Dodoma: Adaiwa Kumuua Mkewe kwa kumchoma kitu chenye ncha kali shingoni

Ameeen
 
Familia na malezi ndipo palipo na shida hapo..!!
 
Daaaaah si jambo la kufrahia kuna haja ya kama taifa kutafakari kwa kina na kuchukua hatua za kuzuia haya mambo kwasababu hawa wanaouawa inawezekana leo hawatuhusu lakini kuna siku moja watakua Dada zetu, Shangazi zetu, Mama zetu, wadogo zete na hata ndugu zetu. Narudia inaweza isiwe leo ama kesho ama keshokutwa lakini ipo tu siku. Bila kujali mtu kafanya kosa gani lakini kutoa adhabu ya kifo kwa mtu mwingine ni mbali sana huko kama hayawezekani bora watu waachane tu.
 
Dunia ya sasa hivi watu wanajiingiza kwenye ndoa kwa ajili ya kunufaika, Ndoa za mkataba ndiyo suluhusho wa mauaji ya wanandoa, Maana kama kuna sintofaham yoyote katika kipindi cha mkataba, basi huwo mkataba usitishwe Mara moja.
 
Kuna mmoja ka comment huko juu et here we go anajiona mwamba kumbe jinga la mwisho na mihemko ipo juu kuliko ufanisi wa akili

Sikujua kama watu wengi wana tatizo la afya ya akili
JF machizi tunao wengi na ndo hao wa mtaani wauaji..!!

Hapa jukwaani ukitaka upendwe na wanaume usiwakosoe, wakikutukana unyamaze..!! Hapo utasifiwa mpole na una haiba ya kike.

Jaribu kumjibu uone mtiti wake..
Atakutafutia parody ili aje akutukane, akushushie heshima. Hapo ni mtandaoni.

Sasa mijitu kama hiyo uraiani inakuua kwa kukosa akili na jinsi ya kuzuia mihemko yao.

Ndio ujue vichaa na wenye changamoto ya afya ya akili ni wengi.
 
Kupitia haya matukio, wapo wanaume wanaofurahia lakini wapo wanaume wanaondelea kujenga uwoga wa kuingia kwa ndoa. Kitakachotokea mbele huko ni waume kuoa waume wenzao. Ujasiri wa kiume unatoweka taratibu.
 
Wanawake wana maudhi sana. Ukimkuta mwenye maudhi mengi ndiyo anakunyima raha kabisa, kila saa unamuwazia mabaya tu.
 
Ni zamu ya wanawake kuishi na wanaume kwa akili,mtaisha!!
Cjajua akina Ke huwa wanawaza nini na kivipi - mitongozo miwili au mitatu tayari anasema ndiyo-basi haya(in Gwajima's voice). Haangalii mengine. Wanadhani labda kuishi ni sawa na kula tunda kimasihara. Wanasahau "Familiarity breeds contempt". Penzi linachuja kadri muda unavyokwenda.
Kadri haya matukio yanavyopewa muda mwingi kwenye social media ndiyo yatazidi kuibuka kila siku.
Sidhani. Hii social media inasaidia sana Awareness creation kwa akina Ke. Wajue kuzitambua na kuzisoma alama za nyakati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…