Binafsi nakereheka mno na hii mbinu waliyojiwekea ya kuijadili ripoti ndani ya kamati ya pac ambayo nayo haitakuwa na tija Bali muendelezo wa business as usual!
Nashauri wabunge wanaojitambua na wenye angalau kachembe ka uzalendo kalikobakia wapeleke hoja mahsusi bungeni ya kuomba bunge liishinikize serikali ipeleke mswada wa Sheria bungeni wa kumpa mamlaka ya kisheria ya kushitaki na kuendesha kesi kwa wake wanaokutwa na makosa ya matumizi mabaya ya fedha za umma.
Tunayo mahakama ya uhujumu uchumi hivyo sioni sababu ya takukuru kupewa uwezo wa kushitaki na kumnyima cag uwezo huo. Wote wapewe uwezo sawa wa kushitaki na kuendesha kesi za uhujumu uchumi na ufisadi. Najua walafi watatumia nguvu kubwa lakini serikali izibe masikio na kufunga macho kumwezesha cag kushitaki moja kwa moja ili nchi ipone.