Fei Toto agonga mwamba TFF, bado ni mali ya Yanga

Umebaki mwaka 1. Aondoke bure, Kuna timu italeta ofa kubwa kweli mezani?
Unajua Yanga wameandika barua TFF kwamba hawamuoni Fei,ile barua ina maana kubwa sana kwani Feisal mpaka sasa bado mkatataba wake umebakia mwaka na nusu, sema wanasheria wake Fei wanamdanganya.Ile barua bado TFF hawajapanga siku ya kuisikiliza,kwani Fei atapewa adhabu na kurudi kuitumikia Yanga kwa sehemu ya mkataba uliobakia (mwaka na nusu).

Katafuteni Intv aliyo ifanya Rage YouTube ndio mtaelewa, iliyo barua ya pili ni mtego mwengine wa kisheria wa Fei na yy kishajaa.
 
Asiporudi? Ni rungu gani kubwa linaweza mkuta kutoka TFF au Yanga?
 
Wakati wenzio wanasoma sheria wewe ulikuwa unawinda ndege na Mzee wako mashambani.

Nani kakwambia kuna WAnasheria wa kesi za mashamba?


Anyway issue inaenda CAS ndio utajua Kati ya WAnasheria wa YAnga na Fatma Nani ni Bora !
 
Yanga wanalipa kutokana.na masharti ya mkataba. Hawafanyi Kama fadhila. Fei yupo yanga bado na huo mfano wako wa umeme kukatika hauingii hapo. Fei hajaondoka Yanga.
Fei yupo wapi? Mshahara wa mwezi huu uliopita aliupokea?
 
Asiporudi? Ni rungu gani kubwa linaweza mkuta kutoka TFF au Yanga?
Kupigwa faini au hata kufungiwa na kurudi kuitumikia club yake kwa sehemu ya mkataba uliobakia (mwaka na nusu).Mpaka sasa Yanga hawajui Fei yupo wapi.
 
Hii sio kesi ya Jamhuri dhidi ya Yanga, Kuna kesi na shauri na wenye shauri lao watapewa nakala ya maamuzi ya shauri lao, wakitaka wataweka public wasipotaka huna mamlaka ya kuambiwa wewe au umma vipengele walivyotumia. Yanga na Fei ndio wanaopewa nakala zao na usiwe bendera fata upepo. Sio kila kesi lazima iwe public, Kuna mapitio mengine yanabaki siri kwa wenye mashauri hayo.
 
Nimependa alichozungumza yule jamaa yake jaydee sijui anaitwa edward kumwembe,ushauri wake mzuri japo mimi simtambui kama mchumbuzi
Kasemaje? Edo niliacha kumfuatilia baada ya kuona kaacha kuwa mwanahabari kaamua kuwa shabiki wa Arsenal....nilimfuata kama mwanahabari kwenye kurasa zake.
 
Dogo mpira ndio umeishia hapo. Akaungane na Kamanda wa connection visiwani
 
Kupigwa faini au hata kufungiwa na kurudi kuitumikia club yake mwa sehemu ya mkataba uliobakia (mwaka na nusu).Mpaka sasa Yanga hawajui Fei yupo wapi.
Faini inaweza kuwa zaidi ya kile alichokiweka kwenye akaunti alipotaka kuvunja mkataba? Najaribu kutafuta "WIN" ya yanga.
 
Faini inaweza kuwa zaidi ya kile alichokiweka kwenye akaunti alipotaka kuvunja mkataba? Najaribu kutafuta "WIN" ya yanga.
Faini inaweza kuwa ya kawaida, ila mchezaji kukaa nje bila kucheza ni zaidi ya faini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…