KakaJambazi
JF-Expert Member
- Jun 5, 2009
- 18,804
- 12,227
Kifupi ni kuitwa ikulu na kunywa soda sio?!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna watu wanahoji, kwanini Kamati Kuu Chadema imeamua kuhudhuria sherehe za Uhuru leo baada ya kususia kwa miaka kadhaa.
Kuna fununu zinasikika zikifanywa na viongozi wa dini na wazee wastaafu kuhakikisha maridhiano yanapatikana baina ya serikali na vyama vya upinzani hasa Chadema, kama ni kweli basi hatuna budi kuipongeza serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli na kamati kuu ya Chadema kwa uamuzi wake huo. Najua Chadema italaumiwa na wengi hasa wahafidhina wasiopenda mabadiliko, lkn kama imeamua kwa misingi ya kujenga umoja wa kitaifa basi tuipe ushirikiano kwa manufaa ya nchi.
Inawezekana ni udhaifu fulani Chadema imeonyesha, lkn kwa jicho jingine inawezekana pia ni ukomavu wa kisiasa na ni mwanzo mzuri kwa umoja wa kitaifa. Kwanini tuumizane kwa kugombea fito.
Nchi jirani ya Kenya kwa kipindi kirefu kumekuwa na mvutano baina ya Serikali ikiongozwa na Mhe. Uhuru Kenyata dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Upinzani Raila Odinga. Lakini baada ya uchaguzi mkuu wa 2017 tumeona juhudi kubwa za wazi za upatanishi zikiongozwa na rais Uhuru mwenyewe, kwa kiasi fulani zimeanza kuzaa matunda na nchi inasonga, ila kwa kufanya hivyo Uhuru amempoteza marafiki wake wengi akiwepo rafiki wake wa karibu Ruto.
Wasiopenda Maridhiano watabeza, wasiotaka amani hawatapenda tukio hili lifanikiwe.
Maendeleo hayana chama.
Vizazi vijavyo vitakuja kushangaa tu ilikuwaje watu wakafanyiwa figisu za hatari kwny uchaguzi wa serikali za mitaa,wakapewa kesi za kutosha mahakamani,mwenzao mmoja mpk akapewa ulemavu wa kudumu na bado watu hao hao wakaenda kwny sherehe iliyoandaliwa na wababe wao na wakitoka hapo bado wataenda kwny hafla kule ikulu ndogo.Kumuomba Jiwe maridhiano haimaanishi kuwa hayo maridhiano lazima uyashuhudie wewe au mimi, bali hata vizazi vijavyo vinahitaji uwanja sawa wa kufanya siasa.
Time wasting discussion. Deductively, you ought to have seen the facts!Acha story leta data mkuu.
Lakini yule waliyemkataa, anawatambua uwepo wao ndio maana kawapa nafasi ya kusalimia Taifa. Tuwe wakomavu tu jamani, hii ni nchi yetu sote!Lini chadema walimtambua Magufuli Kama Raisi? Kuapishwa walisusa kuwa hawamtambui,bungeni alipoenda Kama Raisi walitoka kumkataa.
Watoe kwanaza tamko la kumtambua Magufuli Kama Raisi.
Wanataka maridhiano na Magufuli Kama Nani kwao ?
Vizazi vijavyo vitakuja kushangaa tu ilikuwaje watu wakafanyiwa figisu za hatari kwny uchaguzi wa serikali za mitaa,wakapewa kesi za kutosha mahakamani,mwenzao mmoja mpk akapewa ulemavu wa kudumu na bado watu hao hao wakaenda kwny sherehe iliyoandaliwa na wababe wao na wakitoka hapo bado wataenda kwny hafla kule ikulu ndogo.
Ni maajabu kwa kweli.
Ndiyo muwe na adabu na akili ziwarudie muwache kuropoka hovyoHahahaa kamanda umenichekesha sana..kumbe upo hapo?? Niko na delegation ya diplomats nakuja maeneo hayo
Viva Magufuli, Heko watanzania
Hiyo haijalishi. Kenya walikuwa na mtifuano mkubwa zaidi yetu.... Lakini Leo Uhuru na Laila wanakaa Meza moja.Lini chadema walimtambua Magufuli Kama Raisi? Kuapishwa walisusa kuwa hawamtambui,bungeni alipoenda Kama Raisi walitoka kumkataa.
Watoe kwanaza tamko la kumtambua Magufuli Kama Raisi.
Wanataka maridhiano na Magufuli Kama Nani kwao ?
Haijalishi kwa sababu Mbowe anajifurahisha tu.Haijalishi
Hebu punguza jazbaMbowe hiyo nafasi hakuitumia vizuri angeanza hivi sisi Kama chadema tuna makosa mengi tumeifanyia Serikali ya CCM na Raisi hatuwezi sema sisi hatuna makosa sababu sisi sio miungu.Pia CCM yaweza kuwa imetukosea upinzani kwa kujua au kutojua kwani CCM sio miungu kwa muktadha huo tunaomba maridhiano na kusameheana kuwa kitu kimoja tujenge nchi moja.
Lakini Mbowe alivyoongea ninkana kwamba wao Ni malaika na CCM na Magufuli ndio mashetani wanaotakiwa walete maridhiano ya kitaifa!!!! Wao chadema Ni akina malaika Gabriel na mikael
mnyakiti wa ccm...Wanataka maridhiano na Magufuli Kama Nani kwao ?
Huwezi kutaka maridhiano na mtu anaye kuchukulia poa,anaye kuzidi nguvu na kila kitu na anajua hamna kitu utamfanya.Hiyo haijalishi. Kenya walikuwa na mtifuano mkubwa zaidi yetu.... Lakini Leo Uhuru na Laila wanakaa Meza moja.
Maridhiano wanafanya watu walio more or less kwenye level moja.Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amemtaka Rais Magufuli kuleta maridhiano ya kitaifa na kwamba yeye na chama chake wamenyoosha mkono wa mapatano
Ifuatayo ni Hotuba Fupi ya Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini Tanzania Freeman Aikael Mbowe mbele ya Watanzania katika kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru:
Mheshimiwa Rais,
Waheshimiwa viongozi wote mlioko mahali hapa,
Waheshimiwa watanzania wenzangu!
Nimekuja kushiriki sherehe za miaka 58 ya Uhuru kama uthibitisho wa ulazima wa kuwepo maridhiano, kuwepo upendo, na kuwepo mshikamano katika Taifa letu.
Nawapongeza sana watanzania kwa siku hii ya leo na ninamuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama Taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu demokrasia. Tukajenge Taifa lenye upendo na mshikamano.
Na Mheshimiwa Rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika Taifa kwani kuna wengine wanalalamika, wengine wanaumia. Basi Mheshimiwa Rais tumia nafasi hiyo ukaliweke Taifa katika hali ya utengamano.
Nakushukuri sana. Asante sana.
_____________
Hotuba fupi ya Mwenyekiti wa CHADEMA na KUB, Mh *Freeman Mbowe* katika sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, zilizofanyika Jijini Mwanza leo 9 Disemba 2019
View attachment 1286525
Umenena kweli tupu. Mimi Ni mmoja ninayemwona Rais Magufuli kama mtawala anayetumia si ushawishi kwa watu wa nchi bali mabavu kufanya anachokifanya. Na mbaya kuliko yote, amekuwa ni adui mkubwa wa demokrasia na haki za binadamu changanya na kupata uungwaji mkono wa wazee wasiojielewa kama Mwinyi na Malecela.Magufuli aliyepinda na anaye endelea kupindisha Katiba ya Tanzania ndiye anastahili KUNYOOSHWA…!