Dkt. Tulia: Ripoti ya CAG itajadiliwa kwenye Mkutano Novemba, 2023
Yaani ndugu yangu, Kwa mwenendo huu mie naona, hilo bunge la Chama kimoja Tz ,litaendelea kulinda maslhi Yao tu, hadi wananchi watapozinduka kwenye usingizi mzito, huku spika wa bunge naye akitumia hadaa za kisheria, kuendelea kuwaruhusu watuhumiwa wa CAG, wa ubadhilifu kuendelea kula bata hadi baada ya November '23, ..... Naona Tz kweli maigizo hayawezi kuisha aiseee.. .tukubali yaishe....
Wakati huo mafisadi yaliyokubuhu yatakuwa yamepoteza vielelezo na ushahidi!
 
Kumbe na nyie mnanjaa Kali Sanaa. Tulieni CCM itawalishaa msihofuu

CCM itamlisha nani wakati yenyewe inategemea wizi wa kura ili iendelee kula hela za wananchi? Au unadhani kodi za wananchi ni fedha zinazotokana na miradi ya CCM?
 
Imewafuga Wala ruzuku
Watamfuga nani wakati hata majengo ya urithi wa enzi za chama kimoja wameshindwa kupiga rangi? CCM ingekuwa na uwezo huo viwanja vya mpira walivyopora visingechoka kihivyo. Acheni mazoea na hela za wanaume tafadhali.
 
Ruzuku unakulaa au hulii
 
Tulisema hapa na tunaendelea kusema kila siku. Tuna bunge la ovyo kabisa kuwahi kutokea, ovyo kabisa.
Kweli kabisa. Hata manyani yaliponyimwa mbaazi yakasema mbaazi zeneyewe mbichi. Kiboko yao tundulissu kapata mbunge mmoja tu huku alikuta wabunge 107 wa Luwassa na Dr Slaa. Akawapoteza wote kwa matusi akiwamo boss mbowe na Halima.
 
Kanuni zinamruhusu Spika kupangia ratiba taarifa ya CAG baada ya kuwa imeshakabidhiwa Bungeni?
Huu uzwazwa una malengo gani hasa?
Ndiyo maana tunahitaji katiba mpya. Kwa riport hii ya CAG bunge lilipaswa kuagirisha shuguli zingine japonkwa siku 3 kujadili report na kuielekeza serikali kuwawajibisha wapigaji.
 
Ndiyo maana tunahitaji katiba mpya. Kwa riport hii ya CAG bunge lilipaswa kuagirisha shuguli zingine japonkwa siku 3 kujadili report na kuielekeza serikali kuwawajibisha wapigaji.
Bunge lipi unalisema?

Hakuna Bunge siriaz hapo. Tunapigwa hadaa za kufa mtu kwa gharama za kodi zetu
 
Kwani mlishakubali kuwa mligaragazwa kihalali?
2020 hakukuwa na uchaguzi bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Kwani hao wanaoiba fedha za umma ndio waliona uchaguzi ulikuwa wa maana?
 
Simulijikanyaga eti hamtachukua mkwanja wa ruzuku kisa eti hamkubali matokeo? Sasa ndio mumukubali kwamba mligaragazwa kweupee
Jitahidi kuandika kwa ufasaha boss. Unaweza pia kurudi shule maana sasa hivi elimu ni bure.
 
Back
Top Bottom