Dkt. Tulia: Ripoti ya CAG itajadiliwa kwenye Mkutano Novemba, 2023
Bungee mnabwabwaja sio la wananchi, ila mkwanja wa ruzuku ya kuendeshea chama chenu hamsusi, mnanya Kwa nguvu kama vile manila anavyonyakua boli. Mnavhekesha kweli.

Acha kujitoa kwenye mada. Mambo ya ruzuku hata DP anapokea ni haki yao. Ila suala la bunge kulinda mafisadi halikubaliki.
 
Si mnabwabwaja eti nibunge la hovyo na wakati bungee hilohilo ndio linalopitusha bajeti ya ruzuku ya chama chenu. Ebu wanachadema pongezeni bungee hili ili lipitishe bajeti nzuri na nyie ruzuku iwe nzuriii zaidii

Ruzuku inatoka kwenye kodi ya kila mwanachi, hata wa upinzani wanalipa sio bunge. Issue ni kwamba bunge linaweza kupitisha azimio la kumpongeza rais wiki nzima lakini kujadili ripoti hatabkwa siku tatu wanarusha hadi mwisho wa mwaka. Stupid bunge.
 
tuache uongo hajaoiga marufuku ameelezea utaratibu ulivyo kwa mujibu wa kanuni za bunge

Utaratibu upi?. Bunge limejadili ushoga na kupitisha azimio la kumpongeza Rais, ila kutenga siku tatu kujadili wizi na kutoa maazimio imekuwa shida.
 
Ruzuku inatoka kwenye kodi ya kila mwanachi, hata wa upinzani wanalipa sio bunge. Issue ni kwamba bunge linaweza kupitisha azimio la kumpongeza rais wiki nzima lakini kujadili ripoti hatabkwa siku tatu wanarusha hadi mwisho wa mwaka. Stupid bunge.
Kwani Kodi ikikusanywa kutoka Kwa hao wananchi inaenda Moja Kwa Moja kwenye chama chenu, au inapitishwa kama bajeti ya makusanyo yote halafu bungee linasomewa na kulidhia na ndioo mgao ule na nyie mnapewaa?? Au nyie mnakusanya na kuwana wenyewee. Haaaaaa haaaaa. Unachekesha kweliii. Tena tuwaombee wabunge wa CCM Mungu awabariki Kwa KAZI nzuriii. Habari ya report ya CAG umeshaambiwa itajadiliwa lini, Sasa shida Iko wapiii
 
Unachekesha sana, bajeti inapitishwa na bunge ila pesa haitolewi na bunge , bali pesa inayoka kwa wananchi wenyewe na wahisani. Ndio maana nikakwambia ruzuku ni haki ya vyama maana pesa inatoka kwa raia sio serikali na ruzuku ni haki kikatiba sio hongo. Kwa hivyo bunge la vilaza wa ccm halitoi hata shilingi kumi lenyewe linapitisha bajeti na sio kutoa pesa.

Unajadili bajeti ambayo robo yake imeibiwa?. Mpaka waziri mkuu amezuia mikopo ya halmashauri isitolewe. Yani baadla mkae mshughulikie wizi kwenye bajeti, mnakimbilia kupitisha bajeti ili wezi waibe vizuri.
 
Kwahiyo mnakusanya wenywe na kujigawia wenyewee na hao raia wenuuu
 
Nini lengo la audit (duniani)?

Mashirika ya serikali au binafsi yenye shareholders; yanaendeshwa na managements ambazo ni wasimamizi tu wa mali za wengine. Kwa serikali ni mali ya watanzania wote au kodi zao ndio zinatumika kugharamia serikali.

Hizo managements zinaweza kuwa na maslahi yao. Mfano ili aonekane bora anaweza ongopa shirika lina mapato mazuri ukienda chunguza unakuta kuna potential income hewa, hayo madeni wadaiwa awajulikani na wala hizo nyaraka za madeni hazipo ni uongo tu ili waonekane wana income nzuri kwenye vitabu vyao.

Managers pia wanaweza kuwa wabadhirifu, wana matumizi ya ovyo, ufujaji wa hela na mambo mengine ya ovyo.

Jukumu la auditor ni kwenda kuchunguza kama wanachosema ni kweli hakina uongo kwa maslahi yao managers na hela inatumika vizuri.

Auditor anamfanyia nani kazi (agency theory).

Auditor anawafanyia kazi wananchi wote ndio wamiliki wa mali zinazosimamiwa na serikali, hela za kodi, biashara na taasisi zake. Na wananchi wanawakilishwa na wabunge ndio sababu ya report kuwakilishwa kwa wabunge, waangalie kwa niaba yetu.

Na kwa utaratibu waliojiwekea huko bungeni kwenye kupitia hiyo report na kuiwajibisha serikali sio kwa maslahi ya watanzania isipokuwa matumbo yao. Kwanza mchakato wao unawapa muda majizi kujipanga kwa kutengeneza uongo na watu wenyewe wanao wahoji sio wataalamu.

Hizi ndio sababu wananchi tunatakiwa kumsikiliza CAG kuliko wabunge kwa sababu ata sisi hizo report tunazo; maamuzi pekee tuliyonayo ni kuwatoa wabunge kama Kibabaj wanaotetea mijizi isijadiliwe haraka na hatua zichukuliwe.

Kazi ya audit inafanyikaje?

Kazi za auditing na taratibu zake aifanywi kwa sheria za nchi tu pekee, bali zinafuata pia miongozo ya kimataifa zinazotolewa na IAASB taasisi inayotengeneza regulations (International Standards on Audit, “ISA”).

ISA 200 inatoa maelezo ya nini auditor anachotakiwa kufanya kabla ya kuanza kazi, nini chakuchunguza na decision process ya kutoa opinion.

Kwa upande wa sheria za nchi taasisi za serikali 100% zinatakiwa kutengeneza statements zao kupitia IPSAS frameworks na zenye ubia IFRS (tofauti sio kubwa sana), However kwenye accounting system wote wanatakiwa kuandaa vitabu kwa kufuata ‘International Accounting Standard’ (IAS). Na haya mambo wahasibu wote wapo trained kuweza kufanya.

Kwa ivyo CAG yeye anachokagua ni hizo taratibu kama zinafuatwa kwenye shughuli za kila siku na kama hizo system ni imara ndani ya shirika. Kazi zingine value for money and so forth.

Report ya CAG

Report ya CAG inaelezea mapungufu ya kimfumo, sehemu ambazo kuna ubadhirifu na kadhalika aitoki kabla ya kuwapa muda wahusika kujibu hoja kwanza. Kwa hivyo inapotoka ni final, uhitaji tena mmbunge kwenda kuhoji ni kupoteza muda, hapo unataka raisi au wahusika kuchukua hatua kwa majizi.

Wabunge ni kuisimamia serikali itimize wajibu kwa kuchukua hatua sahihi, kwenda na wao kujadili ni kupoteza muda na kuwapa watu nafasi ya kutunga uongo ambao si ajabu CAG asiuangalie tena mwaka unaofuata.

Jukumu la wenye nchi

Ni kuhakikisha watu kama hakina Betina, Mhagama na Kibabaj tunawatoa uchaguzi ujao wapo kwa sababu ya kutetea majizi sio kulinda maslahi ya watanzania walio wapeleka hapo. Na kutaka kuona huu mfumo wa kupokea na kujadili report unabadilika kwa sasa upo kwa faida ya majizi sio wenye mali.

Udhaifu wa report za CAG

Ameanza kuingiza ushabiki wa siasa na kutoa maoni without ‘sufficient appropriate evidence’ huku ni kujiondolea credibility wakati kazi iliyobaki asilimia kubwa ni ya kitaalamu ukisoma sababu zake. Huyu Kichere nae ajitafakari kama anatosha kwa kuanza kuingiza majungu ya siasa.
 
Point yangu ni kwamba , unajadilije bajeti wakati robo ya bajeti iliyopita imepigwa?. Unajadili bajeti kwa ajili ya kuliwa au kufanya kazi?. Wangeanza kwa kujadili ripoti hata kwa wiki moja halafu , halafu watoe maazimio kama ya richmond.
Mkuu Economist nchi inaendeshwa kwa mujibu wa sheria kwahiyo ni takwa la kikatiba wao kujadili bajeti kwa sasa. Hapo kwenye kuliwa au kutoliwa taratibu zake zinajulikana. Pia bunge lina nguvu kubwa endapo litatumia nafasi yake vizuri. Kuacha kujadili bajeti na kuziungumzia ushoga ni upuuzi wa hali ya juu na kujishushia heshima kama bunge. Hoja yako yenye mashiko ni hii ishu ya ripoti ya CAG kujadiiwa Novemba. Mimi binafsi naona kama ni kutoa mwanya kwa watuhumiwa kujipanga.
 
Kanuni zinamruhusu Spika kupangia ratiba taarifa ya CAG baada ya kuwa imeshakabidhiwa Bungeni?
Huu uzwazwa una malengo gani hasa?
Nadhani sheria inaruhusu kutoa siku sio chini ya 60 hivi Ili serikali itoe majibu na PAC kuja na mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa. In fact huko nyuma ripoti ya CAG ilikua inachambuliwa bunge la January yaani miezi zaidi ya 6 tokea iletwe meza ya Spika!!

So pengine kanuni zilikosewa kutungwa ila Kwa hili Spika yupo sawa kisheria maana CCM ndio walizipitisha ili kutow nafasi kwa PAC kuhoji Kila mshtakiwa.
 
Kwa mtaaamo wangu ni kwamba
Kama CAG alitoa muda wa kureconcile hesabu na wahusika ni wazi ripoti yake ipo clear. Lakini kusema kuwa wajiandae kujibu, sielewi wanajibu kitu gani walichoahindwa kumjibu CAG?
Inawezekana kosa la maadili ya uongozi likawa limetendeka kwa walioshindwa kujibu hadi waje kujitetea mbele ya kamafi ya PAC.

Anyways subira si haba
 
Mkuu Economist nchi inaendeshwa kwa mujibu wa sheria kwahiyo ni takwa la kikatiba wao kujadili bajeti kwa sasa. Hapo kwenye kuliwa au kutoliwa taratibu zake zinajulikana. Pia bunge lina nguvu kubwa endapo litatumia nafasi yake vizuri. Kuacha kujadili bajeti na kuziungumzia ushoga ni upuuzi wa hali ya juu na kujishushia heshima kama bunge. Hoja yako yenye mashiko ni hii ishu ya ripoti ya CAG kujadiiwa Novemba. Mimi binafsi naona kama ni kutoa mwanya kwa watuhumiwa kujipanga.
Sawa mkuu nimekuelewa.
 
Back
Top Bottom