Maendeleo gani, uchumi umekua zaidi ya watangulizi wake. Naona hotuba ya leo haijaongelea kabisa maendeleo ya kilimo yanayogusa 80 pc ya watanzania.Dawa imewaingia na imekaa kunako
Mapinduzi ya kimaendeleo yaliyofanyika ndani ya miaka minne hii utakuwa mjinga kama ukaendelea kupinga
VIVA Magufuli
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa Mbowe ameenda Mwanza kibwege bwege. Na sio yeye tu, yaani Heche, Mnyika, Sugu, Lema, Boniface waende Mwanza bila kuwa na jambo la maana? Sidhani
Mbowe ni Professor wa siasa AfrikaYaani CHADEMA ni mabingwa wa siasa. Baada ya Mh rais kuwakwepa kuongea nao leo kajikuta ana wapa nafasi ya kumpa ukweli bila yeye kujua ana wapa mwanya. Mbowe amefikisha ujumbe na alie tumiwa ujumbe ameusoma. Nani mjanja? Ccm au CHADEMA kuhudhuria sherehe? Nani katoka na faida? Lumumba semeni!!!
Mbowe na chadema waomba POO kwa JPM. Hii ndio stori.Acha upotoshaji ww mpuuzi, cdm walisema hawatambui uchaguzi wa Zanzibar, na kilichowafanya bungeni ni kwakuwa Dr. Shein alishiriki ufunguzi ule wa bunge. Hata hivyo ushindi wa Magufuli ilikuwa ni utata mtupu. Nampongeza sana Zitto kutoshiriki hiyo sherehe na wahuni. Naalani viongozi wa cdm kushiriki kwenye sherehe pamoja na wahuni wanaonajisi demokrasia yetu.
Ila leo Mbowe kamuita mheshimiwa Rais maana yake keshakubali yaisheLini chadema walimtambua Magufuli Kama Raisi? Kuapishwa walisusa kuwa hawamtambui,bungeni alipoenda Kama Raisi walitoka kumkataa.
Watoe kwanaza tamko la kumtambua Magufuli Kama Raisi.
Wanataka maridhiano na Magufuli Kama Nani kwao ?
Wameenda kuomba POO.. si mchezo JPM.Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa Mbowe ameenda Mwanza kibwege bwege. Na sio yeye tu, yaani Heche, Mnyika, Sugu, Lema, Boniface waende Mwanza bila kuwa na jambo la maana? Sidhani
Hapana kwa kweli sema Mbowe sasa amegundua kwenye kuzira alikuwa anachemka. Kuomba maridhiano maana yake ameinua mikono na kiburi sasa kimeishaMbowe ni Professor wa siasa Afrika
Unaweza kuthibitisha hoja yako hii mahakamani, au ndio ukipandishwa kizimbani unaanza kuji*ea !ny*ea na kutesa familiaUnaenda kumpigia magoti mtu aliyemtandika risasi 38 nduguyo utadhani anaua CHATU na kama haitoshi akaendelea kumshughulikia vivyo hivyo huku akiwa hoi kitandani.
CHADEMA hakuna kitu
Mkuu hapa umetuchapa, msikilize tena Mbowe.Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amempongeza Rais John Magufuli kutokana na juhudi mbalimbali anazozifanya katika kuliongoza taifa.
Huu ndiyo ulikuwa ujumbe wake mkuu kwa Raisi.Akizungumza katika maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya uhuru wa Tanzania bara yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza, katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mbowe amesema kuna ulazima wa kuwepo maridhiano na mshikamano ili taifa lizidi kusonga mbele.
Huu ndio uongo mchana kweupe, wote tumemsikia Mbowe na mpira sasa uko kwa JPM. Amekumbushia jambo ambalo walishaliomba enzi zile za UKUTA.Mbowe amewaacha solemba makamanda
Wanajipendekeza kwa majudge au nani, maana ndio wanaosikiliza kesi.Viongozi wengi wa chadema wameshaambiwa na wanasheria wao kuwa kifungo kipo njiani ndio maana wanajipendekeza ili wapate huruma
USSR
Mbowe na chadema waomba POO kwa JPM. Hii ndio stori.
Sina. Wewe je? Una lingine?Ni kweli, una jingine?
Wameonesha ukomavu wa kisiasa,hakika wamekuwa kisiasa siyo kupinga pinga hata vitu vyenye maslahi kwa nchi na kujifanya kuzila zila kila kituMwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amemtaka Rais Magufuli kuleta maridhiano ya kitaifa na kwamba yeye na chama chake wamenyoosha mkono wa mapatano
Ifuatayo ni Hotuba Fupi ya Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini Tanzania Freeman Aikael Mbowe mbele ya Watanzania katika kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru:
Mheshimiwa Rais,
Waheshimiwa viongozi wote mlioko mahali hapa,
Waheshimiwa watanzania wenzangu!
Nimekuja kushiriki sherehe za miaka 58 ya Uhuru kama uthibitisho wa ulazima wa kuwepo maridhiano, kuwepo upendo, na kuwepo mshikamano katika Taifa letu.
Nawapongeza sana watanzania kwa siku hii ya leo na ninamuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama Taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu demokrasia. Tukajenge Taifa lenye upendo na mshikamano.
Na Mheshimiwa Rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika Taifa kwani kuna wengine wanalalamika, wengine wanaumia. Basi Mheshimiwa Rais tumia nafasi hiyo ukaliweke Taifa katika hali ya utengamano.
Nakushukuri sana. Asante sana.
_____________
Hotuba fupi ya Mwenyekiti wa CHADEMA na KUB, Mh *Freeman Mbowe* katika sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, zilizofanyika Jijini Mwanza leo 9 Disemba 2019
View attachment 1286525
Na ndiyo imefunika kabisa sherehe za uhuru.Naweza kusema Nchi inajadili Horuba ya Mbowe kwa sasaHotuba ya Mbowe yafunikwa kwa mbali sana hotuba zote za siku ya uhuru
Sina. Wewe je? Una lingine?
Unaweza kuthibitisha hoja yako hii mahakamani, au ndio ukipandishwa kizimbani unaanza kuji*ea !ny*ea na kutesa familia
Kwa hyo mlivyosusia uchaguzi wa serikali za mitaa??
Hakika !Na ndiyo imefunika kabisa sherehe za uhuru.Naweza kusema Nchi inajadili Horuba ya Mbowe kwa sasa