Summit zinasaidia nini ama zimeisaidia nini Palestina?. Matokeo ya hizo summits ni nini, yako wapi maamuzi ya summits?
South Afrika haikuhitaji Summits kuishtaki Israel. Mexico haikuhitaji Summits kujiunga kwenye kesi. Jana Brazil haikuhitaji Summits kumuondoa balozi wake Israel sababu ya mauaji, Colombia haikuhitaji Summits kumuondoa balozi wake Israel na kumtuhumu Netanyahu hadharani.
Nchi pekee yenye ujasiri wa kuishtaki Israel ni South Africa. Nchi nyingine zimeunga mkono mashtaka lakini hakuna nchi ya kiarabu iliyotangaza kujiunga kwenye kesi.
Kesi ya SA dhidi ya Israel imeleta matokeo mengi sana mazuri, Netanyahu kutakiwa kukamatwa, lakini pia imeonyesha unafiki na mgawanyiko wa nchi nyingi za Ulaya watetezi wa haki za Binadamu waliotangaza kuiwekea vikwazo ICC ili kuilinda Israel na wengine kutangaza kumkamata Netanyahu ikiwa atahitajika ICC.
Nchi za Ulaya, Norway, Spain na Ireland kutangaza kuitambua Palestina kama nchi na kuweka bendera yake kwao na kutangaza kutaka wapewe mabalozi, nchi gani ya kiarabu imefanya hivyo?
Wakati hayo yanafanyika waumini wa dini ya Allah alikozaliwa Allah mwenyewe na mtume wake wao wanaendesha summits tu Cairo na kwingineko, hovyo kabisa. Wamuombe basi allah aingilie kati maana wao wameshindwa.
Nikisema wewe hakuna unachojua nitakua nakosea!??
Hao BRAZIL,SPAIN,COLOMBIA,MEXICO,BELGIUM wote walifanya maamuzi baada ya kuona kilichofanyika na kilichosikika Arab peace summit.
Arab peace summit walihudhuria takriban MATAIFA YOTE YA G20 ikiwemo South Africa.
Kiongozi wa Brazil,Spain,Colombia n.k n.k wote walihudhuria,na wakatoa risala zao na maoni yao ya nini kifanyike juu ya mzozo wa Israel dhidi ya Gaza.
Na katika hiko kikao Elsisi na viongozi wengine walionesha ushahidi na mlolongo mzima wa kilichotokea Gaza kuanzia August mpaka kuja Oktoba 7.
Pia wakajadili mzozo kuanzia 1947 ilipochorwa mipaka ya Israel na Palestina kuja mpaka mipaka ya sasa ya Palestina iliyodhulumiwa.
Hadi ANTONIO GUTTERES GS wa UN alihudhuria.
Ndipo alitoa tamko UN security council akisisitiza kuwa"the cause of conflict is not October 7,this did not start October 7".
Asingeongea haya kama asingehudhuria Arab peace summit na kusikiliza na kuoneshwa ushahidi na WAARABU wenyewe kuhusu mzozo wa Gaza.
Na kikao kimoja cha mwisho kilifanyika wakati wa kutoa tuzo za UNRWA,kilifanyika DOHA QATAR.
Sheikh Tamim Al Thani alitoa hotuba ya wito wa mataifa yote kuungana na Palestina.
Hiko kikao viongozi wa mataifa ya EU walihudhuria akiwemo waziri wa haki za kibinadamu wa SPAIN.
Baada ya hapo ndipo mataifa yakaona alichofanya Israel ndio wakachukua hatua.
Kama isingekua WAZUNGU NA SOUTH AFRICA kuhudhuria Arab peace summit basi wasingejua ukweli uliotokea Gaza na wasingekua na mwangaza wa kufungua kesi na kwenda kinyume na Israel.
HUO USHAHIDI ALOTUMIA S.AFRICA KWENDA ICJ ALIUTOA ARAB PEACE SUMMIT.
Au wewe ulidhani kisa ni Arab peace summit basi walihudhuria mataifa ya kiarabu peke yake!!??
Hadi viongozi wa Botswana walihudhuria.
Walichofanya waarabu ni kumpa mbwa jina baya kwanza,walitumia mlengwa wa kisiasa ama kidiplomasia kuionesha dunia Israel ni taifa la namna gani,na hiyo imelipa.
Kiufupi Arab Peace Summit ndio iliyowaamsha South Africa na mataifa mengine kwenda kinyume na Israel.
Bado mweupe kuhusu huu mzozo wa middle east hujui siasa za dunia zinaendaje.