Umuofia Kwenu wana JF,
Bonne Annee and X-mas!!
Ndugu Sigfrid Sisti Kimbi na familia yake yote yateketea kwa moto uliotokana na gesi! Mke na watoto mapacha wawili ndio walianza kufa na mme amefariki akiwa njiani anakimbizwa hospital KCMC kwa matibabu.
=======
Ndugu zangu sisi familia ya Kimbi tumepata janga kubwa na msiba mzito ambao bila maombi hatuwezi kuukabili.
Ndugu yetu Sigifrid Sist Kimbi aliunguliwa na nyumba tarehe 25 kuamkia tarehe 26 na familia nzima wakiwa ndani wamelala. Bahati mbaya kabisa mkewe na watoto wetu wawili walifariki dunia siku hiyo hiyo kwa kuungua vibaya sana na moto huo.
Ndugu yetu alikimbizwa hospital na kuanza kupatiwa matibabu. Jana tuliendelea kuandaa mazishi ya mkewe na watoto ili tuwazike leo. Wakati tukijipanga jana jioni ndugu Sigifrid nae akafariki dunia. Kwa hiyo leo tunawahifadhi kaburini familia nzima ya Sigi Kimbi.
Kwa niaba ya familia tunawashukuru wote mnaoendelea kutushika mkono kwa chochote Mungu alichowajaalia katika kuhakikisha tunafanikisha mazishi haya. Tunaomba msichoke kutuombea maana jambo hili hi gumu mno ktk mioyo yetu. Peke yetu bila sala hatuwezi. Tunaendelea kuwashukuru sana.
Mazishi yatafanyika leo Uru Kisomboko karibu na Uru seminary. Mungu awalaze roho za marehemu pema peponi amina.
28/12/2020
View attachment 1660824
View attachment 1660825
View attachment 1660826
View attachment 1660828