Wewe kwa akili yako, unaamini kwamba hayo mashirika ya kimataifa na nchi wafadhili wanafurahishwa na huo ujinga wa chadema wanaomfanyia Mama? Ulishaona kwao vyama vya upinzani vinafanya maujinga kama ya chadema nchini kwao? Upinzani unafanywa kwa nguvu ya hoja zenye ushawishi kwenye mabunge yao na baada ya hapo mabunge yao hupiga kura ya kukubali hoja au kuikataa na mambo huishia hapo; na maamuzi ya mabunge hayo huheshimiwa na kila mtu na kutekelezwa. Ndiyo maana ya demokrasia. Inavyofanya kazi kupitia wawakilishi wa wananchi kwenye mabunge yao. Demokrasia haimaanishi vyama vya upinzani kujambajamba ovyo mitaani na kuchafua hewa wanayovuta wananchi.
Mnajua kabisa kwamba hoja yenu ya katiba mpya ya Waryoba haiwezi kushinda kwenye bunge letu la sasa. Mngalikuwa na akili mngalisubiri kunadi hoja yenu hiyo nchi nzima na kwa nguvu zote kwa watanzania wote wakati wa kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 ili wananchi waamue. Kipindi hicho huwa ni kuanzia miezi 3 kabla ya uchaguzi mkuu kwa mjibu wa sheria na katiba ya nchi yetu. Mngalikuwa na akili mngalijua kwamba kufanya hivyo sasa hivi ni kuvunja sheria na katiba ya nchi na hivyo kukamatwa na polisi inakuwa halali yenu.