FT: RS Berkane 2-0 Simba SC | Fainali CAF Confederation Cup | 17 Mei, 2025

FT: RS Berkane 2-0 Simba SC | Fainali CAF Confederation Cup | 17 Mei, 2025

Mpira huwa una matokeo ya kikatili sana
Na Afrika fainal ni mechi ya kwanza ukicheza hovyo mechi ya pili huwa ni sherehe tu.

Uhovyo wa mechi ya pili Afrika huwa ni wa kusikitisha na kuudhi pia maana unaanzia nje ya uwanja mpaka ndani.
 
Umeona goli la offside na yale magoli mawili aliyoyazuia Camara?
Embu chukulia angeshindwa kuwazuia yale mawili na lile la offside lingekua goli.
Camara amewaokoa sana ila back line ya Simba hamkuweza kuzuia kitu.
Mtu anatambuka watu wanne!??
Alooo!
Sasa mzee tuanze kuzungumzia magoli ambayo hayakukubaliwa? Mbona Barça walidhulumiwa magoli game yao na Inter na bado hawakutoboa nusu fainali
 
Yaani nyie mafara wa jangwani tukishinda game ya Tz sijui mtaficha wapi sura zenu
Tatizo mtani siyo kushinda.
Mtashinda ngapi?
Mtaweza kubana pale nyuma au mtamruhusu mwarabu awaguse?
Angalia goli la pili la leo, walinzi watano wa Simba dhidi ya mshambuliaji mmoja yupo katikati yao kawageuza.
 
Mechi ya mkondo wa pili naomba hata serikali ya zanzibar waseme amani complex una tatizo kipindi cha jua unakuwa mgumu sana ili mechi ikachezwe hata Sudan kule.... Maana walah tutapata aibu.😂😂😂😂
 
Watarudia wamelowa chaps chaps.
Mwarabu siyo mtu mzuri.
Na wameloa na mvua yaan wanachapwa na mvua juu inawachapa hakuna cha kusema mvua ikinyesha basi Simba inashinda sio kule kwa Amani kule Simba wanachezea tena wanatiwa 2 saafi
 
We jamaa bhana nimekufwatilia sana,inaonekana mpira unaujua kiundani,maana mambo mengi huwa unaeleza kiufundi na yanatokea,lakini swali langu kwako ni hili,hivi game ya nyumbani tukisema Mutale asimame kama namba 10, sababu ana Kasi,ni mbunifu na anatoa pasi haraka kwa wenzake huku pia anakaba haraka timu ikipoteza mpira,halafu pembeni yake 7 asimame Mpanzu kwasababu na yeye ana Kasi,ni mbunifu na anatoa mipira Kwa haraka,halafu namba 11 aanze Kibu au Chasambi,namba 9 asimame Mukwala,nimepanga hivyo sababu tunahitaji goal nyingi yani 3,lakini pia Ahoua aanze benchi maana ni mzito,mchoyo na hana ubunifu,naomba kuskia maoni yako brother
Unajua kuona matukio uwanjani yanayofanywa na wachezaji ni jambo lingine

Na kuunganisha matukio hayo kama mbinu yenye chemistry ya kuweza kuwapa matokeo ni jambo jingine.

Ugumu huo unaoonekana hapo ndio watu sasa wanaona wamuajiri mtu special aliyeenda kusomea mambo hayo wakampa jina la Kocha.

Japo ni kweli tunaweza kuona na kukosoa mbinu za mwalimu katika baadhi ya scenario ila bado kocha anakuwa na nafasi kubwa sana ya kuaminiwa kulingana na kile anachokiona kwenye mazoezi na maelekezo anayowapa wachezaji.

Mfano kocha wa zamani wa Ajax na Barca alikuwa na falsafa yake ya "Total football" ambapo wachezaji walihamasishwa kucheza kwa nafasi na siyo tu kufunga.

Sasa huwenda tunayoyaona sisi sio malengo au falsafa za mwalimu hivyo tukawa tunautizama mpira katika jicho jingine tofauti na kocha.
 
Na Afrika fainal ni mechi ya kwanza ukicheza hovyo mechi ya pili huwa ni sherehe tu.

Uhovyo wa mechi ya pili Afrika huwa ni wa kusikitisha na kuudhi pia maana unaanzia nje ya uwanja mpaka ndani.
Mbona Yanga walikaza game ya pili na walikuwa wanakaribia kutoboa
 
Actually goals 2 sio nyingi ila shida ni matumizi ya nafasi kwa simba. 6 chances 1 goal
 
Back
Top Bottom