Fatma Karume ataka uondolewe ukakasi kwenye mchango wa gari la Lissu ndio achangie

Fatma Karume ataka uondolewe ukakasi kwenye mchango wa gari la Lissu ndio achangie

Unasema uongo bila hata aibu! Fatma amesema wapi kuwa hatachangia mpaka suala la bima litakapowekwa wazi? Yeye amesema ni wajib wake kuchangia.

Hilo la bima ni ushauri tu na sio sharti. Kuwa ingekuwa vyema kama Lissu angeeleza kama alilipwa chochote kutokana na Bima ya gari.

Amandla...
Amandlaaaaaa, umkomthowesizwe [emoji123]
 
Kwamba bima itakubali kulipia alafu gari wamuachie Lissu?

Alafu ile gari inahitaji matengenezo iweje bima ilipe gharama za gari lote ili hali gari ni la matengenezo?

Maana sababu kubwa ya wananchi kuchangia ni gari kubaki kua kama kumbukumbu,(libaki kama lilivyo baada ya kushambuliwa)
Waambie hao wasiyo amini
 
Ila chadema ni mataaira[emoji1787][emoji1787][emoji1787] sasa anataka gari la milioni 30 na watu wanamchangia, kwani lissu alikua anafanya kazi gani kabla hajawa mbunge? [emoji1787] yani cdm wakiishika hii nchi kuiongoza mi nahamia guantanamo[emoji1787] na wanachama wanachangia eti ni WAJIB[emoji1787]
Hata ukijinyonga kajinyonge tu maana huna faida yoyote kwenye jamii ya watanzania.
 
Tundu Lissu ameomba huruma kwa wananchi wamchangie ili apate gari lingine, alivyo mjanja sasa alikaa na Maria sarungi ambaye hana shughuli za kufanya wakatengeneza dili LA kupiga hela,kwamba maria aanzishe mchango na Kisha atakula 10%, kimsingi gari la lissu lilikuwa na bima na lissu ni lawyer na anajua madhara yakuendesha gari bila bima, ss inakuwaje unaomba uchangiwe hela ukanunue gari wakati gari ilikuwa na insurance, halafu tang uanzishe harakati hizo na kimada wako kwanin chama chako kimekaa kimya hakiungi mkono jambo hilo? Unajifanya mwadilifu kumbe mwizi tu kama walivyo wezi wenzio.
Wewe ni zaidi ya nguchiro
 
Bima huwa ni mwaka moja tuu, hii gari ya Lissu ilikuwa polisi tangia September 2017kwa hiyo bima ili expire zamani sana na Polisi siyo jukumu lao ku renew
Unakosea. Malipo ya Bima ni wakati tukio lilipotokea, sio baada. Ukiongelea Bima baada ina maana angeendelea kulipa Bima baada ya gari kuharibiwa.

Na pia kuna vigezo kwa Bima kulipa - wanaweza kulipa ili lifanyiwe matengenezo, kwa sababu wanaweza kusema gari sio right off
 
Kupitia akaunti yake ya X mwanamama mwenye misimamo mikali Bi Fatma Karume amehoji juu ya sintofahamu ya michango ya Lissu.
Amehoji kwa nini asilipwe gari na bima wakati gari ilikuwa na bima?

Ametaka huu ukakasi uondolewe ndio achangie.

Na mimi namuunga mkono kwenye hili.

Tundu asije tufanyia ujanja wa kuchukua michango ya wananchi na kuzunguka kampuni ya bima kuchukua hela zake.

Tuwe makini na hii michango isiyokuwa na auditing ambayo imeshamiri kwenye chadema.
View attachment 3001416
Fatima aelimishwe. Lengo ni kwamba gari lisitengenezwe ili libaki kama kumbukumbu ya harakati za demokrasia katika kipindi cha Magufuli. Michango haifanywi kwa kuwa Bima hawajalipa au hawatalipa, au Tundu amesema hawezi kutengeneza. Tundu ameombwa asilitengeneze gari na achangiwe jingine ili hilo lenye matundu 30 ya risasi libaki kama memorabia.

Mfikishieni Fatma huu ujumbe ili achangie kama anataka kuchanga
 
Ila chadema ni mataaira🤣🤣🤣 sasa anataka gari la milioni 30 na watu wanamchangia, kwani lissu alikua anafanya kazi gani kabla hajawa mbunge? 🤣 yani cdm wakiishika hii nchi kuiongoza mi nahamia guantanamo🤣 na wanachama wanachangia eti ni WAJIB🤣
Tatizo kubwa la JF ni kuwa kila mtu ana haki ya kuitwa mwana JF na kutoa maoni yake
 
Hajaombwa mchango na wala sio lazima yeye kuchanga wanao jisikia kuchanga bila kihoji watanga tuu
Ni kweli kuchangia siyo lazima, lakini usisahau kuwa Tundu Lisu ni mwanasiasa, kila kinachofanywa na mwanasiasa ni hoja.
Maana kuna siku mwanasiasa aweza kuwa kiongozi wa jamii.
Aje hadharani ajibu, ndiyo siasa.
 
Back
Top Bottom