Erdogan azitaka nchi za kiislamu kuungana dhidi ya taifa la Israel

Erdogan azitaka nchi za kiislamu kuungana dhidi ya taifa la Israel

Angalau wewe unaelewa ukweli ulivyo kwamba hakuna mbabe wa kuweza kuiondoa Israel pale alipo, hakuna.
Turkey aiondoe Israel pale kwa interests zipi?
Hata Hamas na Hezbollah wana interests tofauti lakini sema wana adui mmoja, inabidi uelewe hilo.

Interests za Iran, China na Russia ni tofauti japo wana ungana dhidi ya Magharibi, lakini kila mmoja anajua anachohitaji kwa sababu wana adui common.

Hivyo usifikiri watu wanaingia vitani kama walevi wa pombe vilabuni hata walevi wana interests zao utakuta wanapigania mwanamke n.k.

Endapo ikitokea Israel inaingilia maslahi ya Turkey kiuchumi hapo lazima watashikana mashati na Turkey kijeshi ni mkubwa kuliko Israel.

Ndio maana licha ya nchi za magharibi kui support Israel kwenye vita yake huko Palestine, hujaona Israel ikilalia upande wa Ukraine kwenye vita dhidi ya Russia, umesikia hata Israel anapeleka au amepeleka iron dome? Zelensky kuna kipindi alihitaji lakini kufanya hivyo ni kuingilia maslahi ya Russia kitu ambacho Israel inaifahamu vizuri Russia.. Israel wenyewe wanaogopa.
 
Angalau wewe unaelewa ukweli ulivyo kwamba hakuna mbabe wa kuweza kuiondoa Israel pale alipo, hakuna.
Turky, ataungana na iran, na mataifa ya afrika kaskazini haya ya kiislamu wakiongozwa na russia kwenda kuivamia israel kijeshi na still watashindwa hiyo vita haina miaka mingi itatokea, inaitwa Gog na Magog war. Kama vile haitoshi Kutatokea mtawala tokea jumuia ya ulaya atajifanya rafiki saaana wa israel kiasi cha israel kumuamini na kulegalega kijeshi baadae mtawala huyo ataongoza jeshi kubwa kutokea sehemu kubwa ya dunia kwenda kuipiga israel kweli israel itachapika ila mwishoni itashinda hiyo vita kimuujiza.
Katika vita zote kuna supernatural power zitakazoisaidia israel kushinda maana infact hayo mataifa mengine yatakuwa yakiongozwa na shetani kuivamia israel so Mungu atakuwa akiingilia kati na kuiwezesha israel kushinda.
Hivyo anachoongea erdogan ni kweli mataifa ya kadhaa ya kiislamu yataunganishwa na russia kuivamia israel na still yatakula kichapo.
 
Hili ni suala la human right abuse, hao ni wabaguzi wa kidini tu wanaendekeza udini kwenye human rights issue.

Wewe pia ni mbaguzi wa kidini ndiyo maana unaona ubaguzi wa kidini ni sawa tu.
Mimi si mbaguzi wa kidini ila "ukibaguliwa bagulika.
Si vyema kujipendekeza kwa mtu anayekubagua.
Lazima ujue thamani ya uwepo wako Duniani.
 
Kwa nini nchi za Kiislamu?

Afrika ya Kusini imeanzisha mpaka kesi dhidi ya Israel kwenye mahakama za kimataifa, na si nchi ya Kiislamu. Haoni kuwa kaitenga?
Ndio ujinga wao wa kiimani
 
Wataishia kuvimba tu kwenye vyombo vya habari lakini kukaa msitari wa mbele kupambana na Israel hilo sahau kuona wakiungana.

Kuna waarabu wenzao wengi tu wasiopenda uharamia wa Hamas na Houth kama Saudi Arabia na wengineo ambao wako chini ya USA na washirika wake.

Israel mbele kwa mbele.
Israeli hana uwezo wa kupambana na yoyote, bila msaada wa basha wake amerika tayari angekalishwa na Hamas.
 
Muulize Vladimir Putin askari wake Nagorno-Karabakh walipatwa na nini walipokutana na jeshi la Uturuki.
Israel hawezi simama na Uturuki abadan hata kwa mwezi.
Kama Hamas tu na Hizbollah wanamsumbua Israel je hiyo Uturuki itakuaje?
Hawajapigana
 
Mimi si mbaguzi wa kidini ila "ukibaguliwa bagulika.
Si vyema kujipendekeza kwa mtu anayekubagua.
Lazima ujue thamani ya uwepo wako Duniani.
Sasa watoto wasiojua kitu wa Gaza wamekubagua vipi?
 
Sasa watoto wasiojua kitu wa Gaza wamekubagua vipi?
Hizo jamii mbili Yahudi na Islamu zimekutana, wote ni wazee wa jino kwa jino. Na wote wanakawaida ya kujiona bora kuliko jamii zingine.
Kwao kufutiana vizazi ni kawaida.
Islam kuuwa na kuchinja watoto ni kawaida na Yahudi kuuwa na kuchinja watoto ni kawaida.
 
Unajibu swali ambalo sijakuuliza, wakati swali nililokuuliza hujalijibu.

Nimekuuliza hivi.

Sasa watoto wasiojua kitu wa Gaza wamekubagua vipi?
 
Unajibu swali ambalo sijakuuliza, wakati swali nililokuuliza hujalijibu.

Nimekuuliza hivi.

Sasa watoto wasiojua kitu wa Gaza wamekubagua vipi?
Hayo ni mazungumzo baada ya habari.
Mada ni edogan katubagua sio mimi nimebagua.
Edogan anataka jumuia za kiislamu ziingilie kati, maana yake ni kwamba km wewe sio muislamu hayakuhusu hata hao
watoto wa Gaza hawakuhusi
 
Hii vita ni ya Wapalestina na WaIsraeli.

Kama Wapalestina wanaonewa, Wapalestina wanahitaji support ya kila mtu, kwa sababu za haki za kibinadamu, si kwa sababu za kidini.

Erdogan si msemaji wa Wapalestina, ni mpambe tu mwenye matatizo yake ya kisiasa na huenda anatumia vita hii kupata umaarufu kisiasa, cheap popularity. Huko kwao Uturuki kuna Waislamu kibao anawanyanyasa, kama kweli anawapenda Waislamu wenzake mbona yeye mwenyewe ananyanyasa Waislamu wenzake kwao?

Hizi ni sarakasi za kinafiki za kisiasa tu, kwa nini unaruhusu mwanasoiasa akutoe kwenye reli ya mambo ya haki za binadamu, kwa kauli za kidini?

Kwa nini unaruhusu mtu ambaye hata si muhanga wa vita kujifanya yeye ndiye msemaji wa wahanga halisi?

Inaonekana kama unatumia hisia zako zaidi ya mantiki.
 
Umeongea vyema
Ila kwa upande wangu sioni kama wapalestina wanaonewa kiasi cha kuwahurumia.
Wameyaanzisha wenyewe, wayamalize wenyewe.
Oct 7 waliuwa watu wasio na hatia hawakuchagua wakuuwa na walisherekea kwa nderemo na vifijo.
Hapo wamekutana na wazee wa jino kwa jino.
Usinifundishe kuhurumia watu wasio na huruma.
 
Kwa nini unaanzia na Oct 7 kama vile mgogoro wote umeanzia Oct 7 wakati mgogoro ni wa muda mrefu?
 
Back
Top Bottom