FT: Simba 0-3 Raja Casablanca | CAF Champions League | Estadio Benjamin Mkapa | 18.02.2023
Hiyo penati hata sijaiona nilikuwa katika harakati za kutoka uwanjani

Ila nilichojifunza mashabiki inabidi tubadilike sana

Wakati natoka nje hapa kwenye hizi ngazi uwanjani nimestuka na kelele za watu waliokuwa wanamkinbiza mtu wakimuita mwiz

Alikuwa ni dogo tu maskini watu wamemzinga wamepiga kipigo kikali watu wakijua ni mwizi

Lakini mwisho wa siku kumbe dogo alikuwa anashangilia penati ya Raja

Wamemuumiza sana dogo anavuja damu hata nguvu ya kusimama amekosa

Dear friends timu yako kama haichezi kwa Mkapa sio sehemu salama wewe kwenda ukifikiri utakuwa huru kushangilia wapinzani wako wakifungwa kama ukiwa mtaani au humu jukwaani
Watanzania tuna vichaa kufungwa ni kawaida, hata kama kwa idadi si wa kwanza sisi.
 
Back
Top Bottom