Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
- Thread starter
- #81
Nakubaliana na wewe kwa wakati fulani inaweza kuwa msaada ingawa mara chache sanaMi naona ni sawa...
Kuna kijana alivamiwa na vibaka wakampiga na kumjeruhi, wakaiba simu yake na kuondoka...
Baada ya siku chache kuna kijana mmoja akaenda na hio simu kwa fundi itolewe zile PIN/lock sasa sikujua ni mmoja wa wale vibaka au labda aliuziwa na wale vibaka... ile simu yule kijana aliyejeruhiwa alikuwa ameweka picha yake, yule fundi simu kuona ile simu na ile picha kwenye screen saver kumbe anamfahamu yule kijana aliyeibiwa simu ...
Fundi akawapigia ndugu za yule kijana, kijana alikuwa hospitali kalazwa kwa matibabu.. walimpiga kichwani na kitu kina ncha kali...
Ndugu walikuja na polisi wakamkamata yule jamaa mwenye simu, msako ukafanyika wakakamatwa wote waliohusika..
Yule kijana alifia hospitalini akiwa anapatiwa matibabu, wale vibaka nadhani walihisi walivyomjeruhi labda angepona...
Kwa wakati fulani inaweza kuwa na msaada... na sidhani kama ni vibaya...