Freeman Mbowe: Rais leta maridhiano ya Kitaifa, sisi CHADEMA tuko tayari
Iddi Amin alipokubaliana na watekaji wandege ya air France 1976, ilitumika njia ya majadiliano ya kumlghai ili ajione anaweza kumbe makanda wa IDF walikuwa kwenye rehearsal kwaajili ya kufanya uokozi.

Asomaye na afahamu.
Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia...............
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amemtaka Rais Magufuli kuleta maridhiano ya kitaifa na kwamba yeye na chama chake wamenyoosha mkono wa mapatano

Ifuatayo ni Hotuba Fupi ya Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini Tanzania Freeman Aikael Mbowe mbele ya Watanzania katika kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru:

Mheshimiwa Rais,
Waheshimiwa viongozi wote mlioko mahali hapa,
Waheshimiwa watanzania wenzangu!

Nimekuja kushiriki sherehe za miaka 58 ya Uhuru kama uthibitisho wa ulazima wa kuwepo maridhiano, kuwepo upendo, na kuwepo mshikamano katika Taifa letu.

Nawapongeza sana watanzania kwa siku hii ya leo na ninamuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama Taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu demokrasia. Tukajenge Taifa lenye upendo na mshikamano.

Na Mheshimiwa Rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika Taifa kwani kuna wengine wanalalamika, wengine wanaumia. Basi Mheshimiwa Rais tumia nafasi hiyo ukaliweke Taifa katika hali ya utengamano.

Nakushukuri sana. Asante sana.
_____________
Hotuba fupi ya Mwenyekiti wa CHADEMA na KUB, Mh *Freeman Mbowe* katika sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, zilizofanyika Jijini Mwanza leo 9 Disemba 2019
View attachment 1286525
Hotuba nzuri sana hii.....,
 
Lini chadema walimtambua Magufuli Kama Raisi? Kuapishwa walisusa kuwa hawamtambui,bungeni alipoenda Kama Raisi walitoka kumkataa.

Watoe kwanaza tamko la kumtambua Magufuli Kama Raisi.

Wanataka maridhiano na Magufuli Kama Nani kwao ?
Utajuaje mbinu za adui usipofanya urafiki naye? Asomaye na afahamu.
 
Kesho Mbowe akisema hataki maridhiano wanaCHADEMA mtakuja kushangilia humu

Kwani wote tunamuunga mkono kwenye hayo maridhiano aliyokwenda kutafuta leo? Mbona alishawishi tukajiandikishe kupiga kura na bado tulimgomea wazi wazi hapa jukwaani? Tuna uwezo wa kutambua mambo bila kufuata anachosema yeye, sana sana tunamuunga mkono anaposema kile kilicho kwenye utashi wetu.
 
Hiki la Akwilina ndio lina wapasua kichwa hawakujua litakuwa gumu kiasi hiki. Sasa wanataka maridhiano kwani waligombana wapi na serekali???
Kikwete aliwaita sana lakini hwapi ,wapinzani wa bongo ni pasua kichwa

Wapinzania watafungwa kwa ishu ya akwilina mambo ya kuomba maridhiano sio time yake

USSR
 
Nenda katunze mahesabu ili isipotee bila habari.
Kuna tetesi mtaani ambazo bado sijazithibisha zinadai hao wapo kwenye mgao wa ruzuku ya chama chenu ambayo matumizi yake yanatiliwa Shaka kila ripoti ya CAG inapotolewa
 
Unaenda kumpigia magoti mtu aliyemtandika risasi 38 nduguyo utadhani anaua CHATU na kama haitoshi akaendelea kumshughulikia vivyo hivyo huku akiwa hoi kitandani.

CHADEMA hakuna kitu
Utajua siku moja kuwa Chadema kuna kitu. tena si muda mrefu. Utashangaa Tibisii wani kuna mtu anatangaza hivi: "Tunaomba watanzania waendelee na shughuli zao kama kawaida. hatuna shida na wananchi, tuna shida na huyu adui wa demokrasia, adui wa utu, upendo, mshikamano, na fashsti mkubwa. Watu hawawezi kuishi kwa hofu kama wapo uhamishoni wakati wenye jukumu la kuwahakikishia ustawi wao tupo.Sasa tumeamua kushika hatamu. Baaada ya miezi sita wananchi watamchagua chaguo lao. Asanteni kwa kunisikiliza na majukumu mema ya ujenzi wa Taifa"
 
mbowe ni kiongozi poa sana .. kwa hotuba hiyo fupi imebeba tafsiri nying sana
 
Hii nchi ina maigizo sana
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amemtaka Rais Magufuli kuleta maridhiano ya kitaifa na kwamba yeye na chama chake wamenyoosha mkono wa mapatano

Ifuatayo ni Hotuba Fupi ya Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini Tanzania Freeman Aikael Mbowe mbele ya Watanzania katika kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru:

Mheshimiwa Rais,
Waheshimiwa viongozi wote mlioko mahali hapa,
Waheshimiwa watanzania wenzangu!

Nimekuja kushiriki sherehe za miaka 58 ya Uhuru kama uthibitisho wa ulazima wa kuwepo maridhiano, kuwepo upendo, na kuwepo mshikamano katika Taifa letu.

Nawapongeza sana watanzania kwa siku hii ya leo na ninamuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama Taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu demokrasia. Tukajenge Taifa lenye upendo na mshikamano.

Na Mheshimiwa Rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika Taifa kwani kuna wengine wanalalamika, wengine wanaumia. Basi Mheshimiwa Rais tumia nafasi hiyo ukaliweke Taifa katika hali ya utengamano.

Nakushukuri sana. Asante sana.
_____________
Hotuba fupi ya Mwenyekiti wa CHADEMA na KUB, Mh *Freeman Mbowe* katika sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, zilizofanyika Jijini Mwanza leo 9 Disemba 2019
View attachment 1286525
 
Acha upotoshaji ww mpuuzi, cdm walisema hawatambui uchaguzi wa Zanzibar, na kilichowafanya bungeni ni kwakuwa Dr. Shein alishiriki ufunguzi ule wa bunge. Hata hivyo ushindi wa Magufuli ilikuwa ni utata mtupu. Nampongeza sana Zitto kutoshiriki hiyo sherehe na wahuni. Naalani viongozi wa cdm kushiriki kwenye sherehe pamoja na wahuni wanaonajisi demokrasia yetu.
Zitto usimwamini sana atakutelekeza na kukuacha kwenye mataa we endelea kumshangilia
 
Nina shaka kama mods wanautaalamu wowote wa kujua maudhui na kuangalia tija ya posts kwa mustakabaliwa wa taifa. Hivi wanatumia vigezo gani kuunganisha posts au kufuta?
 
Lini chadema walimtambua Magufuli Kama Raisi? Kuapishwa walisusa kuwa hawamtambui,bungeni alipoenda Kama Raisi walitoka kumkataa.

Watoe kwanaza tamko la kumtambua Magufuli Kama Raisi.

Wanataka maridhiano na Magufuli Kama Nani kwao ?
Tafakari kabla ya kusema. Wanataka kuweka ushahidi ili siku moja iwe jasification ya hatakayo fuata.
 
Mbona wapinzani wamekua wakiingia ikulu miaka nenda miaka rudi? Wanaalikwa kila siku na wapinzani wengine huudhuria kwa wingi tu, hao walisusia shughuli zote za kimaendeleo na serikali

Kuanzia kutomtambua Rais, kutoka bungeni nk
 
Either with us or against us, hakuna maridhiano na wasaliti.
unaongelea CCM au Watanzania "with us" maana kuna tofauti. Watanzania wengi hawana hata vyama. Waliobaki toa asilimia 36%-40% ya upinzani ndiyo CCM. Hivyo msije mkafikiri kila Matanzania yuko kwenye Chama wengi wetu ni wataifa tu
 
yaan kila kitu matakaga kuji involve tuu, chadema waliaadhimia kwenye kikao chao cha ndani kihudhuria
LOL ni huyu tu ndio yupo desperate na issue za Tanzania

Nope nimesahau

Sio huyu tu, ni wakenya karibu wote, ukienda YouTube kwenye video za JPM ndio wanaongoza ku comment
 
Kwani wote tunamuunga mkono kwenye hayo maridhiano aliyokwenda kutafuta leo? Mbona alishawishi tukajiandikishe kupiga kura na bado tulimgomea wazi wazi hapa jukwaani? Tuna uwezo wa kutambua mambo bila kufuata anachosema yeye, sana sana tunamuunga mkono anaposema kile kilicho kwenye utashi wetu.
Ningekuwa na gazeti langu, Kesho Kichwa cha habari kingekuwa, "Mbowe ashauri mwafaka wa Kitaifa........ halafu huyu mwingine namweka kurasa za ndani huko.
 
Back
Top Bottom