Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Hawakuwepo sababu waligoma kutambua matokeo na kumtambua raisi! Ila leo wamemtambua
Hiyo sherehe ya uhuru ni siku ya utambulisho wa rais?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawakuwepo sababu waligoma kutambua matokeo na kumtambua raisi! Ila leo wamemtambua
iko hivi , Mbowe ndiye mtoa mwongozo na dira ya Taifa
Siku ya kuapishwa rais Magufuli Chadema walisusa Zitto alihudhuria na akampongeza, leo Zitto kasusa Chadema wamehudhuria, ndiyo siasa zilivyo.
Watanzania zaidi ya milioni 25 walioshiriki Sherehe hizo ktk Uwanja wa CCM Kirumba Mkoani Mwanza.
Umesahau Zitto hakutoka bungeni wakati jamaa anahutubia bunge kwa mara ya kwanza kama rais
Asingehudhuria angepelekaje ujumbe wake? Kama walimwalika kumtega huku wakijua atasusa basi wamejiharibia maana hawakutegemea Kama angeenda! Na hata aliyempa nafasi ya kutoa salami alitegemea kusifiwa lakini kapewa ukweli na sura yake ilisomeka vyema kwa maneno aliyoambiwa na Mbowe! Mbowe kaitumia fursa ya kumsema hadharani ambalo mashahidi wameshangilia uwanjani hapa!
Chadema wawashauri wachaga kuwa Wawe na maridhiano na makabila mengine wasijione superior au kuonea watu wasio kabila yao au kujipendelea kwenye maeneo yenye watu wa makabila tofauti iwe maeneo ya kazi,iwe kwenye siasa ndani ya chadema au popote.
Wachaga wanahitaji maridhiano na makabila mengine ndani ya chadema yenyewe ili chadema isionekane Chama Cha wachaga
Fununu zilizopo ni kuwa mishale ya saa kumi jioni watakuwa na kikao Cha maridhiano kitakachoshirikisha cdm's crew, baadhi ya maaskofu, mawaziri wakuu wastaafu na aliyepo, Marais wastaafu na mkulu mwenyewe hapo ikulu ndogo jijini mwanza. Sio kikao Cha kitoto!
Sisi ambao tumeona hali halisi ya madikiteita, Idd Amin, Mbowe ametimiza wajibu wake lakini SAHAU any positive move from a dictatorKuna watu wanahoji, kwanini Kamati Kuu Chadema imeamua kuhudhuria sherehe za Uhuru leo baada ya kususia kwa miaka kadhaa.
Kuna fununu zinasikika zikifanywa na viongozi wa dini na wazee wastaafu kuhakikisha maridhiano yanapatikana baina ya serikali na vyama vya upinzani hasa Chadema, kama ni kweli basi hatuna budi kuipongeza serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli na kamati kuu ya Chadema kwa uamuzi wake huo. Najua Chadema italaumiwa na wengi hasa wahafidhina wasiopenda mabadiliko, lkn kama imeamua kwa misingi ya kujenga umoja wa kitaifa basi tuipe ushirikiano kwa manufaa ya nchi.
Inawezekana ni udhaifu fulani Chadema imeonyesha, lkn kwa jicho jingine inawezekana pia ni ukomavu wa kisiasa na ni mwanzo mzuri kwa umoja wa kitaifa. Kwanini tuumizane kwa kugombea fito.
Nchi jirani ya Kenya kwa kipindi kirefu kumekuwa na mvutano baina ya Serikali ikiongozwa na Mhe. Uhuru Kenyata dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Upinzani Raila Odinga. Lakini baada ya uchaguzi mkuu wa 2017 tumeona juhudi kubwa za wazi za upatanishi zikiongozwa na rais Uhuru mwenyewe, kwa kiasi fulani zimeanza kuzaa matunda na nchi inasonga, ila kwa kufanya hivyo Uhuru amempoteza marafiki wake wengi akiwepo rafiki wake wa karibu Ruto.
Wasiopenda Maridhiano watabeza, wasiotaka amani hawatapenda tukio hili lifanikiwe.
Maendeleo hayana chama.
Kikwete aliwaita sana lakini hwapi ,wapinzani wa bongo ni pasua kichwa
Wapinzania watafungwa kwa ishu ya akwilina mambo ya kuomba maridhiano sio time yake
USSR
Yesu alisema samehe saba Mara sabini. Siku zote kisasi ni cha Mungu mwenyewe.Unaenda kumpigia magoti mtu aliyemtandika risasi 38 nduguyo utadhani anaua CHATU na kama haitoshi akaendelea kumshughulikia vivyo hivyo huku akiwa hoi kitandani.
CHADEMA hakuna kitu
UENYEKITIIII KWENU UMEKUWA WA UKOO KAMA MILA ZA KICHAGA NA KINA MANGIMwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amemtaka Rais Magufuli kuleta maridhiano ya kitaifa na kwamba yeye na chama chake wamenyoosha mkono wa mapatano
Ifuatayo ni Hotuba Fupi ya Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini Tanzania Freeman Aikael Mbowe mbele ya Watanzania katika kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru:
Mheshimiwa Rais,
Waheshimiwa viongozi wote mlioko mahali hapa,
Waheshimiwa watanzania wenzangu!
Nimekuja kushiriki sherehe za miaka 58 ya Uhuru kama uthibitisho wa ulazima wa kuwepo maridhiano, kuwepo upendo, na kuwepo mshikamano katika Taifa letu.
Nawapongeza sana watanzania kwa siku hii ya leo na ninamuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama Taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu demokrasia. Tukajenge Taifa lenye upendo na mshikamano.
Na Mheshimiwa Rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika Taifa kwani kuna wengine wanalalamika, wengine wanaumia. Basi Mheshimiwa Rais tumia nafasi hiyo ukaliweke Taifa katika hali ya utengamano.
Nakushukuri sana. Asante sana.
_____________
Hotuba fupi ya Mwenyekiti wa CHADEMA na KUB, Mh *Freeman Mbowe* katika sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, zilizofanyika Jijini Mwanza leo 9 Disemba 2019
View attachment 1286525