Kuna manzi mmoja nlimtania tu alifika ofisini kwangu nikachukua namba yake ya simu...aisee hata sijamtongoza tayari kashaanza kuniita baby, sijakaa vizuri vibomu ,vinaanza ...mara ooh baby ninashida ya pesa naomba nitumie.Nikamchekecha tu kuwa askilizie kuna ishu ikikaa poa ntamtumia....dah zilianza txt kama ugomvi ....umenidanganya hujanitumia, vp unantumia saa ngapi...n.k nkamrushia pesa ...kesho yake kuamka tu anashida tena ya pesa, mara sijui ana njaa hajanywa chai, mara sijui ana shida hii na ile .....ukicheki ni mke wa mtu. Nmempotezea mazima akipiga simu yake naiangalia tu siipokei.
Some women are disgusting parasites, hawana faida yoyote zaidi ya kukunyonya tu.
Kuna mwingine nilikuwa na namba yake muda mrefu tu, siku nikamtxt tu...kwenye kuchat ..akaanza nina shida ya kiasi kadhaa niazime ntakurudishia ..daaah nikampa kumpima tu ila nlijua kuwa hapa hakuna mpango wa kurudishiwa, mara ametengeneza mazingira niwe mpenzi wake , sijakaa vizuri vibomu vinaanza mara sijui nina shida ya pesa hivi, mara sijui hapa nadaiwa kwenye biashara ,mara mtoto wangu anaumwa sina pesa ya hospitali n.k .Nikaancha kumpa attention, na yeye akapunguza mawasiliano na mimi, nikimtxt hajibu sms zangu kama mwanzo ,unaweza ukamtxt watsapp ukaona blue ticks halafu asijibu, nikakata mawasiliano , ila cha ajabu hanitafuti mpk awe na shida ya kitu kutoka kwangu .Nishamjulia nami namfungia tinted tu.
Duniani kuna wanawake wawili tu ndio wamekuwa wema kwangu, wa kwanza ni Mama yangu kipenzi (Mungu amjaalie afya na umri wenye baraka tele) na wa pili ni mke wangu kipenzi. Hawa ndio wanawake bora kwangu.
Mke wangu alinipenda in a mysterious unconditional way na kama nikifanikiwa huko mbeleni naweza kuandika kitabu juu yake. Nathubutu kusema kuwa sijapata na sidhani kama ntakuja kupata tena mwanamke kama yeye mpk naondoka katika mgongo huu wa ardhi.