Fredrick Lowassa: Kama sio Rais Samia, Baba asingefika juzi

Fredrick Lowassa: Kama sio Rais Samia, Baba asingefika juzi

"Baba ni mpambanaji alipambana sana mpaka dakika ya mwisho lakini kwa yaliyotokea tunasema ni kazi ya Mungu na kama familia tulipokea kwa amani kabisa, tunasema acha baba apumzike...
Kazingua.

Samia ni Mungu?

Ndo maana Huwa wanasema ukifiwa hutakiwi hata kuongea
 
Stahiki za mstaafu na aliyeacha kazi zikoje?

Aliyewahi kuwa PM na PM mstaafu zinapaswa kuwa na maana mbili tofauti.

Nadhani sababu ya watu kutokuwa na uwajibikaji wa KUJIUZULU, ni kwasababu, nadhani unapaswa kukosa stahiki zako zote!
Stahiki ni kwa aliyewahi kuwa PM haijaliishi aliacha vipi hiyo nafasi. Hata Ndugai anapata stahiki za aliyewahi kuwa Spika.

Sio kila mtu anayejiuzulu anafanya hivyo kwa sababu anakiri kuwa alifanya makosa. Wakati mwingine kujiuzuru ni ishara ya kuwajibika kwa matendo yaliyofanywa na walio chini yako au mambo yaliyotokea katika taasisi unayoongoza. Wakati mwingine mtu anajiuzuru kwa kushinikizwa hata kama hajafanya kosa lolote.

Wakati mwingine mtu anajiuzuru kuepuka kufukuzwa kwa sababu anajua mwenye madaraka juu yake hamtaki kwa sababu zake mwenyewe. Mtu anajiuzuru ili kuwaokoa wengine ambao wangeweza kuathirika kama angebakia.Unaweza kusema kuwa kujiuzuru kwa Lowassa kulipunguza joto kwenye serikali yake kuhusu mkataba wa Richmond.

Sasa ukitaka kuwaadhibu wanaojiuzuru hatajiuzuru mtu hata kama morali alipaswa kujiuzuru. Wengi hawataki kujiuzuru kwa sababu wanajua itachukuliwa kama wanakiri makosa hata kama sivyo.

Amandla...
 
"Baba ni mpambanaji alipambana sana mpaka dakika ya mwisho lakini kwa yaliyotokea tunasema ni kazi ya Mungu na kama familia tulipokea kwa amani kabisa, tunasema acha baba apumzike...
Kauli Ina ukakasi japo ufafanuzi wake una mantiki.

Tunamsamehe Kwa kuteleza ulimi.
 
Ni sawa kuwa mwema kwa binadamu wenzio hasa ukiwa katika nafasi aidha ya uongozi ama kifedha lakini si sawa kubagua misaada yako iwe kwa walionazo tu na si makapuku wanaostahili hasa msaada wako.

Samia ni mwema sana kwa matajiri/watu maarufu na wanasiasa lakini walio chini kabisa kila siku wanazidi kulia kwa hali mbaya na ugumu wa maisha.
Nani aliwahi kuwa mwema sana Kwa watu maskini na shida zao akazimaliza?
 
Hayo ni Maradhi yako kutokana na Life Style zaidi Tajiri hatembei kwa miguu anatembea kwa Motokari Tajiri anakula kula vyakula kama unavyojua Diet za Kiafrika mkaango mwingi.

Masikini kwa upande mwingine anatembea kwa miguu sana anakula Ugali na Nsansa akibahatika na Kauzu maskini wa Kiafrika maradhi yake labda Ujinga.
Kuna watu nawajua zaidi ya wawili wa hali ya chini na wana kisukari
 
"Baba ni mpambanaji alipambana sana mpaka dakika ya mwisho lakini kwa yaliyotokea tunasema ni kazi ya Mungu na kama familia tulipokea kwa amani kabisa, tunasema acha baba apumzike"

"Lakini katika vita yake hii ya kupigania maisha yake lazima niseme kipekee naomba sana kutoa shukrani za familia kwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, niseme ukweli kutoka moyoni, kama isingekuwa mama Samia Suluhu Hassan baba yetu asingefika hata hiyo juzi, mama Samia amekuwa ni ndugu, amekuwa mzazi na mlezi wetu hatuna cha kumlipa" - Fredrick Edwad Lowassa, Mtoto wa Hayati Lowassa

Familia haina shida ya pesa sasa Mama kasaidia lipi?. Ugojwa wake ulikuwa hauna dawa zaidi ya therapy tu za kupunguza makali
 
Badala ya kuwashukuru madaktari yeye anashukuru Mama .... kwa vile tu pesa ya nchi hii haitoki bila mkono wa Mama.Mungu mtu wa Bongo...
Hakuna haja ya kumlaumu mfiwa,

Ni hakika matibabu ya Hayati yanaweza kuwa yamegharimikiwa na serikali kwa kuwa kwa nafasi yake anastahili hivyo

Lakini,ni kweli hatujui kuwa kila pesa ya serikali inapotolewa kufanya jambo lolote inasewa "Mama ametoa" na sifa zote zinaenda kwake? Kwa hiyo kwa tafsiri ya haraka haraka watu watajua Mama ametoa msaada kumbe ni stahiki za mhusika

Tusimlaumu mtoto wa ENL maana yuko na majonzi,kwa kuwa hata wale ambao wanakua hawajafiwa wako fit kabisa hutumia kauli hizo hizo za tunamshukuru Mama kwa kutupatia hiki na kile
 
..yuko kwenye majonzi lakini uchawa hajasahau!!
 
Hakuna haja ya kumlaumu mfiwa,
Ni hakika matibabu ya Hayati yanaweza kuwa yamegharimikiwa na serikali kwa kuwa kwa nafasi yake anastahili hivyo...
Huyo mzee kaiba hela nyingi sana haitqji hela ya samia kutibiwa muhimbili,fred kavimbiwa
 
"Baba ni mpambanaji alipambana sana mpaka dakika ya mwisho lakini kwa yaliyotokea tunasema ni kazi ya Mungu na kama familia tulipokea kwa amani kabisa, tunasema acha baba apumzike"

"Lakini katika vita yake hii ya kupigania maisha yake lazima niseme kipekee naomba sana kutoa shukrani za familia kwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, niseme ukweli kutoka moyoni, kama isingekuwa mama Samia Suluhu Hassan baba yetu asingefika hata hiyo juzi, mama Samia amekuwa ni ndugu, amekuwa mzazi na mlezi wetu hatuna cha kumlipa" - Fredrick Edwad Lowassa, Mtoto wa Hayati Lowassa
Fred nae bhwana, (hata ukiwa mfiwa bado unafikiria cheo) kwani Samia ndiye alikuwa anamhudumia hospitali?
 
Back
Top Bottom