Freeman Mbowe: Rais leta maridhiano ya Kitaifa, sisi CHADEMA tuko tayari
Mbowe alionyesha kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli ku kuwataka watanzania wapendani ili kuendelea kuleta maendeleo kwani maendeleo hayana vyama.

Hongera sana KUB Mbowe.

Naunga mkono 5 tena kwa Mbowe!
Juhudi za Magufuli ni kufarakanisha Taifa, anataka Tanzania nayo iwe kama Kwao Burundi, Viongozi wenye akili na Mapenzi mema kwa Taifa kama Mheshimiwa Mbowe wanajitokeza kumkanya!
 
Mbona wapinzani wamekua wakiingia ikulu miaka nenda miaka rudi? Wanaalikwa kila siku na wapinzani wengine huudhuria kwa wingi tu, hao walisusia shughuli zote za kimaendeleo na serikali

Kuanzia kutomtambua Rais, kutoka bungeni nk

Wacha kujitoa ufahamu, nenda kwenye huu uzi ukaelimishwe na Watanzania wenzako
 


Hakika wahenga walisema kuwa uyaone! Hotuba ya salamu za Mheshimiwa Mbowe kiongozi wa Chama kikuu cha upinzani Tanzania Leo hii uwanja wa CCM Kirumba imewaacha sio wanachadema tuu hadi wanaccm na watu wengine pia mdomo wazi.

Hakuna aliyetegemea Mbowe angezungumza kijasiri namna ile katikati ya Wapinzani wake na watesi wake na bila kutegemea angepewa nafasi hiyo. Ukiangalia viongozi wengine waupinzani na hata wale mawaziri wakuu wastaafu waliokuwa upinzani walizungumza katika hali ya kuchanganyikiwa na kusifu tuu, huku Sumaye akiita hii ni awamu ya tatu ile ya kwake.

Salamu zilizo enda kwa Magufuli zimewasilishwa katika hali ya unyenyekevu na heshima anayostahili Rais yeyote muelewa hivyo kama Magufuli atashindwa kuzifanyia kazi lawama ni zake sio za kundi analog wakilisha Mbowe.
Binafsi kama mheshimiwa Rais ataheshimu heshima aliyopewa na Mbowe na kubadilika, nami Nita badilika na katika mtazamo juu yake.

Leo hakukuwa na kejeli wala vijembe kama vya yule zuzu wa mzizima.
Tuheshimiane!
 
Kiukweli pamoja na kupinga Mbowe kwa u Mugabe wake lakini kwa hili namkubali sana.
 
Chadema wanasikitisha. They are so naive, yaani wanaamini kabisa huyo mtu atabadilika.
Taifa halihitaji maridhiano yoyote! Haki ndio inahitajika.
Tunahitaji katiba mpya na tume huru ya chaguzi.
 
Lini chadema walimtambua Magufuli Kama Raisi? Kuapishwa walisusa kuwa hawamtambui,bungeni alipoenda Kama Raisi walitoka kumkataa.

Watoe kwanaza tamko la kumtambua Magufuli Kama Raisi.

Wanataka maridhiano na Magufuli Kama Nani kwao ?
Siku lowasaa aliporejea nyumbani
 
Watu wanamakovu makubwa na kama atashupaza shingo basi tushukuru kwa yote.
 
Swala la amani ya taifa letu nafikiri karibu kila Mtanzania mwenye akili timamu analiunga mkono.

Sasa sioni ajabu kwa Mh. Mbowe naye kusapoti swala la amani.

Ila the problem is nyie vichaa wa ccm mnafikiri mbowe anasapoti ujinga na madudu yenu ccm inayoyafanya awamu hii ya 5.
Kitu kilichonifurahisha leo pale kirumba stadium ni itifaki ya ukaaji.

KUB Mbowe alikuwa katikati ya Dr Bashiru na Mzee Mangula kwa upande mmoja na Prof Lipumba kwa upande mwingine.

Mzee Sumaye alikuwa na wazee wenzie Pinda na Lowassa.

Lakini kilichonifurahisha ni namna mh Mbowe na Dr Bashiru walivyotumia muda mwingi wa uwepo wao pale kiwanjani kuteta mambo mbalimbali ya kitaifa na ya vyama vyao. Hata aliposimama kusalimia Mbowe alionyesha kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli ku kuwataka watanzania wapendani ili kuendelea kuleta maendeleo kwani maendeleo hayana vyama.

Hongera sana KUB Mbowe.

Naunga mkono 5 tena kwa Mbowe!
 
Kuna wakati niliona Mheshimiwa dr Bashiru akimtajia namba ya simu Mheshimiwa mwenyekiti wa Chadema.
Nilibaki najiuliza ni kweli hawa watu walikuwa hawana mawasiliano baina yao au naona vibaya?
Naamini kuwa, kuwa vyama tofauti siyo uadui sasa iweje watu hawa wawili ambao kwa namna moja au nyingine taifa linawategemea wakose kuwa na mawasiliano baina yao kwa muda wote huu waliokaa kwenye uandamizi wa siasa?
Wewe ndii umesema kweli. Hata mimi niliona hilo la kupeana namba za simu.
 
Yaani CHADEMA ni mabingwa wa siasa. Baada ya Mh rais kuwakwepa kuongea nao leo kajikuta ana wapa nafasi ya kumpa ukweli bila yeye kujua ana wapa mwanya. Mbowe amefikisha ujumbe na alie tumiwa ujumbe ameusoma. Nani mjanja? Ccm au CHADEMA kuhudhuria sherehe? Nani katoka na faida? Lumumba semeni!!!
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amemtaka Rais Magufuli kuleta maridhiano ya kitaifa na kwamba yeye na chama chake wamenyoosha mkono wa mapatano

Ifuatayo ni Hotuba Fupi ya Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini Tanzania Freeman Aikael Mbowe mbele ya Watanzania katika kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru:

Mheshimiwa Rais,
Waheshimiwa viongozi wote mlioko mahali hapa,
Waheshimiwa watanzania wenzangu!

Nimekuja kushiriki sherehe za miaka 58 ya Uhuru kama uthibitisho wa ulazima wa kuwepo maridhiano, kuwepo upendo, na kuwepo mshikamano katika Taifa letu.

Nawapongeza sana watanzania kwa siku hii ya leo na ninamuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama Taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu demokrasia. Tukajenge Taifa lenye upendo na mshikamano.

Na Mheshimiwa Rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika Taifa kwani kuna wengine wanalalamika, wengine wanaumia. Basi Mheshimiwa Rais tumia nafasi hiyo ukaliweke Taifa katika hali ya utengamano.

Nakushukuri sana. Asante sana.
_____________
Hotuba fupi ya Mwenyekiti wa CHADEMA na KUB, Mh *Freeman Mbowe* katika sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, zilizofanyika Jijini Mwanza leo 9 Disemba 2019
View attachment 1286525
 
Huu ndiyo upotoshaji uliopo ktk watu wanaojiita wadau wa siasa Tz, Mbowe kuongea na mtu wa chama kingine wala siyo story kabisa...........sisi wote ni watz na inawezekana wana mahusiano mengine nje ya vyama........
 
Kitu kilichonifurahisha leo pale kirumba stadium ni itifaki ya ukaaji.

KUB Mbowe alikuwa katikati ya Dr Bashiru na Mzee Mangula kwa upande mmoja na Prof Lipumba kwa upande mwingine.

Mzee Sumaye alikuwa na wazee wenzie Pinda na Lowassa.

Lakini kilichonifurahisha ni namna mh Mbowe na Dr Bashiru walivyotumia muda mwingi wa uwepo wao pale kiwanjani kuteta mambo mbalimbali ya kitaifa na ya vyama vyao. Hata aliposimama kusalimia Mbowe alionyesha kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli ku kuwataka watanzania wapendani ili kuendelea kuleta maendeleo kwani maendeleo hayana vyama.

Hongera sana KUB Mbowe.

Naunga mkono 5 tena kwa Mbowe!

Mwenyekiti Mbowe ana hekima na Busara kuliko maccm 20 akiwepo baba jesca
 
Wacha kujitoa ufahamu, nenda kwenye huu uzi ukaelimishwe na Watanzania wenzako
LOL wanielimishe nini sasa?

Wapinzani wanavyohudhuria shughuli za kiserikali kila leo?
 
Lini chadema walimtambua Magufuli Kama Raisi? Kuapishwa walisusa kuwa hawamtambui,bungeni alipoenda Kama Raisi walitoka kumkataa.

Watoe kwanaza tamko la kumtambua Magufuli Kama Raisi.

Wanataka maridhiano na Magufuli Kama Nani kwao ?
HAWAJAENDA PALE KWA AJILI YA RAISI,WAMEENDA KWAJILI YA SIKUKU YA UHURU WA Tanganyika
 
Wewe unataka kulinganisha hali ya uhasama Kenya kuwa sawa na Tanzania?

Ninyi mliuana kwa mamia kwenye machafuko ya kisiasa yaliyochagizwa na ukabila sasa hiyo hali Usifananishe na hizi sarakasi za hide and seek za CCM na chadema


Hatujafika hiyo level yenu
 
Back
Top Bottom