi anayoisimamia against utawala kwann alirudi utawalani akala teuzi?
 
Kama hawangemtibua Silaa ungekuta Chadema wapo juu sana. Alijitahidi kukiondoa chama kwenye mfuko wa mtu mmoja ila akamwaga manyanga.
Dhana ya Chadema kuwepo juu kutokana na mtu fulani ilimdanganya Mwendazake akawapa vyeo akina Silaa, Silinde, Nassari, Lijuakali na wengine, huku akiwapa Ubunge Halima Mdee na wenzake kwa mategemeo ya kuidhoofisha Chadema. Hii ni dhana potofu. Kilichopo ni kwamba, CCM ni sawa na Samaki aliyeoza. Hata ikitokea Freeman Mbowe akahamia CCM, Chadema itaendelea kuwa juu kwa sababu CCM imeuawa na Wanasiasa waliokikabidhi Chama hicho mikononi mwa Polisi. Kwa nini Waafrika hatujifunzi? Jeshi la Polisi la Makaburu lilikuwa na nguvu sana. Jiulizeni, kilichokuwa Chama Tawala cha Makaburu kiko wapi? Yale Magari ya kuwamwagia upupu wafuasi wa ANC ya Nelson Mandela yamehama Afrika Kusini baada ya kununuliwa na Jeshi la Polisi Tanzania, chini ya Chama cha Mapinduzi, CCM. Kwa nini CCM inashindwa kujifunza kutokana na Historia hii ya miaka ya karibuni?
 
Siasa za nchi hii zinaendeshwa kichumia tumbo watu wanatafuta fursa binafsi ili washibishe matumbo yao tu ndio maana wanabadilika badilika kama kinyonga wanaangalia wapi kwenye fursa kwa wakati huo na wao ndipo wanapoelekea na huko wanawakuta mazuzu wanawapigia makofi na kuwaita kwa majina mazuri na ya kishujaa.
 
[emoji28][emoji28][emoji28]yuko vzr kichwani ila imani tena haaminiki
Ni wapumbavu TU wanaomwita Dr .Slaa Msaliti.
Dr.Slaa hakuwa tayari kumweka madarakani Lowasa . Alikua ameshamtangaza kuwa ni Fisa aliyewaibia watanzania kupitia serikali ya CCM. Sasa angewezaje Tena kumweka madarakani Mwizi.

Ni sawa na kumwachia nyumba kibaka ili alinde.

Slaa alipima kati ya kumpigia kampeni Lowasa na kumsema vibaya JPM ambaye Kwa wakati ule ndiye Waziri Aliyekua anasifiwa na kila mtu Kwa uchapa kazi na kuwashughulikia makandarasi wababaishaji.
Aliona dhamira yake itamsuta.
Dr. Slaa mbali na siasa lakini ni mcha MUNGU. Anaamini katika haki,wema ,ukweli, ,uadilifu na msimamo wenye dhamira njema.

Dr. Slaa akirudia Chadema nitamuunga mkono asilimia mia moja
 
Kama ni kweli basi mbowe na wahuni wenzie wamekubali kuwa chadema ipo shimoni sasa wanatafuta mtu wa kukitoa chama shimoni .. wakumbuke huyo jamaa alikuwa mfuasi wa siasa za magufuli [emoji1787]tuliwaambia chadema siku nyingi kuwa kumpinga mzalendo ni kujichimbia shimo wenyewe wakabisha ....chadema washukuru kuwa sasa hivi hakuna chama chochote cha upinzani chenye kubeba legasi ya nyerere wala magufuli vinginevyo wangebaki mdomo wazi maana kifo cha hicho chama kinge vunja rekodi ya vifo vyote
Magufuli ana mazuri yake Kama uchapakazi.. lakini Ni kiongozi mbaya Sana..
Nyie ndugu zake magufuli muelewe ukweli huu..yaani kiongozi anaogopa upinzani Hadi kuwauwa Ni kiongozi mpuuzi Sana
Mbona Samia amewaacha wapinzani waongee lakini hakuna shida yoyote..
 
Siasa ni dynamic. Hakuna rafiki wa kudumu na adui wa kudumu

Kama CCM walimpokea tena Lowasa tena kwa mbwembwe, kwa nini Chadema wasimpokee tena katibu wao mkuu bora wa wakati wote?

Chadema ya leo ni mti ambao Mzee Slaa alishiriki kuupanda.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] msiwachezee watu akili aisee....
 
Na kukisaliti wakati kilipokuwa kinahitaji sana uwepo wake?

Kweli duniani maajabu hayakomi.
Dr. Slaa hakuisaliti CDM bali yeye alisalitiwa na viongozi wakuu wa CDM kina Mbowe. Sera ya CDM ilikuwa wazi kupinga ufisadi ulioongozwa na Lowassa. Ghafla ufisadi unaondolewa kwenye sera ya CDM na list of shame inafutwa kwenye website ya CDM. Hapo nani alisalitiwa?
 
Hakuna Chama kitakachoungia madarakani kikiwa na wanachama waliokiasisi peke yao.

Hata wakati wa wakaloni Kuna wazungu walikua wanapitia mlango wa nyuma kuunga mkono harakati za weusi kuondoa ukoloni.

Mfano wajerumani waliondokewa na Waingereza. Haki ikatengamaa kidogo. Wananchi wakapumua .

Waingereza nao wakaondolewa Kwa shinikizo la Amerika. Kuzifanya nchi ziwe huru Kwa ajili ya soko huru.

Vijana wa Chadema watambue kuwa hata Uhuru Kenyatta ni zao la KANU lakini aliibukia nje ya Chama hicho ambacho hakipo Tena. Hivi vyama ni lebel TU ya kumtambua mtu ndio maana tunataka hata Mgombea huru. Mtu Bora hata akiwa ndani ya ACT anaonekana TU, akija Chadema wampokee.

Tatizo ni Moja Kwa Sasa Chadema hakina dira maalumu.
Hatujui wanapambana kuitoa madarakani CCM ili iweje mana hata CCM Ikitoka madarakani bila kuwa na Kiongozi au mfumo utakaowahughulikia mafisadi Bado tutakua na wakati mgumu sana kimaendeleo.
Lazima pawe na unafuu wa MAISHA Kwa watu wa chini . Lakini pia ni lazima wanayopewa madaraka ya kuteuliwa wabanwe sana na kuwekewa SHERIA Kali ikiwezekana ya kunyongwa au kufilisiwa wanapoonekana kuwa wamekwapua Mali za umma au wamshiriki kufanya ufisadi.

Kuna Mahakimu na majaji ni lazima watahadharishwa kuhusu watu wanaohujumu uchumi. Mtu anaiba bilioni 20 halafu anapigwa faini Milioni 50 bila kuambiwa arudishe pesa alizoiba.Matokeo yake panakua ni mradi kati ya wasimamia shereria na wezi wa kubwa wa Mali za umma.
 
Hatimaye CDM wamesikiza ushauri,

Binafsi nimekuwa nikishaauri wazi umuhimu wa Slaa CDM,

Nashauri arudi nafasi ya Katibu mkuu wa chama, chama kitaimarika sana kimkakati na kisera kuepuka siasa za matusi ,ushabiki na kuvizia matukio.


Dr Slaa anaweza kuwajibu Kwa HOJA wazee wa CCM kama wassira na PINDA kuelekea kupata njia ya kuandika KATIBA mpya.

Ni kwema mbeleni, ni kwema mbeleni.

Mungu ibariki TANZANIA,

Mungu ibariki CDM.

Aamen
 
Tawireeeee!. Huyu Dr. Slaa si alisema hataki tena siasa za majukwaani huyu?
 
Back
Top Bottom