Moderator Hukutakiwa kukerwa na heading niliyoweka , nimekuwekea ninachokijua ndani ya uzi kama ushahidi wa Mbowe kuwa juu ya wazee wetu wa zamani ...
Nimekusoma , tena mara mbili mkuu Erythro ili nihakikishe sikukosa kuelewa ulichoandika hapa.
Kama nia yako ya mada hii haikuwa kuwalenga watani zako, kama ilivyo Simba na Yanga, kichwa cha mada kama kilivyorekebishwa ndio sahihi kabisa kulingana na mada yako.
Lakini kama lengo lako la mada uliyowasilisha hapa lilikuwa ni kusikia watani zako watasemaje, basi huenda kichwa cha mada ulichotumia mwanzo kilikuwa ndiyo bora kwa kazi hiyo ya kuwapandisha mizuka hao watani zako.
Nilisita kuandika haya, lakini imenilazimu niyaweke hivyo hivyo baada ya kuona ulalamishi uliouweka hapa.
Mbowe hawezi kutokua mashuhuri kama anastahiri, kwa vile tu Mandela, Nkrumah au Nyerere walikuwa mashuhuri. Kazi zake zitaonekana na watu watasifu kazi hizo bila kujali analinganishwa na nani, tena kwa nyakati tofauti kabisa!
Nisichoweza kuhoji juu ya mada yako, ni huyu mkoloni mweusi CCM na viongozi wake. Ametokea kuwa mkoloni mbaya zaidi ya yule aliyelazimika kuondoka wakati tunapata uhuru wetu.
Kazi ya kumwondoa huyu mkoloni mpya ni dhahiri itakuwa ngumu zaidi, na itahitaji ushirikiano wa makundi mbalimbali zaidi ya washirika wa utani wa Yanga na Simba.