Dkt. Tulia: Ripoti ya CAG itajadiliwa kwenye Mkutano Novemba, 2023
Spika Tulia amesema Ripoti ya CAG itajadiliwa kwenye Mkutano wa mwezi November 2023

Huyo ni baada ya Kamati za Bunge kuwa zimeshakamilisha wajibu wake wa kisheria.

==========

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amesema ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2021/22 itajadiliwa kwenye mkutano ujao wa bunge, Novemba 2023, baada ya kamati za hesabu za Serikali kumaliza kazi zake.

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amesema Bunge halitachukua hoja zitakazochangiwa na mbunge sasa kuhusu ripoti ya CAG kwa sababu mkutano wa sasa wa bunge ni wa bajeti na si kujadili ripoti hiyo.

View attachment 2586406
Source: Swahili Times
Kama ni hivyo kwanini aliruhusu mjadala huo bungeni kama haukuwa wakati wake? Bunge la bajeti linajdili Mapato na matumizi ya Serikali. CAG report inaelezea matumizi Mabaya ya Serikali hivyo kwanini matumizi mabaya ya Serikali yasijumuishwe kwenye mjadala wa bajeti ili kuzuia yasijirudie?
 
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amesema Bunge halitachukua hoja zitakazochangiwa na mbunge sasa kuhusu ripoti ya CAG kwa sababu mkutano wa sasa wa bunge ni wa bajeti na si kujadili ripoti hiyo.

Source:
Sugu endelea kukusanya point 2025 tupa kule Mwakaleli ikafilieko mbali
 
Km hawataki kufata sheria basi wasilalamike sheria ikichukuliwa mkononi na wananchi....

Mafisadi wanajulikana na wanaishi mitaani na watu, serikali iwe sikivu tu imalize hii issue,

Kukaa kikao siku 3 kuna ugumu gani, yaani kuwawajibisha watu 15 kwa faida ya taifa na kuilinda amani imekua ngumu aisee.

Kweli mnataka kuvunja nyumba mlioijenga kwa mikono yenu wenyewe.

Si tupo tunaangalia
 
Ndio nikasema hivi, mnajadili bajeti kwenda kuibiwa?. Yani baadala msolve suala la wizi kwenye bajeti, nyie mnahangaika kupitisha bajeti ili ikaibiwe tena. Ni common reasoning tu, tuache mambo ya procedure tuangalie je ni haki kupitisha bajeti bila kushughulikia wizi?. In short bunge lipo kutetea serikali na mafisadi.

Kwani wakimaliza kikao cha bajeti ndio itakua mwisho wa bunge kwamba hakutakua na mijadala!?
 
Hiyo ni gia ya kukimbia uajibikaji. Hapo ikifika mwezi wa kumi na moja watadai mambo yote yameshashughulikiwa. Bunge la kijinga likiongozwa na spika kilaza na mjinga. Shenzi kabisa

Hakikisha unawasliana na mwakilishi wako wajadili yote unayoyataka kabla ya mwezi wa kumi
 
Yeye ndio muongo. Aseme ukweli analinda ufisadi wa mumewe usijadiliwe bungeni. DR James wa EWURA.

siiaijii ni mchonganishi sana. na ukiendelea kumsikiliza utapata vidonda vya moyo. wee mtu anasema reli imejengwa kwa gharama za juu kuliko wastani. haya ukimuuliza wastani huo umetoa wapii. anaanza kusema mimi najua. ukisema tupe comparable projects tujilinganishe, anaishia kusema, usinichimbe. 🤣 😂 😛

1681456074274.jpeg
 
Kwa Bunge hili la ccm kama litachukua hatua kwa wana ccm wenzao wezi wa fedha za umma niiteni mbwa na nimekaa pale 👉
 
Bungee mnabwabwaja sio la wananchi, ila mkwanja wa ruzuku ya kuendeshea chama chenu hamsusi, mnanya Kwa nguvu kama vile manila anavyonyakua boli. Mnavhekesha kweli.

Kwani hizo pesa zinatolewa na hilo bunge kibogoyo?
 
Huyu dada ni masalia ya mwenda zake. Hivi unaambiwa kuna mwizi yuko kwako, uta subiri akuibie au uta zuia wizi?
Huyu spika wa mchongo ameona jinsi Mh Rais alivyo chukizwa na hili jambo, yeye haoni kama ni tatizo. Ati hadi Nivember wezi waendelee kukaa ofisini ndipo bunge liwajadili. Hizi ni akili au matope?
Kwanini haoni udharura wa kujadili hili jambo mapema kwa dharura?
Au kwa vile ofisi yake nayo imo kwenye kulipa mabilioni kwa wabunge hewa?
Bunge la mchongo nao wana muunga mkono spika wa mchongo. Aibuuuuu.
 
Kwani hizo pesa zinatolewa na hilo bunge kibogoyo?
Bajeti ya serikali inapitishwa na nanii?? Sio Hilo binge unalolisimangaa?? Huku ukisahau ndiko linalopitusha bajeti ili na wewe chama chako kipate ruzuku
 
Bajeti ya serikali inapitishwa na nanii?? Sio Hilo binge unalolisimangaa?? Huku ukisahau ndiko linalopitusha bajeti ili na wewe chama chako kipate ruzuku

Hilo bunge ni rubber stamp tu, hakuna lolote wanaloweza kuzuia likipangwa na serikali. Hata hiyo kuwa bunge linatunga sheria ni porojo tu, sheria zote hupelekwa bungeni na serikali, na hilo bunge huishi kurusha tu mate na mwisho sheria hupita kama ilivyopelekwa na serikali, ama hata kuwa mbaya zaidi, lakini katika kuinufaisha serekali.
 
Ila linapitisha ruzuku ya chama chako
 
Ila linapitisha ruzuku ya chama chako
Narudia tena, hao ni rubber stamp, wanapitisha chochote cha serikali, na wala sio kuwa wanapitisha kwa hisani bali ni wajibu wao. Au ulitaka CDM ndio wakapitishe? Kama vipi ongea nao waambie wasipitishe tuone huo ubavu wao.
 
Kumbe umekubali niwajibu wao wakupitishie bajeti ya ruzuku ya chama chako ili upate fedha za kununulia bando la kuwatukana hapa mitandaoni.
 
Back
Top Bottom