Dkt. Tulia: Ripoti ya CAG itajadiliwa kwenye Mkutano Novemba, 2023
Lengo gani ?. La kuwalinda mafisadi?. Huyo anamlinda mme wake, ambaye ana tuhuma za ufisadi.

Kila jambo na muda wake kwa mpango wake
Kama vile wewe usivyoweza kuvaa suruali mabegani na shirt mapajani umwache Tulia asimamie kikao cha bajeti ikifikia wasaa wa kujadili report itajadiliwa
 
HUWEZI endesha kikao cha bunge bila utaratibu
Muda wa BAJETI wakianza kuchambua ripoti ya CAG hiyo bajeti itajadiliwa lini!?
Unaongea km umetoka kunya ubongo,ko unavoambiwa bunge ni dhaifu ambacho unakataa ni nini?!!

Unawekaje utaratibu wa kupitisha bajeti mpya kabla ya kuhakiki matumiz ya bajeti iliyopita na kuwawajibisha waliokwamisha miradi ya maendeleo ama kuitia hasara taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu huu taratibu na kanuni za bunge za kujadili hii report ya CAG ni mfumo unao toa mwanya wa wahusika wa ubadilifu kujipanga kwa kuhalalisha ufisadi uliojitokeza. Nadhani muda umefika wa kuwa na utaratibu ambao utaleta tija na mafisadi kuuogopa.
Tulishangilia wapinzani kuondolewa bungeni sasa tunalia kilio cha mbwa koko.

Tumeumizwa sana.
Wahuni si watu
 
Unaongea km umetoka kunya ubongo,ko unavoambiwa bunge ni dhaifu ambacho unakataa ni nini?!!

Unawekaje utaratibu wa kupitisha bajeti mpya kabla ya kuhakiki matumiz ya bajeti iliyopita na kuwawajibisha waliokwamisha miradi ya maendeleo ama kuitia hasara taifa

Sent using Jamii Forums mobile app

Na hicho kinyesi nilichokinya kinaitwa Son Of Andrew
 
HUWEZI endesha kikao cha bunge bila utaratibu
Muda wa BAJETI wakianza kuchambua ripoti ya CAG hiyo bajeti itajadiliwa lini!?
Unajadili bajeti gani isiyoakisi utekelezaji wa iliyopita?

Huu utetezi wako ni kwa ssbabu ya upofu na mahaba kwa chama tawala
 
Spika Tulia amesema Ripoti ya CAG itajadiliwa kwenye Mkutano wa mwezi November 2023

Huyo ni baada ya Kamati za Bunge kuwa zimeshakamilisha wajibu wake wa kisheria.

==========

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amesema ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2021/22 itajadiliwa kwenye mkutano ujao wa bunge, Novemba 2023, baada ya kamati za hesabu za Serikali kumaliza kazi zake.

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amesema Bunge halitachukua hoja zitakazochangiwa na mbunge sasa kuhusu ripoti ya CAG kwa sababu mkutano wa sasa wa bunge ni wa bajeti na si kujadili ripoti hiyo.

View attachment 2586406
Source: Swahili Times
SAWA tunaelewa Kuna mbinu chafu za kuzika hoja za ulaji! Rais aliomba siku 21 makatibu Wakuu watoe majawabu na Kwa ansadi ya Bunge Naibu wako Zungu alikiri Hilo linafanyika ndani ya siku hizo.
Kuna haja gani kuja kujadili uozo ulio wazi kabisa Mwezi November hata walizokula hamtapata hata Senti nyeupee.
Kweli Tanzania nchi ngumu.
 
Tulishangilia wapinzani kuondolewa bungeni sasa tunalia kilio cha mbwa koko.

Tumeumizwa sana.
Wahuni si watu
Mkuu nadhani ingependeza sana kama CAG akimaliza ukaguzi wake iwepo Taasisi ya kitaamu ambayo itashughulia KAGUZI HIZO. Aidha ni vema kabla ya ukaguzi unao fuata ni vyema Wananchi waka elezwa yatokanayo na utekelezaji wa ukaguzi uliopita. Huu utaratibu wa ukaguzi wa kila mwaka na Wananchi hawapati mrejesho wa utekelezaji wake hauna afya kwa CAG na Watanzania kwa ujumla wao.
 
Mkuu nadhani ingependeza sana kama CAG akimaliza ukaguzi wake iwepo Taasisi ya kitaamu ambayo itashughulia KAGUZI HIZO. Aidha ni vema kabla ya ukaguzi unao fuata ni vyema Wananchi waka elezwa yatokanayo na utekelezaji wa ukaguzi uliopita. Huu utaratibu wa ukaguzi wa kila mwaka na Wananchi hawapati mrejesho wa utekelezaji wake hauna afya kwa CAG na Watanzania kwa ujumla wao.
Hoja makini ssna
Lakini usidhani hili suala kuna mtawsla atakubali.

Yaani polisi waibe kisha wsonekane na issues kwenye ukaguzi kisha utekelezwaji wa hatua dhidi ya wahusika ufanyike?

Shida ni kwamba dola haikubali haya maoni yako.

Tubadilishe mkoloni tumuweke mtu mpya na chama kipya pale magogoni kisha haya yote yatafanyika
 
Spika Tulia anapaswa kuadhibiwa kwa kutokuona umuhimu wa kujidali ripoti hii hata kwa dharura.
Naelewa ilipaswa kamati za bunge ziipitie lkn kutoa mwanya huu mafisadi watapoteza ushahidi.

Wana Mbeya watusaidie kumwadhibu 2025
Huyo anadhani wanambea ni wajinga, labda magu afufuke
 
Nimesikitika sana nilipomuona Mhe. Spika akitoa taarifa kwa Wabunge kuwa taarifa ya CAG isijadiliwe katika kikao kinachoendelea sasa huko Dodoma.

Najiuliza wenye hela ni sisi wananchi kwa nini taarifa hii muhimu isiendelee kujadiliwa Bungeni?. Au Serikali inaendelea kuaibika kutokana na taarifa hiyo?

Jana Mhe. Mpina alisema kuwa ukijumlisha upotevu wote wa fedha za umma ni Trillioni 33. Hili ni jambo la kusikitisha sana. Kuanzia taasisi kabisa ya juu mpaka Mtendaji wa kijiji wanatakiwa wajiuzulu mara moja.
 
Tuliiii Hana shida,

Mwenye shida ni KITI Cha Supika.

Akisimama ni mwingine, na akikalia KITI ni mwingine.

Wakishika vitabu vya IMANI, wanaapa Kwa Mungu aliyeumba Tanzania, lakini wakikalia viti, wanamtumikia muungu mwingine wa chini, asiyetaka kuona maskini na wafungwa wanaafunguliwa minyororo Yao.

Tusubiri tetemeko lipite hapo na pale kuvitikisa viti vyote vya enzi Ili vitii SHERIA ya Mungu yule aliyekuja kuongea na Adamu Kila jioni katika Bustani ya EDEN.

Siku inakuja ambayo watakaoshika vitabu na kuapa Kwa Mungu, wakikengeuka na kutenda vyinginevyo, waliwe na CHANGO.

Aamen.
 
Siku kadhaa baada ya ripoti ya CAG kutoka ,kamati kuu ya CCM iliketi na moja ya maazimio yake ni kuhahakikisha waliotajwa wanachukuliwa hatua kali haraka iwezekanavyo.

Kama spika wa bunge amesema ripoti atajadiliwa mwezi novemba ina maana gani katika utelezaji wa azimio la Kamati kuu ya CCM? Je, kazi za bunge kwenye utekelezaji wa ripoti ya CAG ni ipi?

Jambo la pili, naona kuna vita inaendelea na hili ni kupitia kauli za Spika. Kauli ya kwanza ' Naiagiza serikali ifanyie maboresho....'. Je, kikatiba Spika anayo mamlaka ya kuiagiza Serikali? Kama kazi ya bunge ni kuijadili miswada (bill) na kuifanya sheria, je bunge lina mamlaka ya kuiagiza Serikali ?

Naiona vita Kali sana katikati ya haya
 
Nimesikitika sana nilipomuona Mhe. Spika akitoa taarifa kwa Wabunge kuwa taarifa ya CAG isijadiliwe katika kikao kinachoendelea sasa huko Dodoma. Najiuliza wenye hela ni sisi wananchi kwa nini taarifa hii muhimu isiendelee kujadiliwa Bungeni?. Au Serikali inaendelea kuaibika kutokana na taarifa hiyo?. Jana Mhe. Mpina alisema kuwa ukijumlisha upotevu wote wa fedha za umma ni Trillioni 33. Hili ni jambo la kusikitisha sana. Kuanzia taasisi kabisa ya juu mpaka Mtendaji wa kijiji wanatakiwa wajiuzulu mara moja.

Hilo bunge sio la wananchi, hivyo hawaoni hatari kutokujadili wizi wa fedha zetu. Tusiopoandamana na kuhakikisha hayo majizi ya kura hayaingii humo bungeni, wataendelea kutuona mafala tu.
 
Back
Top Bottom