PostGE2025 Elezea kinagaubaga jinsi mabeberu wanavyohujumu nchi yetu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Magari ya kifahari wanayotumia sehemu kubwa ubunifu umefanyika huko wanakoita kwa mabeberu.
 
Mfumo gani ambao si wa kibeberu unadhani unafaa kutumika kuendeshea nchi yetu. Na huo mfumo unafanyaje kazi?
Tuna kazi sana kizazi hiki kufuta huu ujinga uliowavaa watanganyika kwa muda mrefu wakiamini kuwa mfumo unaoweka watu wa kuwaibia na kuwadidimiza kwa kutumia chama ndio mzuri na hauna madhara ila demokrasia ambayo inalenga kuwapa raia mamlaka ya kuwa na maamuzi ya mwisho na kuamua hatima ya maisha yao ni mfumo wa kibeberu a.k.a mfumo kandamizi.

Yaani watanganyika wanaamini kabisa kuna siku hizi serikali za kidalali za kiafrika kama CCM ambazo zinaongozwa na wazee na mawazo ya kishamba na uongo uongo huku wao na familia zao wakizidi kuneemeka zitakuja kuwatoa katika ugumu wa maisha wanaopitia.
 
Inafikirisha sana. Eti demokrasia ni mfumo wa kibeberu, ukiwauliza ni mfumo gani mbadala unaofaa, hawana majibu!
 
Ni sahihi wanaharakati hawajafanya hayo,ila walihamasisha watu kwenda road kwa ulaghai kwamba jeshi litawalinda wananchi,kitu ambacho ni uongo

Kwahiyo nao hawawezi kwepa lawama ya kilichotokea
Kwanini waseme jeshi litawalinda? Ilikuwa liwalinde dhidi ya nani ndani ya nchi?
 
Hatuna tatizo na wao kupush maovu ya serikali na uchafu mwingine mwingi tu,ugomvi wetu na wao ni njia za kutatua changomoto hiyo

Njia ya kuhamasisha fujo na vurugu haikuwa njia sahihi
Wakati mwengine usahihi na sio usahihi inategemea na mtazamo wa mtu au mazingira ya wakati husika.
 
Lengo letu ni moja kumfanya mtanzania ajitambue,ajue wajibu wa kulinda amani ya nchi upo mikononi mwake,asitegemee kuna mtu atapambania amani ya Tanzania kama sio sisi wenyewe

Waache kutumiwa kwa manufaa ya wengine
Sio kweli mkuu suala la kulinda amani ni la pande zote mbili kwa maana ya serikali na wananchi, haiwezekani suala la kulinda amani uwe mzigo wa mwananchi tu ila serikali yeye ateke na kuuwa(ambayo sio matendo ya amani) halafu mwananchi avumilie tu kwa sababu ya ana wajibu wa kulinda amani.
 
Ni kweli sema raia walizani polis wanatania
Raia walijua kuwa watakutana na nguvu ya jeshi la polisi ila hawakujua kama polisi wangeweza kutumia nguvu ya kiwango kile cha mauwaji ya kikatili.
 
Raia walijua kuwa watakutana na nguvu ya jeshi la polisi ila hawakujua kama polisi wangeweza kutumia nguvu ya kiwango kile cha mauwaji ya kikatili.
Sijui kama watarudia baada ya kuujua uhalisia wa nguvu ya polisi naona hata D9 waliamua kubaki nyumbani
 
Mabeberu ni mataifa au makampuni au mitandao inayotumia fedha, mikopo au ushawishi wa sera ili kudhibiti nchi nyingine.

Ili uwe beberu unahitaji nguvu ya kiuchumi na kisiasa.

Nchi yenye uongozi kamili huhujumiwa kwa mikataba isiyo na usawa na mashinikizo ya kifedha au kidiplomasia.

Hiyo mifano ni hii hapa:
Classified 🚫
 
Sijui kama watarudia baada ya kuujua uhalisia wa nguvu ya polisi naona hata D9 waliamua kubaki nyumbani
Nguvu ya polisi kwa raia wasio na silaha, sidhani kama ni sahihi kujipa nguvu ya polisi kwa mazingira hayo at least yule Hamza alikuwa kipimo kizuri kujua nguvu ya polisi.
 
Anaye ihujumu Tanzania anajulikana
 
Mabeberu wana itaka tanzania kwa mali ghafi zake.
Hatukuwapa tumewapa wachina na warusi.
Ugomvi wote upo hapo.

Turudi kwenye siasa ya Ujamaa.
 
Nguvu ya polisi kwa raia wasio na silaha, sidhani kama ni sahihi kujipa nguvu ya polisi kwa mazingira hayo at least yule Hamza alikuwa kipimo kizuri kujua nguvu ya polisi.
Walitahadhalishwa kabla hawakusikia wakazani ni utani
 
Walitahadhalishwa kabla hawakusikia wakazani ni utani
Walitahadharisha kuwa watauwa kikatili bila kujali anayehusika au asiyehusika? Watu walijipanga kukabili virungu,mabomu ya machozi, kukamatwa na maji ya kuwasha.
 
Walitahadharisha kuwa watauwa kikatili bila kujali anayehusika au asiyehusika? Watu walijipanga kukabili virungu,mabomu ya machozi, kukamatwa na maji ya kuwasha.
Na wakajiandaa pia kuchoma Mali za watu hilo umelisahau
 
Na wakajiandaa pia kuchoma Mali za watu hilo umelisahau
Nalikumbuka hilo ila hilo halijatajwa kama ndio sababu ya yale mauwaji, hata wewe mwenyewe ukiangalia unaona ina make sense kweli kwamba yale mauwaji ni kwa sababu ya vibaka tu walikuwa wanachoma mali na kuiba huku wakiwa hawana silaha?
 
Hapana mimi sikubaliani kuwa ndio sababu kutakuwepo na sababu nyingine muhimu zaidi juu ya yaliyotokea

Ila hebu tufikirie mkuu, kwa kasi Ile ya uchomaji wa miundombinu wale jamaa wangeachwa nini kingetokea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…