Droo ya Play-off, Yanga yapangwa na Club Africain ya Tunisia

Droo ya Play-off, Yanga yapangwa na Club Africain ya Tunisia

Pia niwakumbushe kuwa wachezaji wa Club Africain walipewa lawama nyingi kutoka kwa mashabiki kwa kosa la kupata ushindi mwembamba wa goli 7-0

Naskia baada ya sintofahamu hiyo walitoa ahadi kwa mashabiki kuwa watarekebisha makosa yao kwenye mechi inayofuata

Tutegemee jackpot
 
kwa anaejua,natafuta Engrish corse ya kiarabu nataka nichukue uraia wa Tunusia haraka sana.
 
Yanga wamepangiwa hatua ya mtoano dhidi ya Club Africain ya waarabu. Hawa ndio wale waliowapiga Kipanga FC 7-0 huko shirikisho.

Club Africain ni timu Kongwe na walishatwaa ubingwa wa Klabu bingwa Afika mwaka 1991. Hawa jamaa wanamiliki uwanja wao unaobeba watazamaji 60,000/= kama kwa mkapa tu. Wapinzani wao wakubwa na wanaocheza nao derby ni ES Tunis na pia wana upinzani wa jadi na Etoel du sahel na MC Alger ya Algeria.

Club Africain ni timu inayocheza kwa mbinu za hali ya juu wakiwa ugenini huwa wanacheza kwa tahadhari ya kutopoteza mchezo na wakiwa nyumbani huwa wanaachia majini yao yote na ndio kilichomkuta kipanga.

Yanga wasichukulie kuwa hawa ni wepesi kwa kuwa kwenye ligi yao walimaliza nafasi ya 4. Tunajua wenzetu uwekezaji wao ulivyo hata timu za chini zina uwezo mkubwa.

Tarehe 2 November itakuwa kipimo kingine kwa Yanga ambao kwa hapa ndio underdog na wataanzia tena nyumbani kama kawaida.
View attachment 2391040
Yanga rudi nyumbani kumenoga
 
Back
Top Bottom