Nini lengo la audit (duniani)?
Mashirika ya serikali au binafsi yenye shareholders; yanaendeshwa na managements ambazo ni wasimamizi tu wa mali za wengine. Kwa serikali ni mali ya watanzania wote au kodi zao ndio zinatumika kugharamia serikali.
Hizo managements zinaweza kuwa na maslahi yao. Mfano ili aonekane bora anaweza ongopa shirika lina mapato mazuri ukienda chunguza unakuta kuna potential income hewa, hayo madeni wadaiwa awajulikani na wala hizo nyaraka za madeni hazipo ni uongo tu ili waonekane wana income nzuri kwenye vitabu vyao.
Managers pia wanaweza kuwa wabadhirifu, wana matumizi ya ovyo, ufujaji wa hela na mambo mengine ya ovyo.
Jukumu la auditor ni kwenda kuchunguza kama wanachosema ni kweli hakina uongo kwa maslahi yao managers na hela inatumika vizuri.
Auditor anamfanyia nani kazi (agency theory).
Auditor anawafanyia kazi wananchi wote ndio wamiliki wa mali zinazosimamiwa na serikali, hela za kodi, biashara na taasisi zake. Na wananchi wanawakilishwa na wabunge ndio sababu ya report kuwakilishwa kwa wabunge, waangalie kwa niaba yetu.
Na kwa utaratibu waliojiwekea huko bungeni kwenye kupitia hiyo report na kuiwajibisha serikali sio kwa maslahi ya watanzania isipokuwa matumbo yao. Kwanza mchakato wao unawapa muda majizi kujipanga kwa kutengeneza uongo na watu wenyewe wanao wahoji sio wataalamu.
Hizi ndio sababu wananchi tunatakiwa kumsikiliza CAG kuliko wabunge kwa sababu ata sisi hizo report tunazo; maamuzi pekee tuliyonayo ni kuwatoa wabunge kama Kibabaj wanaotetea mijizi isijadiliwe haraka na hatua zichukuliwe.
Kazi ya audit inafanyikaje?
Kazi za auditing na taratibu zake aifanywi kwa sheria za nchi tu pekee, bali zinafuata pia miongozo ya kimataifa zinazotolewa na IAASB taasisi inayotengeneza regulations (International Standards on Audit, “ISA”).
ISA 200 inatoa maelezo ya nini auditor anachotakiwa kufanya kabla ya kuanza kazi, nini chakuchunguza na decision process ya kutoa opinion.
Kwa upande wa sheria za nchi taasisi za serikali 100% zinatakiwa kutengeneza statements zao kupitia IPSAS frameworks na zenye ubia IFRS (tofauti sio kubwa sana), However kwenye accounting system wote wanatakiwa kuandaa vitabu kwa kufuata ‘International Accounting Standard’ (IAS). Na haya mambo wahasibu wote wapo trained kuweza kufanya.
Kwa ivyo CAG yeye anachokagua ni hizo taratibu kama zinafuatwa kwenye shughuli za kila siku na kama hizo system ni imara ndani ya shirika. Kazi zingine value for money and so forth.
Report ya CAG
Report ya CAG inaelezea mapungufu ya kimfumo, sehemu ambazo kuna ubadhirifu na kadhalika aitoki kabla ya kuwapa muda wahusika kujibu hoja kwanza. Kwa hivyo inapotoka ni final, uhitaji tena mmbunge kwenda kuhoji ni kupoteza muda, hapo unataka raisi au wahusika kuchukua hatua kwa majizi.
Wabunge ni kuisimamia serikali itimize wajibu kwa kuchukua hatua sahihi, kwenda na wao kujadili ni kupoteza muda na kuwapa watu nafasi ya kutunga uongo ambao si ajabu CAG asiuangalie tena mwaka unaofuata.
Jukumu la wenye nchi
Ni kuhakikisha watu kama hakina Betina, Mhagama na Kibabaj tunawatoa uchaguzi ujao wapo kwa sababu ya kutetea majizi sio kulinda maslahi ya watanzania walio wapeleka hapo. Na kutaka kuona huu mfumo wa kupokea na kujadili report unabadilika kwa sasa upo kwa faida ya majizi sio wenye mali.
Udhaifu wa report za CAG
Ameanza kuingiza ushabiki wa siasa na kutoa maoni without ‘sufficient appropriate evidence’ huku ni kujiondolea credibility wakati kazi iliyobaki asilimia kubwa ni ya kitaalamu ukisoma sababu zake. Huyu Kichere nae ajitafakari kama anatosha kwa kuanza kuingiza majungu ya siasa.