Freeman Mbowe: Rais leta maridhiano ya Kitaifa, sisi CHADEMA tuko tayari
Jamani kukiwa na dalili ya huu ushauri kuzingatiwa mnitonye. Maana ninahisi kuna biashara ya kujaribu kupaka hewa rangi inaendelea.
 
Mbowe anaogopa kufungwa,yaani hata akifungwa miezi watakosa muda wa kujiandaa kwa uchaguzi mkuu
Mbowe anatakiwa kwanza aunge mkono juhudi za Rais wetu.ndipo awezekukaribishwa kwa chai
 
Unaenda kumpigia magoti mtu aliyemtandika risasi 38 nduguyo utadhani anaua CHATU na kama haitoshi akaendelea kumshughulikia vivyo hivyo huku akiwa hoi kitandani.

CHADEMA hakuna kitu
Kwa hiyo ulitaka CHADEMA wafanyeje?.Waingie msituni ili kulazimisha HAKI na Demokrasia?.Kama Taifa tushukuru kuwa na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani mwenye,BUSARA,HEKIMA na UVUMILIVU mkubwa.Vinginevyo........
 
Well done Mbowe!

Ubaya haulipwi kwa ubaya


Mbowe ametumia busara sana
Tukiwa tunaimba Tz ina Amani ni kwa mtindo huu
Upinzani/Chadema big up sana mmelikomboa Taifa kutoka kwenye kumwaga damu
Wanaowabeza hawaelewi
Keep moving mtashinda Tz itarudi kuwa moja tena...
Roho za uharibifu msizipe nafasi
Msg Sent!

#mwenyemasikionaasikie
 
Kesho Mbowe akisema hataki maridhiano wanaCHADEMA mtakuja kushangilia humu
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amemtaka Rais Magufuli kuleta maridhiano ya kitaifa na kwamba yeye na chama chake wamenyoosha mkono wa mapatano

Ifuatayo ni Hotuba Fupi ya Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini Tanzania Freeman Aikael Mbowe mbele ya Watanzania katika kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru:

Mheshimiwa Rais,
Waheshimiwa viongozi wote mlioko mahali hapa,
Waheshimiwa watanzania wenzangu!

Nimekuja kushiriki sherehe za miaka 58 ya Uhuru kama uthibitisho wa ulazima wa kuwepo maridhiano, kuwepo upendo, na kuwepo mshikamano katika Taifa letu.

Nawapongeza sana watanzania kwa siku hii ya leo na ninamuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama Taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu demokrasia. Tukajenge Taifa lenye upendo na mshikamano.

Na Mheshimiwa Rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika Taifa kwani kuna wengine wanalalamika, wengine wanaumia. Basi Mheshimiwa Rais tumia nafasi hiyo ukaliweke Taifa katika hali ya utengamano.

Nakushukuri sana. Asante sana.
_____________
Hotuba fupi ya Mwenyekiti wa CHADEMA na KUB, Mh *Freeman Mbowe* katika sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, zilizofanyika Jijini Mwanza leo 9 Disemba 2019
View attachment 1286525
Haahahaaaa akaombe maridhianoooo sikuya UCHAGUZI WA MWENYE KITI ....
 
Utamu WA Siasa ni kusahau matatizo yako Kwa kaulimbiu vya "Yanga Mbele kurudi nyuma mwiko" ukiangalia Siasa ya Tanzania utagundua kunatatizo la umoja wa kitaifa katika kutatua matatizo na hii inasababishwa na Sifa (Ndiyo maana ni Bora ungekuwa Uhuru wa BINTI MARINGO" kuliko Uchumi:.

Moja ya maandiko ya mwalimu Nyerere alikataza kitu kimoja Tu ambacho hata VIPI hakutakuwa na umoja wa kitaifa "Vyumba vya kupanga havitakiwi" mwisho wa kunukuu Mambo mengine yote "tumetaka wenyewe"

Ni rahisi kusikia "your finding first president fuki" watu wakaanza kutafutà raisi wa kwanza badala fuki ya para ya "hakutakiwi vyumba vya kupanga"

👉👉👉👉 people majibu yote yapo kwenu wenyewe


Mkuu wewe kweli ni SIMPLE MIND!
Huna hazina ya information background.
Refer Mwalimu;
Kutaifisha njia kuu za uchumi(kujitawala kiuchumi)
Viwanda lukuki vya mazao
Mashirika ya umma huduma kwa wote
(ATC,BIC,NBC,BORA shoes,NDC,TISCI,TEMDO,TIRDO,UDA,KAMATA,NARCO etc)
Vyuo vya uchumi na biashara(Busuness college Dsm, SHYCOM, IFM etc)

Na mengine mengi , sijui tusemeje
 
Unaenda kumpigia magoti mtu aliyemtandika risasi 38 nduguyo utadhani anaua CHATU na kama haitoshi akaendelea kumshughulikia vivyo hivyo huku akiwa hoi kitandani.

CHADEMA hakuna kitu
We nawe

Kwa hiyo ulitaka afanyaje
 
Sahihisho:

Kila mara huwa wanaalikwa na nafasi yao huwa ipo siku zote, ila walikuwa wanasusia kama watoto wakisubiri kubembelezwa, sasa wameona wanapoteza zaidi hivyo wameamua kujileta.
BTW, sijasikiliza alichosema Mbowe.

Nakuelewa itakuchukua ujasiri wa hali ya juu na nguvu nyingi mno kumskliza Mbowe hata kwa sekunde tano, ndivyo chuki za kisiasa huwa, haswa kama umezichukulia kibinafsi ukiwa na msimamo mkali.
Mbowe amemuomba rais atumie hii fursa kama mwanzo mpya, mlango umefunguka sasa, rais aweke historia.
Naye Lipumba akasema ni fursa nzuri kwa rais wenu kuboresha demokrasia.

Hata sisi tuliwahi kuwa na misimamo kama hiyo yako, ila taratibu kila mmoja akaweka utaifa mbele na kukumbatiana. Kwa sasa inaeleweka, utakua mkali sana ila taratibu utapata nafuu.
 
Back
Top Bottom