Alikuwa na nafasi moja nzuri sana ya kujijenga kisiasa na kupata heshima kubwa ya kukumbukwa kama kiongozi aliyeibadili Tanzania kutoka kwenye janga.
Miaka minne hii, angejikita katika kufanya mabadiliko ya kisiasa nchini, akasimamia haki, utawala wa sheria.
Angewanyima wapinzani ajenda ya kumsumbua, na 2025 asingepata upinzani wa kumtisha.
Haya yote kayatupilia mbali kwa muda mfupi sana. Lililobaki kwake sasa ni kuzidi kukandamiza zaidi ili yeye na chama chake waendelee kuwepo madarakani.
Hii ni kazi ngumu. Hakuna ajuae Tanzania itaendelea kuvumilia kuwa chini ya udikteta.