Tayana-wog
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 24,844
- 29,126
Kazingua."Baba ni mpambanaji alipambana sana mpaka dakika ya mwisho lakini kwa yaliyotokea tunasema ni kazi ya Mungu na kama familia tulipokea kwa amani kabisa, tunasema acha baba apumzike...
Viongozi wafundishe watt wao jinsi ya kushukuru ,hii ni kufuru kwakweli.Hii ni zaidi ya kufuru, kumpa mwanadamu mwenzako utukufu sawa na mwenyezi Mungu.
Stahiki ni kwa aliyewahi kuwa PM haijaliishi aliacha vipi hiyo nafasi. Hata Ndugai anapata stahiki za aliyewahi kuwa Spika.Stahiki za mstaafu na aliyeacha kazi zikoje?
Aliyewahi kuwa PM na PM mstaafu zinapaswa kuwa na maana mbili tofauti.
Nadhani sababu ya watu kutokuwa na uwajibikaji wa KUJIUZULU, ni kwasababu, nadhani unapaswa kukosa stahiki zako zote!
Uchawa tu..kama isingekuwa mama Samia Suluhu Hassan baba yetu asingefika hata hiyo juzi,
Naona chadema wamepanga ndani ya kichwa chako.Chadema watakuja kumponda huyo mtoto...na kutukana...wao walitaka kusikia lawama zinaenda Ccm na ikiwezekana Kwa Rais Samia
Numbisa unataa nini walah🤣Duh pesa inarefusha uhai,pesa pesaaa
Kauli Ina ukakasi japo ufafanuzi wake una mantiki."Baba ni mpambanaji alipambana sana mpaka dakika ya mwisho lakini kwa yaliyotokea tunasema ni kazi ya Mungu na kama familia tulipokea kwa amani kabisa, tunasema acha baba apumzike...
CCM imewezesha yote hayo😅Hii nchi ukishakua rais unakua kama Mungu vile
Nani aliwahi kuwa mwema sana Kwa watu maskini na shida zao akazimaliza?Ni sawa kuwa mwema kwa binadamu wenzio hasa ukiwa katika nafasi aidha ya uongozi ama kifedha lakini si sawa kubagua misaada yako iwe kwa walionazo tu na si makapuku wanaostahili hasa msaada wako.
Samia ni mwema sana kwa matajiri/watu maarufu na wanasiasa lakini walio chini kabisa kila siku wanazidi kulia kwa hali mbaya na ugumu wa maisha.
Kuna watu nawajua zaidi ya wawili wa hali ya chini na wana kisukariHayo ni Maradhi yako kutokana na Life Style zaidi Tajiri hatembei kwa miguu anatembea kwa Motokari Tajiri anakula kula vyakula kama unavyojua Diet za Kiafrika mkaango mwingi.
Masikini kwa upande mwingine anatembea kwa miguu sana anakula Ugali na Nsansa akibahatika na Kauzu maskini wa Kiafrika maradhi yake labda Ujinga.
"Baba ni mpambanaji alipambana sana mpaka dakika ya mwisho lakini kwa yaliyotokea tunasema ni kazi ya Mungu na kama familia tulipokea kwa amani kabisa, tunasema acha baba apumzike"
"Lakini katika vita yake hii ya kupigania maisha yake lazima niseme kipekee naomba sana kutoa shukrani za familia kwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, niseme ukweli kutoka moyoni, kama isingekuwa mama Samia Suluhu Hassan baba yetu asingefika hata hiyo juzi, mama Samia amekuwa ni ndugu, amekuwa mzazi na mlezi wetu hatuna cha kumlipa" - Fredrick Edwad Lowassa, Mtoto wa Hayati Lowassa
Hakuna haja ya kumlaumu mfiwa,Badala ya kuwashukuru madaktari yeye anashukuru Mama .... kwa vile tu pesa ya nchi hii haitoki bila mkono wa Mama.Mungu mtu wa Bongo...
Chadema watakuja kumponda huyo mtoto...na kutukana...wao walitaka kusikia lawama zinaenda Ccm na ikiwezekana Kwa Rais Samia
Hakuna haja ya kumlaumu mfiwa,
Ni hakika matibabu ya Hayati yanaweza kuwa yamegharimikiwa na serikali kwa kuwa kwa nafasi yake anastahili hivyo
Lakini,ni kweli hatujui kuwa kila pesa ya serikali inapotolewa kufanya jambo lolote inasewa "Mama ametoa" na sifa zote zinaenda kwake? Kwa hiyo kwa tafsiri ya haraka haraka watu watajua Mama ametoa msaada kumbe ni stahiki za mhusika
Tusimlaumu mtoto wa ENL maana yuko na majonzi,kwa kuwa hata wale ambao wanakua hawajafiwa wako fit kabisa hutumia kauli hizo hizo za tunamshukuru Mama kwa kutupatia hiki na kile
Huyo mzee kaiba hela nyingi sana haitqji hela ya samia kutibiwa muhimbili,fred kavimbiwaHakuna haja ya kumlaumu mfiwa,
Ni hakika matibabu ya Hayati yanaweza kuwa yamegharimikiwa na serikali kwa kuwa kwa nafasi yake anastahili hivyo...
Mkuu siku inakuwa haijafika.Duh pesa inarefusha uhai,pesa pesaaa
Fred nae bhwana, (hata ukiwa mfiwa bado unafikiria cheo) kwani Samia ndiye alikuwa anamhudumia hospitali?"Baba ni mpambanaji alipambana sana mpaka dakika ya mwisho lakini kwa yaliyotokea tunasema ni kazi ya Mungu na kama familia tulipokea kwa amani kabisa, tunasema acha baba apumzike"
"Lakini katika vita yake hii ya kupigania maisha yake lazima niseme kipekee naomba sana kutoa shukrani za familia kwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, niseme ukweli kutoka moyoni, kama isingekuwa mama Samia Suluhu Hassan baba yetu asingefika hata hiyo juzi, mama Samia amekuwa ni ndugu, amekuwa mzazi na mlezi wetu hatuna cha kumlipa" - Fredrick Edwad Lowassa, Mtoto wa Hayati Lowassa