Nikisema wewe hakuna unachojua nitakua nakosea!??
Hao BRAZIL,SPAIN,COLOMBIA,MEXICO,BELGIUM wote walifanya maamuzi baada ya kuona kilichofanyika na kilichosikika Arab peace summit.
Arab peace summit walihudhuria takriban MATAIFA YOTE YA G20 ikiwemo South Africa.
Kiongozi wa Brazil,Spain,Colombia n.k n.k wote walihudhuria,na wakatoa risala zao na maoni yao ya nini kifanyike juu ya mzozo wa Israel dhidi ya Gaza.
Na katika hiko kikao Elsisi na viongozi wengine walionesha ushahidi na mlolongo mzima wa kilichotokea Gaza kuanzia August mpaka kuja Oktoba 7.
Pia wakajadili mzozo kuanzia 1947 ilipochorwa mipaka ya Israel na Palestina kuja mpaka mipaka ya sasa ya Palestina iliyodhulumiwa.
Hadi ANTONIO GUTTERES GS wa UN alihudhuria.
Ndipo alitoa tamko UN security council akisisitiza kuwa"the cause of conflict is not October 7,this did not start October 7".
Asingeongea haya kama asingehudhuria Arab peace summit na kusikiliza na kuoneshwa ushahidi na WAARABU wenyewe kuhusu mzozo wa Gaza.
Na kikao kimoja cha mwisho kilifanyika wakati wa kutoa tuzo za UNRWA,kilifanyika DOHA QATAR.
Sheikh Tamim Al Thani alitoa hotuba ya wito wa mataifa yote kuungana na Palestina.
Hiko kikao viongozi wa mataifa ya EU walihudhuria akiwemo waziri wa haki za kibinadamu wa SPAIN.
Baada ya hapo ndipo mataifa yakaona alichofanya Israel ndio wakachukua hatua.
Kama isingekua WAZUNGU NA SOUTH AFRICA kuhudhuria Arab peace summit basi wasingejua ukweli uliotokea Gaza na wasingekua na mwangaza wa kufungua kesi na kwenda kinyume na Israel.
HUO USHAHIDI ALOTUMIA S.AFRICA KWENDA ICJ ALIUTOA ARAB PEACE SUMMIT.
Au wewe ulidhani kisa ni Arab peace summit basi walihudhuria mataifa ya kiarabu peke yake!!??
Hadi viongozi wa Botswana walihudhuria.
Walichofanya waarabu ni kumpa mbwa jina baya kwanza,walitumia mlengwa wa kisiasa ama kidiplomasia kuionesha dunia Israel ni taifa la namna gani,na hiyo imelipa.
Kiufupi Arab Peace Summit ndio iliyowaamsha South Africa na mataifa mengine kwenda kinyume na Israel.
Bado mweupe kuhusu huu mzozo wa middle east hujui siasa za dunia zinaendaje.