Freeman Mbowe: Rais leta maridhiano ya Kitaifa, sisi CHADEMA tuko tayari
Lini chadema walimtambua Magufuli Kama Raisi? Kuapishwa walisusa kuwa hawamtambui,bungeni alipoenda Kama Raisi walitoka kumkataa.

Watoe kwanaza tamko la kumtambua Magufuli Kama Raisi.

Wanataka maridhiano na Magufuli Kama Nani kwao ?
Kama wewe unaona Mbowe hamtambui Magufuli, basi Magufuli anamtambua Mbowe kama Kiongozi wa Kambi ya upinzani nchi kama alivyomwita basi tutumie kutambulika kwake na magu tufanye kazi
 
Natamani siasa zetu ziwe kama upinzani na utani wa Simba na Yanga, sio za kuoneana na kununiana.

Vv
 
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa Mbowe ameenda Mwanza kibwege bwege. Na sio yeye tu, yaani Heche, Mnyika, Sugu, Lema, Boniface waende Mwanza bila kuwa na jambo la maana? Sidhani
Wala usitumie akili nyingi sana .
Kweli JpM anakaba, aidha usalende au uumie, basi. Wamechagua. Huo nao ni ushujaa
 
Either with us or against us, hakuna maridhiano na wasaliti.
Mtu akitoa mkono wa shirika mnyoshee mkono with a benefit of doubt. Kusema tu wasaliti, ni kujihesabia haki wakati sisi tunaona makandokando yako na unafiki wako.

Vv
 
Fafanua hili somo; charity should begin at home- CHADEMA tufanye maridhiano na Wilbroad kwanza

Maridhiano yepi? Wilbroad ni mwanaccm full stop.
Hivi wewe ukikosa maelewano na mkeo na kesho yake tuu anaondoka na kuolewa na jirani utaamini kweli kutokuelewana kwenu kwa Jana ndiko kumesababisha kumpeleka kwa jirani?
Nyerere aliwaita hao ni wanasiasa Malaya
 
Kati ya Viongozi wa Upinzani waliopewa nafasi ya kuzungumza Mhe. Mbowe ndiye amefunika wote kiukweli!
Ameongea kifupi lakini Hoja yake ni nzito na ina mashiko! Hii inakwenda kuwasha moto wa another BBI in Tanzania!

Hapa Magufuli ametegewa mtego wa kiufundi sana! Hiki kitakuwa kipimo kingine tosha kwa Urais wake. Tayari Uchaguzi wa SM umezidi kutia doa Utawala wake wa kibabe!
Wengi hawakuliona hilo Mkuu. Wameshindwa kuelewa kuwa pale kuna Jumuiya mbali mbali za Kimataifa. Kuna ushahidi wa kutosha endapo atayapuuzia kama kawaida yake.
 
Kwani Chadema walishafuta kauli yao ya kutomtambua JPM kama rais wa JMT?
 
Kitu kilichonifurahisha leo pale kirumba stadium ni itifaki ya ukaaji.

KUB Mbowe alikuwa katikati ya Dr Bashiru na Mzee Mangula kwa upande mmoja na Prof Lipumba kwa upande mwingine.

Mzee Sumaye alikuwa na wazee wenzie Pinda na Lowassa.

Lakini kilichonifurahisha ni namna mh Mbowe na Dr Bashiru walivyotumia muda mwingi wa uwepo wao pale kiwanjani kuteta mambo mbalimbali ya kitaifa na ya vyama vyao. Hata aliposimama kusalimia Mbowe alionyesha kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli ku kuwataka watanzania wapendani ili kuendelea kuleta maendeleo kwani maendeleo hayana vyama.

Hongera sana KUB Mbowe.

Naunga mkono 5 tena kwa Mbowe!
 
Safi Sana Mwamba Mbowe TUVUSHE.
Ule wimbo wa POCHI NENE unamaana kubwa sana,yani baba la baba kakata umeme mpaka sasa wameona bora kujisalimisha.....maridhiano [emoji91][emoji91][emoji91]
 
Namshauri Mh. Mbowe aanzishe Maridhiano kwanza ndani ya Chama chake kabla ya kumshauri Mh Rais kuanzia maridhiano ya Kitaifa.Watu wameumizwa sana ndani ya chama kiasi cha kuwaacha wazee kma Prof. Safari na wenzake wakiwa na maumivu makubwa. Wapinzani(Chadema asili) hatujasahau alichofanyiwa rais mstaafu wa Mioyo Kamanda Dr. Wilbroad Peter Slaa. Kuna kila sababu ya kuanzisha reconcilliation kati yetu Chadema Asili na Chadema Maslahi
 
Naona chadema kwenda mwanza ACT kimewakera sana,kuipitia page yao kule Twitter wanaponda sana
 
Bashiru walivyotumia muda mwingi wa uwepo wao pale kiwanjani kuteta mambo mbalimbali ya kitaifa na ya vyama vya
Are you sure walikuwa wanaongelea hayo uliyoyasema? Nilishawahi kusema kuwa Lumumba kuna takataka tupu! How can you dare say such nonsenses? Can you tell for sure what was being discussed by the duo? (labda kama ulikuwa maid wao and therefore you were in close proximity to hear their talk!, which is very unlikely)
 
Hakuna anayemkatazaga mtu kuhudhulia sherehe ila ni strategy za vyama vyenyewe...........mbona vyama vingine miaka yote vinahudhulia?
 
Back
Top Bottom