fimboyaasali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 8,617
- 8,244
tuache uongo hajaoiga marufuku ameelezea utaratibu ulivyo kwa mujibu wa kanuni za bungeNimesikitika sana nilipomuona Mhe. Spika akitoa taarifa kwa Wabunge kuwa taarifa ya CAG isijadiliwe katika kikao kinachoendelea sasa huko Dodoma. Najiuliza wenye hela ni sisi wananchi kwa nini taarifa hii muhimu isiendelee kujadiliwa Bungeni?. Au Serikali inaendelea kuaibika kutokana na taarifa hiyo?. Jana Mhe. Mpina alisema kuwa ukijumlisha upotevu wote wa fedha za umma ni Trillioni 33. Hili ni jambo la kusikitisha sana. Kuanzia taasisi kabisa ya juu mpaka Mtendaji wa kijiji wanatakiwa wajiuzulu mara moja.
Siku nyingine usiandike usichokuwa na uelewa nacho ... Wkt mwingine mnalazimisha mjibiwe kwa kufokewa ndo muelewe...Wewe mwelevu dadafua tukusikie. Kufoka fika na matusii ni dalili ya incompetence. Jibu swalii.
Sugu atapata hoja ya kumtoa huyu mtetea ufisadiSpika Tulia anapaswa kuadhibiwa kwa kutokuona umuhimu wa kujidali ripoti hii hata kwa dharura.
Naelewa ilipaswa kamati za bunge ziipitie lkn kutoa mwanya huu mafisadi watapoteza ushahidi.
Wana Mbeya watusaidie kumwadhibu 2025
HUWEZI endesha kikao cha bunge bila utaratibu
Muda wa BAJETI wakianza kuchambua ripoti ya CAG hiyo bajeti itajadiliwa lini!?
Kila jambo na muda wake kwa mpango wake
Kama vile wewe usivyoweza kuvaa suruali mabegani na shirt mapajani umwache Tulia asimamie kikao cha bajeti ikifikia wasaa wa kujadili report itajadiliwa
SAWA tunaelewa Kuna mbinu chafu za kuzika hoja za ulaji! Rais aliomba siku 21 makatibu Wakuu watoe majawabu na Kwa ansadi ya Bunge Naibu wako Zungu alikiri Hilo linafanyika ndani ya siku hizo.
Kuna haja gani kuja kujadili uozo ulio wazi kabisa Mwezi November hata walizokula hamtapata hata Senti nyeupee.
Kweli Tanzania nchi ngumu.
Mkutano wa 11 (huu unaoendelea sasa) wa bunge ni mkutano wa bajeti.
Basi endeleeni kupiga kelele, mnajitekenya wenyewe kwa kukosa maarifa.
Hajapiga marufuku!
Hilo bunge sio la wananchi, hivyo hawaoni hatari kutokujadili wizi wa fedha zetu. Tusiopoandamana na kuhakikisha hayo majizi ya kura hayaingii humo bungeni, wataendelea kutuona mafala tu.
Ukitazama kwa jicho la mwewe utagundua jinsi gani rais samia yuko na maadui lukuki bungeni kuliko hata mitaani. Yani mwigulu anafanya ubadhirifu makusudi kisha anamsakizia Raisi kwamba anajua huo ujinga wake. Leo Rais Samia anawataka wezi washughulikiwe mapema ili isimuondolee sura ya amiri jeshi anatokea mtu amekonda makwapa kama kona za kinanda na mataya kama kufuli za magodown ya dangote anamrudisha nyuma na kumchafua mama kwa wananchi wake alioapa kuwatumikia kwa kuzuia mjadala. Hii sio sawa
Sababu gani?. Unajadili bajeti lakini pesa zilizoibwa kwenye bajeti iliyopita msubiri mwezi wa kumi na moja. Kwa kifupi bunge linapitisha bajeti bila kuzingatia wizi wa kwenye bajeti hiyo na kuwapitishia bajeti mafisadi wakaipige vizuri.Mimi Nina imani kubwa sana na spika, kama kweli amekataza kuna sababu ya umuhimu
Wananchi gani hao?
Mkuu koryo1952 , kiukweli uelewa wa baadhi yetu ni mgogoro, Spika hajapiga marufuku taarifa ya CAG kujadiliwa Bungeni bali amesema mjadala rasmi kuijadili ni kikao cha November, ila mbunge yuko huru kutoa maoni yake yoyote kuhusu ripoti ya CAG ila asiiulize serikali kutoa majibu yoyote.
Amesema wameisogeza ili kutoa nafasi kwa wahusika kupewa haki ya kusikikizwa na kamati husika kisha ndipo Bunge litajadili na kutoa Azimio la Bunge kupelekwa serikalini kwa utekelezaji.
P